Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Hapa kibabe sanaNitaacha watangulie kwenda kwenye gari alaf mi nitafuatia baadae nitakavyokuta wamejipanga ndo tutaenda hivyo hivyo
Safi sana hapa umeuaKwangu ni kitu kidogo Sanaa,akae mbele apendavyo huyo mama,shida Moja wanawake tunapenda sometimes kushindana na mama wakwe Kwa vitu vidogo Sanaa..yaani Mimi mama mkwe honestly hanipi shida!!
Ni ujinga kushindana kukaa mbele kwenyw gari,we km mke jiongeze tu mpishe tu akae kwani kwanza mama hakai mda mrefu ataondoka ni WA kupita kushindana na mtu wa kupita ni ujinga tu
Sent from my Infinix X657 using JamiiForums mobile app
SWALI ZURI,KATI YA MAMA NA MKE NANI ANAPASWA KUKAA SITI YA MBELE WAKATI UNAENDESHA GARI?
Anaandika, Robert Heriel
Rafiki yangu Hosea amenipigia simu akaniuliza hivi; Kati ya Mama yake na MKE wake Nani anastahili kukaa SITI ya MBELE ya GARI wakati yeye(Hosea) anaendesha Gari? Nikaona niilete mada Hii kwenu. Ili tujifunze wote.
Imekuwa ni kawaida ya Watu kutaka kuwalinganisha MAMA na MKE kuwa Nani zaidi ya mwenzake.
Nataka kusema kuwa ni makosa makubwa kulinganisha vitu au Watu wasiolingana. Mke ni daraja jingine na Mama ni Daraja jingine.
Pili, Kati ya MKE na Mama hakuna aliyebora zaidi ya mwenzake isipokuwa ubora wao utapimwa Kwa namna watakavyo au walivyotekeleza majukumu yao Kwa nafasi zao. Mama kuzaa pekee yake haimfanyi kuwa Bora isipokuwa yapo majukumu mengine kama malezi. Halikadhalika MKE kukuzalia Watoto pekeake haitoshi kumfanya awe Bora kwako isipokuwa majukumu yake Kwa Watoto pamoja na wewe kama mumewe.
Kama utapima uzito wa majukumu ya MKE na Mama bila kujali madaraja Yao basi utagundua MKE ni zaidi ya Mama, na hapo nazungumzia kimajukumu na kiwajibu. Hata hivyo hiyo haimfanyi MKE kuwa Bora zaidi ya Mama.
Asubuhi nilitoka kuelezea mada isemayo Watu Maskini na wajinga hupenda kuongozwa na Mitazamo na Maoni ya Watu zaidi kuliko Kanuni na sheria. Kama tungefuata Kanuni na sheria Hilo swali lisingekuwepo na haya mambo ya kulinganisha MKE na Mama yasingekuwepo. Kwa sababu Kanuni na sheria zipo wazi kabisa.
Rafiki yangu Hosea aliponiuliza swali hilo nilimjibu Kwa kumuuliza maswali yafuatayo;
1. Nikamuuliza; Kitandani mwako unalala na Nani?
Mbona haukuniuliza Kati ya MKE na Mama yako Nani ambaye utalala naye kitanda kimoja?
Akaguna, akasema hayo mambo ni tofauti na mambo ya SITI za magari.
2. Nikamuuliza, Kati ya Mama na MKE wako Nani anaitwa Mrs. Hosea? Akajibu MKE wangu.
3. Nikamuuliza, Wakati Mama yako anakaa SITI ya MBELE na wewe, je Mkeo atakaa nyuma na Baba yako(mkwewe)? Yaani Wakati Mama yako anang'ang'ania kukaa SITI ya mbele, Baba yako anakuwa yupo wapi au mumewe anakuwa yupo wapi?
4. Nikamuuliza, Watoto wako watakubali Mama Yao(Mkeo) umuweke Nyuma ilhali wewe ndiye mume wake(Baba Yao)? Huoni utajenga kitu kwa Watoto kuwa humpendi Mama Yao na umemuweka katika nafasi ya pili?
Huoni hiyo itakuathiri Huko baadaye Watoto wakikua?
Hata hivyo mtu yeyote anaweza kukaa SITI ya MBELE iwe Mama au MKE au mtoto itategemea Kwa maana hayo ni mambo madpfp ila kama kuna mazingira ya kuonyesha Nani anastahili kukaa MBELE basi MKE ndiye anayestahili. Maana kuna Wamama wengine wanachokochoko Sana. Kumzaa MTU hakukupi Haki ya kuvunja itifaki ya nature na kumfanya MTu uliyemzaa kuwa mtumwa. Nafasi lazima ziheshimiwe.
Kisheria na kikanuni, kwenye familia mama na Baba anashika nafasi ya tatu Huko kama sio ya nne. Kwa mtiririko huu.
1. Mume na MKE.
Hawa ndio nafasi ya Kwanza. Yaani MKE lazima Ampe mumewe nafasi ya Kwanza halikadhalika na Mwanaume/mume lazima Ampe Mkewe nafasi ya Kwanza katika familia.
2. Watoto
Hawa ndio wanashika nafasi ya Pili. mume na MKE huhangaika Kwa Ajili ya Watoto wao kuwalea mpaka wakikua.
3. Wazazi
Baba na Mama. Hawa ndio hushika nafasi ya tatu katika mahusiano ya familia. Baba na Mama yako ni familia nyingine yenye uhusiano wa karibu wa kidamu na ninyi. Ila haina maana wao ndio wawe namba moja.
4. Ndugu
Hawa ni wale mliozaliwa pamoja iwe Baba mmoja, Mama mmoja, mtoto wa Mama mkubwa au mdogo, wajomba, mashangazi n.k.
5. Jamaa
Hawa ni wale wenye undugu wa mbali, undugu wa Tochi.
6. Marafiki.
Hawa ni wale ambao hamna undugu lakini mnaukaribu na mahusiano mazuri.
Zingatia Watoto utakaowazaa wewe kwako ni namba mbili lakini wakishakua na kuanzisha familia wao watakuweka namba tatu. Na wajukuu watakuwa nafasi ya nne Huko, hivyo unakosa mamlaka ya kuingilia familia zao labda wakuombe ushauri.
Jukumu kubwa la mzazi ni kuwalea Watoto wake katika miaka yote ya uhai wake. Lakini sio kudai nafasi zisizo zako. Jukumu la mtoto ni kuwaheshimu wazazi wake, kwa kusikiliza mashauri Mema.
Kama Mama yako anakupenda Sana basi atapaswa aonyeshe upendo huo Kwa Baba yako mzazi. Yaani abaki kwenye nafasi yake. Nafasi ya mume wake asikupe wewe. Wala wewe usimpoke Baba yako nafasi yake Kwa Mama yako. Kila mmoja abaki kwenye nafasi yake.
Baba yako ndio anapaswa kumfanya Mama yako namba moja na sio wewe. Kumfanya Mama yako namba moja ni kutomheshimu Baba yako na kutokumpa heshima Mkeo.
Ni Sawa na Mkeo asikupe nafasi ya Kwanza kama mumewe, lazima ujihisi kudharaulika.
Hujawahi sikia Watu wakilalamika Wake zao hawawasikilizi ila wanasikiliza Wazazi wao.
Ukiona Mkeo hakusikilizi na hakupi nafasi ya Kwanza, fukuza mapema, Huko mbeleni sio salama. Ukiona Mumeo anajifanya anawapenda Ndugu au wazazi wake kuliko wewe kimbia, Achana naye huyo Hana Akili na hajitambui. Mwambie akalale na hao Ndugu zake. Wala usimuonee aibu wala usimfiche, mpe makavu.
Ni hatari kuoa au kuolewa na MTU asiyejua kutenganisha mipaka na makundi ya Watu.
Robert Heriel
Taikon wa Fasihi
Kwa sasa Dar es salaam
SWALI ZURI,
NAMIMI NAKUULIZA SWALI
KATI YA MAMA NA MKE NANI ULIANZA KUISHI NAYE KWANZA KABLA HUJAZALIWA NA BAADA YA KUZALIWA KWAKO????
USIACHE MBACHAO KWA MSALA UPITAO.
NAFIKILI EMENIELEWA
Kuzaa na kulea ni proud na wajibu. Kulea wazazi pia ni proud na wajibu.Mama atakuambia alikuzaa, na anataka Kula matunda ya mwanaye
Waafrica ushamba siku unatuisha na Dunia itakuwa imefikia mwisho, siti ya mbele unaona ishu sana? Kiusalama siti ya mbele haifai mjinga wewe ndio maana hata Raia hawezi kaa siti ya mbele ana kaa katikatiKATI YA MAMA NA MKE NANI ANAPASWA KUKAA SITI YA MBELE WAKATI UNAENDESHA GARI?
Anaandika, Robert Heriel
Rafiki yangu Hosea amenipigia simu akaniuliza hivi; Kati ya Mama yake na MKE wake Nani anastahili kukaa SITI ya MBELE ya GARI wakati yeye(Hosea) anaendesha Gari? Nikaona niilete mada Hii kwenu. Ili tujifunze wote.
Imekuwa ni kawaida ya Watu kutaka kuwalinganisha MAMA na MKE kuwa Nani zaidi ya mwenzake.
Nataka kusema kuwa ni makosa makubwa kulinganisha vitu au Watu wasiolingana. Mke ni daraja jingine na Mama ni Daraja jingine.
Pili, Kati ya MKE na Mama hakuna aliyebora zaidi ya mwenzake isipokuwa ubora wao utapimwa Kwa namna watakavyo au walivyotekeleza majukumu yao Kwa nafasi zao. Mama kuzaa pekee yake haimfanyi kuwa Bora isipokuwa yapo majukumu mengine kama malezi. Halikadhalika MKE kukuzalia Watoto pekeake haitoshi kumfanya awe Bora kwako isipokuwa majukumu yake Kwa Watoto pamoja na wewe kama mumewe.
Kama utapima uzito wa majukumu ya MKE na Mama bila kujali madaraja Yao basi utagundua MKE ni zaidi ya Mama, na hapo nazungumzia kimajukumu na kiwajibu. Hata hivyo hiyo haimfanyi MKE kuwa Bora zaidi ya Mama.
Asubuhi nilitoka kuelezea mada isemayo Watu Maskini na wajinga hupenda kuongozwa na Mitazamo na Maoni ya Watu zaidi kuliko Kanuni na sheria. Kama tungefuata Kanuni na sheria Hilo swali lisingekuwepo na haya mambo ya kulinganisha MKE na Mama yasingekuwepo. Kwa sababu Kanuni na sheria zipo wazi kabisa.
Rafiki yangu Hosea aliponiuliza swali hilo nilimjibu Kwa kumuuliza maswali yafuatayo;
1. Nikamuuliza; Kitandani mwako unalala na Nani?
Mbona haukuniuliza Kati ya MKE na Mama yako Nani ambaye utalala naye kitanda kimoja?
Akaguna, akasema hayo mambo ni tofauti na mambo ya SITI za magari.
2. Nikamuuliza, Kati ya Mama na MKE wako Nani anaitwa Mrs. Hosea? Akajibu MKE wangu.
3. Nikamuuliza, Wakati Mama yako anakaa SITI ya MBELE na wewe, je Mkeo atakaa nyuma na Baba yako(mkwewe)? Yaani Wakati Mama yako anang'ang'ania kukaa SITI ya mbele, Baba yako anakuwa yupo wapi au mumewe anakuwa yupo wapi?
4. Nikamuuliza, Watoto wako watakubali Mama Yao(Mkeo) umuweke Nyuma ilhali wewe ndiye mume wake(Baba Yao)? Huoni utajenga kitu kwa Watoto kuwa humpendi Mama Yao na umemuweka katika nafasi ya pili?
Huoni hiyo itakuathiri Huko baadaye Watoto wakikua?
Hata hivyo mtu yeyote anaweza kukaa SITI ya MBELE iwe Mama au MKE au mtoto itategemea Kwa maana hayo ni mambo madpfp ila kama kuna mazingira ya kuonyesha Nani anastahili kukaa MBELE basi MKE ndiye anayestahili. Maana kuna Wamama wengine wanachokochoko Sana. Kumzaa MTU hakukupi Haki ya kuvunja itifaki ya nature na kumfanya MTu uliyemzaa kuwa mtumwa. Nafasi lazima ziheshimiwe.
Kisheria na kikanuni, kwenye familia mama na Baba anashika nafasi ya tatu Huko kama sio ya nne. Kwa mtiririko huu.
1. Mume na MKE.
Hawa ndio nafasi ya Kwanza. Yaani MKE lazima Ampe mumewe nafasi ya Kwanza halikadhalika na Mwanaume/mume lazima Ampe Mkewe nafasi ya Kwanza katika familia.
2. Watoto
Hawa ndio wanashika nafasi ya Pili. mume na MKE huhangaika Kwa Ajili ya Watoto wao kuwalea mpaka wakikua.
3. Wazazi
Baba na Mama. Hawa ndio hushika nafasi ya tatu katika mahusiano ya familia. Baba na Mama yako ni familia nyingine yenye uhusiano wa karibu wa kidamu na ninyi. Ila haina maana wao ndio wawe namba moja.
4. Ndugu
Hawa ni wale mliozaliwa pamoja iwe Baba mmoja, Mama mmoja, mtoto wa Mama mkubwa au mdogo, wajomba, mashangazi n.k.
5. Jamaa
Hawa ni wale wenye undugu wa mbali, undugu wa Tochi.
6. Marafiki.
Hawa ni wale ambao hamna undugu lakini mnaukaribu na mahusiano mazuri.
Zingatia Watoto utakaowazaa wewe kwako ni namba mbili lakini wakishakua na kuanzisha familia wao watakuweka namba tatu. Na wajukuu watakuwa nafasi ya nne Huko, hivyo unakosa mamlaka ya kuingilia familia zao labda wakuombe ushauri.
Jukumu kubwa la mzazi ni kuwalea Watoto wake katika miaka yote ya uhai wake. Lakini sio kudai nafasi zisizo zako. Jukumu la mtoto ni kuwaheshimu wazazi wake, kwa kusikiliza mashauri Mema.
Kama Mama yako anakupenda Sana basi atapaswa aonyeshe upendo huo Kwa Baba yako mzazi. Yaani abaki kwenye nafasi yake. Nafasi ya mume wake asikupe wewe. Wala wewe usimpoke Baba yako nafasi yake Kwa Mama yako. Kila mmoja abaki kwenye nafasi yake.
Baba yako ndio anapaswa kumfanya Mama yako namba moja na sio wewe. Kumfanya Mama yako namba moja ni kutomheshimu Baba yako na kutokumpa heshima Mkeo.
Ni Sawa na Mkeo asikupe nafasi ya Kwanza kama mumewe, lazima ujihisi kudharaulika.
Hujawahi sikia Watu wakilalamika Wake zao hawawasikilizi ila wanasikiliza Wazazi wao.
Ukiona Mkeo hakusikilizi na hakupi nafasi ya Kwanza, fukuza mapema, Huko mbeleni sio salama. Ukiona Mumeo anajifanya anawapenda Ndugu au wazazi wake kuliko wewe kimbia, Achana naye huyo Hana Akili na hajitambui. Mwambie akalale na hao Ndugu zake. Wala usimuonee aibu wala usimfiche, mpe makavu.
Ni hatari kuoa au kuolewa na MTU asiyejua kutenganisha mipaka na makundi ya Watu.
Robert Heriel
Taikon wa Fasihi
Kwa sasa Dar es salaam
Siti ya mbele haiafai, kwa usalama na hata baadhi ya magari huwa wameandika hio tahadhari sasa nyie mnaona ni ujiko sanaMke anakaa mbele
Akili za Waafrica hizi, walio ubda Magari kam.Wajapani huwezi wakuta wanashobokea sijui sit za mbele njoo sasa kwetu Waafrica nywele ngumu[emoji23][emoji23][emoji23]
Utaziweza Akili za Wanawake.
Wanawake wanapenda kupendwa.
Si unaona swali halijaulizwa Kwa upande wetu kina Baba.
Kwa Wanawake inamaana kubwa, Wanawake ni Watu wa kugombea nafasi za kupendwa[emoji3][emoji3]
Yaani nikisoma yaan nahic aka kakatuni kwenye avatar yako ndo kanaongea. Na sauti yake naisikia kabisaNone of them. I put all of them in the back. I put my kid in the front seat with me.
Never give priority to any woman. Women shouldnt also give priority to women. You will catch pure hell.
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23] khaaaahShemeji tu nae anakaa mbele mke nyuma hii nchi ngumu sana.
[emoji16][emoji16][emoji16][emoji16][emoji16][emoji1787]kafanya Nini Jamani mkeo?daahhhKwanza inategemeana na gari Kama Ni hz Hilux single cabin namtupa mke nyuma kbsa Kisha mam angu mbele
Sent from my Infinix X650 using JamiiForums mobile app
Umefurahi wa kunyumba[emoji16][emoji16][emoji16][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23] khaaaah
Simple tu hakuna complications akae mbele mama baasi...!!!jus simple mathsHii mada ukitaka kujibu vizuri, jaribu kuvaa uhusika wa pande zote. Yaani jifanye mzazi na jifanye mtoto.