Kati ya IT(Information Technology) na Computer Science je ni kozi ipi Ina fursa zaidi na inaongoza kwa watu wengi waliofanikiwa?

Mimi ni miongoni mwa watanzania wachache kuanza kusoma IT kwa ngazi ya chuo kikuu japo sikuhitimi 1998.
Hizi course kwa Africa ni majina tu huwezi kuzitofautisha kuanzia content mpaka practice yake
 
Hizo kozi ni majina tu ila contents zake inafanana
- Je zinafanana kwa mtaala wa wapi?
1731134977516.png

cc Davidmmarista
 
Nipe tofauti ya haya:
Computer Science
Computer Engineering
Computer Programming
Information Technology
Information and Communication Technology
Computer coding
Software Engineering

Computer Science
Computer Engineering
Software Engineering
Kwa upande wa kwenda kufanya kazi tofauti ni ndogo sana hawa wote wataenda kufanya kazi ile ile ya kutengeneza software za aina mbali mbali hakuna kampuni ya tech inayojali wewe umesoma CS au CE etc. Pia hii ni job title inayotegemea kampuni na nchi, unaweza ukawa software engineer kampuni moja ukahamia nyingine ukaitwa computer programmer, developer, ninja etc wakati kazi ni ile ile, kuna nchi haurusiwi kujiita engineer hadi uwe unefanya certification.
Aliyesoma CE labda ana chance kubwa zaidi kwenye kazi zinazogusa hardware.

Kwa upande wa academics kunaweza kukawa na tofauti za hapa na pale CE mara nyingi kutakuwa na kozi zaidi za Engineering hasa electronic. Ila angalia syllabus.

Computer Programming na
Computer coding ni kitendo cha kufanya programming sidhani kama inahusiana na haya mengine.

Information Technology.
Information and Communication Technology.

Hizi mbili nazo hazina tofauti kubwa, IT ni mwamvuli mpana zaidi ambao unaweza kulenga karibia kitu chochote ambacho kipo chini ya "technology" kwa nchi za wenzetu IT mara nyingi wanadeal na computer na service wanazotumia wafanyakazi wa kampuni so kama nahitaji laptop mpya au nashindwa kuingia email account yangu naongea na IT.

Kwa upande wa academics inabidi uangalire syllabus utakuta shule moja inafundisha IT nyingine ICT lakini syllabus ni ile ile, wenye Communication inaweza ikawa ina kozi zaidi za technolojia za communication. Mara nyingi IT sio degree course ni practical zaidi sio academic.
 
Waliosoma wote ndio tupo tunapiga window huku.

Ukiwa na akili za ziada utajikuta umekua fundi simu upande wa software.

Kuhusu kufanikiwa usitegemee kabisa maana hizo kazi hawaajiri beginers, wanataka wazoefu haswa.

Na uzoefu maana yake ni kwamba, Maliza Chuo leo na Degree yako then sugua benchi kwa kujitolea sehem tofaut tofaut kwa miaka hata 10 then ndipo utafute ajira.

Ki ufupi hiyo Kitu naifananisha na SIASA bila mtu aliekutangulia anaekujua kukushika mkono kukupa kitengo.

Jiandae Kuja Kuwa Fundi Simu au Computer
Hahaha, wako waliotoka na wana mafanikio makubwa tu
 
IT nikwajili ya kudeal na mifumo ambayo imeshatengenezwa, kuhakikisha inafanya kazi vizuri. Kutoa mapendekezo itumike mifumo ipi kwajili ya shughuli ipi, kurekebisha mifumo n.k

Computer Science
Ni kwajili ya kudesign na kuunda mifumo mbali mbali kama Operating system, Programming languages, Software za kufanyia kazi kama Adobe n.k

Computer Engineering
Nikwajili ya kuunda mifumo na hardware vitavyofanya kazi kwa pamoja, huyu anaweza kutumia programming language ambayo imekuwa designed na kuundwa na mtu wa computer science ili kutengeneza seti ya maelekezo ambayo mfano itawekwa kwenye ATM machine kwajili ya kumuhudumia mteja.

Anaweza pia kutumia mifumo iliyopo kutengeneza seti ya maelekezo itayofanya kazi kwenye roboti n.k

Nimejaribu kujibu
 
Mimi ni miongoni mwa watanzania wachache kuanza kusoma IT kwa ngazi ya chuo kikuu japo sikuhitimi 1998.
Hizi course kwa Africa ni majina tu huwezi kuzitofautisha kuanzia content mpaka practice yake
Ahh nilisoma miaka 2000s, mpaka nakuja kupata masters hazijafanana. Ntakuambia kitu kimoja Cs iko so deep na imelenga kutengeneza wataalam zaidi waka IT imelenda kutengeneza users,admins
Cs ana pacha mwenzei anaitwa Computer engineering huyu yeye analala zaidi kwenye hardware (although wanapiga software pia but si deep kama CS)

Mitaala hubalika kila baada ya muda fulani so na mambo huanza kujitenga.
Japokuwa kwenye ajira za bongo tofauti ni ndogo, ila kwa huku nchi za nje wako specific

Hawachanganyi kabisa haya mambo
 
Uko sahihi kwa wenzetu ni vitu tofautiila kwa bongo tofauti ni ngumu kuiona,hata chuoni first year tulisoma masomo yanayofanana,maelezo yako mengine yako sawa
 
Wadau msaada

Je, kati ya IT(Information Technology) na Computer Science je ni kozi ipi Ina fursa zaidi na inaongoza kwa watu wengi waliofanikiwa?
Pia zingatia CS ni degree miaka 3-4, IT degree sidhani kama nimewahi kuona ni diploma mara nyingi au short kozi, so degree utakula gharama mara nyingi na cost ya huo muda, CS ni science of computing ni academic sana ndo maana kuna shule zinafundisha lugha ambazo zineshakufa duniani, usipoangalia unaweza kutoka bila skills zinazohitajika kazini, ila siku hizi mambo yanabadilika shule zinajaribu kuwa practical zaidi. Degree inaweza kufungua milango mingi zaidi kuna wapumpavu hawaangalii CV kama haina degree pia kama ukitaka kwenda nje bila degree njia ni chache sana. So yote yana + na -.
 
Soma chochote bro! Inategemea na fulsa zilizopo, taasisi nilipo, ya UN, Nirifikili nikiingia kama engineer, nitapiga pesa ndeeefu, kuliko wote, waaapi, tunakimbizwa na vijana wadogo wenye degree za political science, mazingira, mass communication, geopolitical security,
Inategemea,
 
Pia zingatia CS ni degree miaka 3-4, IT degree sidhani kama nimewahi kuona ni diploma mara nyingi au short kozi, so degree utakula gharama mara nyingi na cost ya huo muda, CS ni science of computing ni academic sana ndo maana kuna shule zinafundisha lugha ambazo zineshakufa duniani, usipoangalia unaweza kutoka bila skills zinazohitajika kazini, ila siku hizi mambo yanabadilika shule zinajaribu kuwa practical zaidi. Degree inaweza kufungua milango mingi zaidi kuna wapumpavu hawaangalii CV kama haina degree pia kama ukitaka kwenda nje bila degree njia ni chache sana. So yote yana + na -.
Kwa hiyo COBOL na PASCAL hazihitajiki siku hizi? Kama nimekuelewa vizuri
 
Kazi za COBOL na PASCAL ni karibia zero, kuna system za zamani baadhi ya mashirika hasa ya uma unaweza kuzikuta lakini wanataka watu wenye experience hauwezi kupata hiyo kazi kama ndo umetoka chuo, pia utaona kuna news story zinatokea kuwa kuna upungufu wa programmers wa COBOL kwa vile wengi wanastaafu lakini ukweli ni kwamba hawalipu mishahara inayofanana na tech za kisasa ndo maana hakuna anayetaka.
 
C++ nadhani at least deal lake ni kubwa sana
 
Waliosoma wote ndio tupo tunapiga window huku.

Ukiwa na akili za ziada utajikuta umekua fundi simu upande wa software.

Kuhusu kufanikiwa usitegemee kabisa maana hizo kazi hawaajiri beginers, wanataka wazoefu haswa.

Na uzoefu maana yake ni kwamba, Maliza Chuo leo na Degree yako then sugua benchi kwa kujitolea sehem tofaut tofaut kwa miaka hata 10 then ndipo utafute ajira.

Ki ufupi hiyo Kitu naifananisha na SIASA bila mtu aliekutangulia anaekujua kukushika mkono kukupa kitengo.

Jiandae Kuja Kuwa Fundi Simu au Computer
Duh Acha kututisha
 
Back
Top Bottom