Kati ya kitimoto na kuku wa kienyeji, ipi tamu zaidi?

Watu wanaacha kula uhondo huu kisa mwarabu kawaambia. Kila jamii ilikuwa na Mila za zamani za makatazo ya nyama Fulani au sehemu ya nyama na sio maelekezo ya Mungu ni mambo ya Mila tuu. Haya makabila ya hapa bongo Kuna watu hawali wanyama Fulani wengine wanakula
Haya sasa!
 
NAKAZIA!
Halafu upate kitimoto yenye vinyweleo kwa mbali😋
Halafu kwanini kitimoto ukila maeneo ya kishua hainogi? Kitimoto uipate pale kwa Shirima Mianzini Arusha, usafi haueleweki nzi kibao mnafanya kuwafukuza halafu kuna kama ka-mtaro ka maji kanapita Shirima anamwagia maji machafu hapo. Yaani inanoga balaa.
 
Hiyo ni ngumu "kumesa"
 
Somewhere in Kigogo Sambusa....

Katika utulivu wa hali ya juu najiuliza haya maisha yangekuwaje bila kitimoto rost, ndizi mbili na kachumbari pembeni? Kungekua na mbadala wake?.... nikiwa ndani ya tafakuri nzito, namwona Dada nadhifu na mrembo akisogelea mezani kwangu kashikilia sinia lenye kitimoto safi imeiva kiwango cha juu.. ni ufundi wa Shirima. Anafika na kuninawisha mikono kisha kutenga vitu na kuanza kuondoka kwa madaha na sinia. Wakati akiondoka namsihi aniletee Mirinda Nyeusi ya baridi.

Basi kazi ikaanza taratibu, yaani one-touch, finyango baada ya finyango. Ile ndo mwendo unaanza kushika kasi, mara ghafla simu ikaanza kuita..... nikajiuliza kwa hasira ni nani huyu anayeweza kunipigia nikiwa kwenye starehe kama hii??..😬😡😡..

Sasa wakati naitoa simu mfukoni kwa bahati mbaya ikaniponyoka.... kwenye harakati za kuiwahi isianguke nikajikuta nimesukuma ile meza ya plastic.... KITIMOTO yote na ile soda ikamwagika.. Aaarghh!!😬😬.. kuja kukaa sawa tayari yule mdada kashafuta meza na kusafisha pale chini huku akidai chake......
 
Kitimoto ni namba nyingine braza, halafu uzuri wa ile nyama yenyewe tu ni chakula hihitaji ugali au ndizi hata ukiamua kuichapa yenyewe inanoga tu.

Uzuri mwingine wa yule mnyama hamna kinachotupwa, mpaka ngozi na kwato vinaliwa pamoja hata bila kutenganisha sio kama wengine mpaka wachunwe sijui ngozi ikaushwe nk nk.
 
Nimechekaje😃

Wewe ni mtunzi mahiri!
 
Kitimoto ni namba nyingine braza, halafu uzuri wa ile nyama yenyewe tu ni chakula hihitaji ugali au ndizi hata ukiamua kuichapa yenyewe inanoga tu.

Uzuri mwingine wa yule mnyama hamna kinachotupwa, mpaka ngozi na kwato vinaliwa pamoja hata bila kutenganisha sio kama wengine mpaka wachunwe sijui ngozi ikaushwe nk nk.
📌🔨
 
Back
Top Bottom