Kati ya Mama na Mke Nani anapaswa kukaa Siti ya mbele wakati unaendesha Gari?

KATI YA MAMA NA MKE NANI ANAPASWA KUKAA SITI YA MBELE WAKATI UNAENDESHA GARI?

Anaandika, Robert Heriel

Rafiki yangu Hosea amenipigia simu akaniuliza hivi; Kati ya Mama yake na MKE wake Nani anastahili kukaa SITI ya MBELE ya GARI wakati yeye(Hosea) anaendesha Gari? Nikaona niilete mada Hii kwenu. Ili tujifunze wote.

Imekuwa ni kawaida ya Watu kutaka kuwalinganisha MAMA na MKE kuwa Nani zaidi ya mwenzake.
Nataka kusema kuwa ni makosa makubwa kulinganisha vitu au Watu wasiolingana. Mke ni daraja jingine na Mama ni Daraja jingine.

Pili, Kati ya MKE na Mama hakuna aliyebora zaidi ya mwenzake isipokuwa ubora wao utapimwa Kwa namna watakavyo au walivyotekeleza majukumu yao Kwa nafasi zao. Mama kuzaa pekee yake haimfanyi kuwa Bora isipokuwa yapo majukumu mengine kama malezi. Halikadhalika MKE kukuzalia Watoto pekeake haitoshi kumfanya awe Bora kwako isipokuwa majukumu yake Kwa Watoto pamoja na wewe kama mumewe.

Kama utapima uzito wa majukumu ya MKE na Mama bila kujali madaraja Yao basi utagundua MKE ni zaidi ya Mama, na hapo nazungumzia kimajukumu na kiwajibu. Hata hivyo hiyo haimfanyi MKE kuwa Bora zaidi ya Mama.

Asubuhi nilitoka kuelezea mada isemayo Watu Maskini na wajinga hupenda kuongozwa na Mitazamo na Maoni ya Watu zaidi kuliko Kanuni na sheria. Kama tungefuata Kanuni na sheria Hilo swali lisingekuwepo na haya mambo ya kulinganisha MKE na Mama yasingekuwepo. Kwa sababu Kanuni na sheria zipo wazi kabisa.

Rafiki yangu Hosea aliponiuliza swali hilo nilimjibu Kwa kumuuliza maswali yafuatayo;

1. Nikamuuliza; Kitandani mwako unalala na Nani?
Mbona haukuniuliza Kati ya MKE na Mama yako Nani ambaye utalala naye kitanda kimoja?
Akaguna, akasema hayo mambo ni tofauti na mambo ya SITI za magari.

2. Nikamuuliza, Kati ya Mama na MKE wako Nani anaitwa Mrs. Hosea? Akajibu MKE wangu.

3. Nikamuuliza, Wakati Mama yako anakaa SITI ya MBELE na wewe, je Mkeo atakaa nyuma na Baba yako(mkwewe)? Yaani Wakati Mama yako anang'ang'ania kukaa SITI ya mbele, Baba yako anakuwa yupo wapi au mumewe anakuwa yupo wapi?

4. Nikamuuliza, Watoto wako watakubali Mama Yao(Mkeo) umuweke Nyuma ilhali wewe ndiye mume wake(Baba Yao)? Huoni utajenga kitu kwa Watoto kuwa humpendi Mama Yao na umemuweka katika nafasi ya pili?
Huoni hiyo itakuathiri Huko baadaye Watoto wakikua?

Hata hivyo mtu yeyote anaweza kukaa SITI ya MBELE iwe Mama au MKE au mtoto itategemea Kwa maana hayo ni mambo madpfp ila kama kuna mazingira ya kuonyesha Nani anastahili kukaa MBELE basi MKE ndiye anayestahili. Maana kuna Wamama wengine wanachokochoko Sana. Kumzaa MTU hakukupi Haki ya kuvunja itifaki ya nature na kumfanya MTu uliyemzaa kuwa mtumwa. Nafasi lazima ziheshimiwe.

Kisheria na kikanuni, kwenye familia mama na Baba anashika nafasi ya tatu Huko kama sio ya nne. Kwa mtiririko huu.

1. Mume na MKE.
Hawa ndio nafasi ya Kwanza. Yaani MKE lazima Ampe mumewe nafasi ya Kwanza halikadhalika na Mwanaume/mume lazima Ampe Mkewe nafasi ya Kwanza katika familia.

2. Watoto
Hawa ndio wanashika nafasi ya Pili. mume na MKE huhangaika Kwa Ajili ya Watoto wao kuwalea mpaka wakikua.

3. Wazazi
Baba na Mama. Hawa ndio hushika nafasi ya tatu katika mahusiano ya familia. Baba na Mama yako ni familia nyingine yenye uhusiano wa karibu wa kidamu na ninyi. Ila haina maana wao ndio wawe namba moja.

4. Ndugu
Hawa ni wale mliozaliwa pamoja iwe Baba mmoja, Mama mmoja, mtoto wa Mama mkubwa au mdogo, wajomba, mashangazi n.k.

5. Jamaa
Hawa ni wale wenye undugu wa mbali, undugu wa Tochi.

6. Marafiki.
Hawa ni wale ambao hamna undugu lakini mnaukaribu na mahusiano mazuri.

Zingatia Watoto utakaowazaa wewe kwako ni namba mbili lakini wakishakua na kuanzisha familia wao watakuweka namba tatu. Na wajukuu watakuwa nafasi ya nne Huko, hivyo unakosa mamlaka ya kuingilia familia zao labda wakuombe ushauri.

Jukumu kubwa la mzazi ni kuwalea Watoto wake katika miaka yote ya uhai wake. Lakini sio kudai nafasi zisizo zako. Jukumu la mtoto ni kuwaheshimu wazazi wake, kwa kusikiliza mashauri Mema.

Kama Mama yako anakupenda Sana basi atapaswa aonyeshe upendo huo Kwa Baba yako mzazi. Yaani abaki kwenye nafasi yake. Nafasi ya mume wake asikupe wewe. Wala wewe usimpoke Baba yako nafasi yake Kwa Mama yako. Kila mmoja abaki kwenye nafasi yake.

Baba yako ndio anapaswa kumfanya Mama yako namba moja na sio wewe. Kumfanya Mama yako namba moja ni kutomheshimu Baba yako na kutokumpa heshima Mkeo.

Ni Sawa na Mkeo asikupe nafasi ya Kwanza kama mumewe, lazima ujihisi kudharaulika.
Hujawahi sikia Watu wakilalamika Wake zao hawawasikilizi ila wanasikiliza Wazazi wao.

Ukiona Mkeo hakusikilizi na hakupi nafasi ya Kwanza, fukuza mapema, Huko mbeleni sio salama. Ukiona Mumeo anajifanya anawapenda Ndugu au wazazi wake kuliko wewe kimbia, Achana naye huyo Hana Akili na hajitambui. Mwambie akalale na hao Ndugu zake. Wala usimuonee aibu wala usimfiche, mpe makavu.

Ni hatari kuoa au kuolewa na MTU asiyejua kutenganisha mipaka na makundi ya Watu.

Robert Heriel
Taikon wa Fasihi
Kwa sasa Dar es salaam
Sasa magari yenyewe hatuna.
 
Nakukumbusha Tuu Kaka
Waheshimu Baba na Mama Upate Miaka Mingi na Yenye Heri Duniani.
Kutomuweka Baba Siti ta Mbele wakati Yeye anahitaji,Wewe Kwa Mfano Ukakata asikae mbele tayari Hujamheshimu,Kwani Ungemkubalia Ungepungukiwa nini?
Ina Maana Akikulaani?
akifedheheka?
Hujamuheshimu na Hutaishi Miaka Mingi yenye Kheri!
Vijana wa Siku Hizi Mitandao aimewaharibu nyie[emoji30]
Zamani Watoto walikuwa wanawaheshimu sana Wazazi wao Bila Kuhojihoji kama wewe ulivyohoji!
Nakwambia Bila wazazi wako huyo Mke usingemjua[emoji12]
 
Mke anakaa mbele

Mwanzo 2:24

"Kwa hiyo mwanamume atamwacha baba yake na mama yake naye ataambatana na mkewe, nao watakuwa mwili mmoja."

Mama yangu naye aende akaambatane na mumewe(baba) na kama hayupo inapaswa aheshimu maana unapokuwa na mke mama inapaswa ajue ni muda wako na mke wako kuwa kitu kimoja,hivyo itabidi akae siti za nyuma.

Nakukumbusha Tuu Kaka
Waheshimu Baba na Mama Upate Miaka Mingi na Yenye Heri Duniani.
Kutomuweka Baba Siti ta Mbele wakati Yeye anahitaji,Wewe Kwa Mfano Ukakata asikae mbele tayari Hujamheshimu,Kwani Ungemkubalia Ungepungukiwa nini?
Ina Maana Akikulaani?
akifedheheka?
Hujamuheshimu na Hutaishi Miaka Mingi yenye Kheri!
Vijana wa Siku Hizi Mitandao aimewaharibu nyie[emoji30]
Zamani Watoto walikuwa wanawaheshimu sana Wazazi wao Bila Kuhojihoji kama wewe ulivyohoji!
Nakwambia Bila wazazi wako huyo Mke usingemjua[emoji12]
 
Hili ni swali pana sana na halina jibu la moja kwa moja. Inategemea mama yupo na baba au yupo peke yake, kama yupo peke yake kiheshima mnapaswa kumpa offer ya kukaa mbele coz kiafrica kiti cha mbele ni cha heshima yeye mwenyewe ndio akatae aseme atakaa nyuma.

Pia inategemea na mchango wa mama mwenyewe jamani kuna watu bila mama usingekuwa wewe na hata huyo mke asingekutazama mara mbili so kama mama yupo peke yake bila baba apewe nafasi ya kuchagua kama Baba yupo baba anakaa mbele mama na mke nyuma

Umenena Vema sana Kaka
“Kiti cha Mbele ni cha Heshima”
Waheshimu Baba na Mama Upate Miaka Mingi na Yenye Heri Duniani.
Kutomuweka Baba Siti ta Mbele wakati Yeye anahitaji,Wewe Kwa Mfano Ukakata asikae mbele tayari Hujamheshimu,Kwani Ungemkubalia Ungepungukiwa nini?
Ina Maana Akikulaani?
akifedheheka?
Hujamuheshimu na Hutaishi Miaka Mingi yenye Kheri!
Vijana wa Siku Hizi Mitandao aimewaharibu nyie[emoji30]
Zamani Watoto walikuwa wanawaheshimu sana Wazazi wao Bila Kuhojihoji kama wewe ulivyohoji!
Nakwambia Bila wazazi wako huyo Mke usingemjua[emoji12]
cc: Lusungo. Rober heriel
 
[emoji1488][emoji1488][emoji1488]

Umeongea vizuri kabisa
Hasa Kwa ndoa za kimila.
Ila hizi ndoa za Kikristo na ndoa za kisasa ambazo ukioa MKE sio kwamba ndio anaondoka kwao moja Kwa moja hapo lazima migigoro izuke.

Mama na Baba zake wakija nao watataka Favour hizohizo unazowapa Ndugu zako.

Sio ajabu Kuna kasumba ya Wanawake kuwachukia Ndugu wa mume ikibidi na mume mwenyewe na kumfitinisha Mumewe na watoto Kwa kile kiitwacho kutokakuwa na HAKI katika ndoa hasa Kwa mambo madogo kama hayo.

Kiafrika MKE sio lolote na wala sio chochote, ndio maana anashika nafasi ya tatu au ya nne ndani ya familia. Yaani Mume anathamini wazazi, kisha Ndugu, alafu Watoto mwisho ndio MKE.
Mtiririko huo umeathiri Maendeleo ya Afrika na ustawi wa Baba hasa anapozeeka.
Watoto humchukia na kumuona Baba katili na Hii yote ni kutokana na kuvunja mtiririko sahihi wa itifaki ya familia.

Wanaume Wakiafrika tunachoshindwa kuelewa kuwa Mke sio Ndugu lakini ni Mama wa Watoto tunaowazaa. Na hakuna asiyejua kuwa Future yetu ipo Kwa Watoto. Kama hutomthamini MKE na kumuweka nafasi yake basi ni wazi future ya Baba Huko mbeleni itakuwa hatarini, Watoto sio ajabu wakamuweka Baba katika nafasi za mwisho Huko.

Ubinafsi wa Waafrika ndio unawafanya waafrika Wasiendelee, na kurithishana utajiri wa Mali na utamaduni.

Nakukumbusha Tuu Kaka
Waheshimu Baba na Mama Upate Miaka Mingi na Yenye Heri Duniani.
Kutomuweka Baba Siti ta Mbele wakati Yeye anahitaji,Wewe Kwa Mfano Ukakata asikae mbele tayari Hujamheshimu,Kwani Ungemkubalia Ungepungukiwa nini?
Ina Maana Akikulaani?
akifedheheka?
Hujamuheshimu na Hutaishi Miaka Mingi yenye Kheri!
Vijana wa Siku Hizi Mitandao aimewaharibu nyie[emoji30]
Zamani Watoto walikuwa wanawaheshimu sana Wazazi wao Bila Kuhojihoji kama wewe ulivyohoji!
Nakwambia Bila wazazi wako huyo Mke usingemjua[emoji12]
 
Nakukumbusha Tuu Dada

Naunga mkono hoja, kuna aina mbili za familia.
1. Nucleus Family
Hapa familia ni baba, mama na watoto. Hizi ni familia za kizungu, wazazi, uncles na aunts sio sehemu ya familia na wakizeeka wanakuwa abandoned kwenye nursing home till death do them away!. Usually familia za hivi zina standard car ya 4 seater, baba na mama mbele, watoto wawili seat ya nyuma. Babu na bibi wakija for visit, they rent a 7 seater, baba na mama wanakaa mbele, watoto wanakaa seat ya pili, babu na bibi wanakaa seat ya nyuma.

2. Extended family
Baba, mama, bibi, babu na watoto.
Hizi ni typical African family, mtu muhimu kuliko hata wewe ni baba na mama, mke, watoto.
Wazazi wakija seat ya mbele unakaa na baba au Mama, mke na Mama au baba seat ya pili na watoto wanakaa kule mwisho.

Akija kaka yangu au ndugu yangu, mke anakaa nyuma na watoto.

Kiafrika undugu ni wa damu tuu, hivyo ndugu ni baba Mama waliokuzaa, wale mliozaliwa nao na watoto wenu, mke sio ndugu na ndugu wa mke ni jamaa tuu!.

Mke ni mtu tuu wa kuja na kupita, anaweza kuachwa ukaoa mwingine au wakaolewa hata wake 10!. Familia za hivi wazazi ndio muhimu zaidi, mama akija home, mke lazima ajishushe kumpisha mama in control.

Wazazi wakizeeka wanakuwa taken care na watoto kwa upendo mpaka siku yao ikifika.

P

Nakukumbusha Tuu Kaka
Waheshimu Baba na Mama Upate Miaka Mingi na Yenye Heri Duniani.Vitabu vya Dini pia vinasemw hili.
Kutomuweka Baba Siti ta Mbele wakati Yeye anahitaji,Wewe Kwa Mfano Ukakata asikae mbele tayari Hujamheshimu,Kwani Ungemkubalia Ungepungukiwa nini?
Ina Maana Akikulaani?
akifedheheka?
Hujamuheshimu na Hutaishi Miaka Mingi yenye Kheri!
Vijana wa Siku Hizi Mitandao aimewaharibu nyie[emoji30]
Zamani Watoto walikuwa wanawaheshimu sana Wazazi wao Bila Kuhojihoji kama wewe ulivyohoji!
Nakwambia Bila wazazi wako huyo Mke usingemjua[emoji12]
 
nje kidogo ya mada : Mimi hata niki request uber huwa nakaa siti ya nyuma.Sio kwasababu za usalama [emoji777] bali naona ndio siti sahihi ( sijui nna chembechembe za uboss)
ile siti ya mbele sijui naionagaje yani siipendi afu naonaga kama ya msela wa dereva..

nikipata nafasi ya kuwa mama mkwe, nakaa siti ya nyuma kiroho safi
 
Umenena Vema sana Kaka
“Kiti cha Mbele ni cha Heshima”
Waheshimu Baba na Mama Upate Miaka Mingi na Yenye Heri Duniani.
Kutomuweka Baba Siti ta Mbele wakati Yeye anahitaji,Wewe Kwa Mfano Ukakata asikae mbele tayari Hujamheshimu,Kwani Ungemkubalia Ungepungukiwa nini?
Ina Maana Akikulaani?
akifedheheka?
Hujamuheshimu na Hutaishi Miaka Mingi yenye Kheri!
Vijana wa Siku Hizi Mitandao aimewaharibu nyie[emoji30]
Zamani Watoto walikuwa wanawaheshimu sana Wazazi wao Bila Kuhojihoji kama wewe ulivyohoji!
Nakwambia Bila wazazi wako huyo Mke usingemjua[emoji12]
cc: Lusungo. Rober heriel
Baba kukaa mbele ni sawa kiheshima na kimaadili kwa pamoja.hata kubadolishana mawazo ni rahisi na kutazama kujadili mbali mbali kipindi cha safari.Mtoa mada amelenga kuonesha hadhi na mpambano ambao inaweza, kujitokeza kulingana na tabia za mama na wanawake kiujumla.ila kihaki na kama kuna mpambano au ushinndani wa chini chini akae mke.kama vita ikiendelea basi na gari liuzwe.kwa hiyo kama mama ndo anaishi kabisa nyumbani hapo ndo kila siku atakaa yeye?
 
Siti ya mbele upande wa abiria siyo ya kugombaniwa ukiweza kuikwepa ikwepe itachukua muda sana kueleweka kwanini nashauri hivyo ndo maana hata viongozi wa kiserekali hawakaagi pale
 
Halafu hii tabia ya kupimisha status ya mama na mke huwa mnaitoaga wapi???
MAMA ni mama jamani!! hata amri kumi za Mungu unaambiwa - Waheshimu baba na mama upate miaka mingi na heri duniani! yani mke hata awaje hawezi kuwa na nafasi kama mama kivyovyote vile yani...
Mke/Mume ni mchizi wako, mpenzi wako & mtu ambae mmeamua kupendana kimapenzi mkaanzisha familia yenu, hawa watu unaweza replace anytime!!!
unaachana na mke unaoa mwingine unazaa wengine maisha yanaendelea hii hata huko kwenye jamii zenu ipo! ila Mama anabaki kuwa Mama

filisika uwe fukara au umwa haswaa, miezi hata sita huna mia mkeo ataangalia ushawahi mfanyia nini maishani mwake kikubwa ndo kitakubeba miezi sita ijayo zaidi ya hapo hutoboi nae nakwambia!!
Mama ako yeye hana cha kuzingatia utakua kwenye mbawa zake maisha yake yote! uumwe usiumwe uwe na mbuni au huna hajali kwake yeye utabaki ni mwanae ambae atakupenda kwa moyo wake wote sikuzote!!!
Acheni huu ufananisho either wa kimajukumu au umuhimu!
 
KATI YA MAMA NA MKE NANI ANAPASWA KUKAA SITI YA MBELE WAKATI UNAENDESHA GARI?

Anaandika, Robert Heriel

Rafiki yangu Hosea amenipigia simu akaniuliza hivi; Kati ya Mama yake na MKE wake Nani anastahili kukaa SITI ya MBELE ya GARI wakati yeye(Hosea) anaendesha Gari? Nikaona niilete mada Hii kwenu. Ili tujifunze wote.

Imekuwa ni kawaida ya Watu kutaka kuwalinganisha MAMA na MKE kuwa Nani zaidi ya mwenzake.
Nataka kusema kuwa ni makosa makubwa kulinganisha vitu au Watu wasiolingana. Mke ni daraja jingine na Mama ni Daraja jingine.

Pili, Kati ya MKE na Mama hakuna aliyebora zaidi ya mwenzake isipokuwa ubora wao utapimwa Kwa namna watakavyo au walivyotekeleza majukumu yao Kwa nafasi zao. Mama kuzaa pekee yake haimfanyi kuwa Bora isipokuwa yapo majukumu mengine kama malezi. Halikadhalika MKE kukuzalia Watoto pekeake haitoshi kumfanya awe Bora kwako isipokuwa majukumu yake Kwa Watoto pamoja na wewe kama mumewe.

Kama utapima uzito wa majukumu ya MKE na Mama bila kujali madaraja Yao basi utagundua MKE ni zaidi ya Mama, na hapo nazungumzia kimajukumu na kiwajibu. Hata hivyo hiyo haimfanyi MKE kuwa Bora zaidi ya Mama.

Asubuhi nilitoka kuelezea mada isemayo Watu Maskini na wajinga hupenda kuongozwa na Mitazamo na Maoni ya Watu zaidi kuliko Kanuni na sheria. Kama tungefuata Kanuni na sheria Hilo swali lisingekuwepo na haya mambo ya kulinganisha MKE na Mama yasingekuwepo. Kwa sababu Kanuni na sheria zipo wazi kabisa.

Rafiki yangu Hosea aliponiuliza swali hilo nilimjibu Kwa kumuuliza maswali yafuatayo;

1. Nikamuuliza; Kitandani mwako unalala na Nani?
Mbona haukuniuliza Kati ya MKE na Mama yako Nani ambaye utalala naye kitanda kimoja?
Akaguna, akasema hayo mambo ni tofauti na mambo ya SITI za magari.

2. Nikamuuliza, Kati ya Mama na MKE wako Nani anaitwa Mrs. Hosea? Akajibu MKE wangu.

3. Nikamuuliza, Wakati Mama yako anakaa SITI ya MBELE na wewe, je Mkeo atakaa nyuma na Baba yako(mkwewe)? Yaani Wakati Mama yako anang'ang'ania kukaa SITI ya mbele, Baba yako anakuwa yupo wapi au mumewe anakuwa yupo wapi?

4. Nikamuuliza, Watoto wako watakubali Mama Yao(Mkeo) umuweke Nyuma ilhali wewe ndiye mume wake(Baba Yao)? Huoni utajenga kitu kwa Watoto kuwa humpendi Mama Yao na umemuweka katika nafasi ya pili?
Huoni hiyo itakuathiri Huko baadaye Watoto wakikua?

Hata hivyo mtu yeyote anaweza kukaa SITI ya MBELE iwe Mama au MKE au mtoto itategemea Kwa maana hayo ni mambo madpfp ila kama kuna mazingira ya kuonyesha Nani anastahili kukaa MBELE basi MKE ndiye anayestahili. Maana kuna Wamama wengine wanachokochoko Sana. Kumzaa MTU hakukupi Haki ya kuvunja itifaki ya nature na kumfanya MTu uliyemzaa kuwa mtumwa. Nafasi lazima ziheshimiwe.

Kisheria na kikanuni, kwenye familia mama na Baba anashika nafasi ya tatu Huko kama sio ya nne. Kwa mtiririko huu.

1. Mume na MKE.
Hawa ndio nafasi ya Kwanza. Yaani MKE lazima Ampe mumewe nafasi ya Kwanza halikadhalika na Mwanaume/mume lazima Ampe Mkewe nafasi ya Kwanza katika familia.

2. Watoto
Hawa ndio wanashika nafasi ya Pili. mume na MKE huhangaika Kwa Ajili ya Watoto wao kuwalea mpaka wakikua.

3. Wazazi
Baba na Mama. Hawa ndio hushika nafasi ya tatu katika mahusiano ya familia. Baba na Mama yako ni familia nyingine yenye uhusiano wa karibu wa kidamu na ninyi. Ila haina maana wao ndio wawe namba moja.

4. Ndugu
Hawa ni wale mliozaliwa pamoja iwe Baba mmoja, Mama mmoja, mtoto wa Mama mkubwa au mdogo, wajomba, mashangazi n.k.

5. Jamaa
Hawa ni wale wenye undugu wa mbali, undugu wa Tochi.

6. Marafiki.
Hawa ni wale ambao hamna undugu lakini mnaukaribu na mahusiano mazuri.

Zingatia Watoto utakaowazaa wewe kwako ni namba mbili lakini wakishakua na kuanzisha familia wao watakuweka namba tatu. Na wajukuu watakuwa nafasi ya nne Huko, hivyo unakosa mamlaka ya kuingilia familia zao labda wakuombe ushauri.

Jukumu kubwa la mzazi ni kuwalea Watoto wake katika miaka yote ya uhai wake. Lakini sio kudai nafasi zisizo zako. Jukumu la mtoto ni kuwaheshimu wazazi wake, kwa kusikiliza mashauri Mema.

Kama Mama yako anakupenda Sana basi atapaswa aonyeshe upendo huo Kwa Baba yako mzazi. Yaani abaki kwenye nafasi yake. Nafasi ya mume wake asikupe wewe. Wala wewe usimpoke Baba yako nafasi yake Kwa Mama yako. Kila mmoja abaki kwenye nafasi yake.

Baba yako ndio anapaswa kumfanya Mama yako namba moja na sio wewe. Kumfanya Mama yako namba moja ni kutomheshimu Baba yako na kutokumpa heshima Mkeo.

Ni Sawa na Mkeo asikupe nafasi ya Kwanza kama mumewe, lazima ujihisi kudharaulika.
Hujawahi sikia Watu wakilalamika Wake zao hawawasikilizi ila wanasikiliza Wazazi wao.

Ukiona Mkeo hakusikilizi na hakupi nafasi ya Kwanza, fukuza mapema, Huko mbeleni sio salama. Ukiona Mumeo anajifanya anawapenda Ndugu au wazazi wake kuliko wewe kimbia, Achana naye huyo Hana Akili na hajitambui. Mwambie akalale na hao Ndugu zake. Wala usimuonee aibu wala usimfiche, mpe makavu.

Ni hatari kuoa au kuolewa na MTU asiyejua kutenganisha mipaka na makundi ya Watu.

Robert Heriel
Taikon wa Fasihi
Kwa sasa Dar es salaam
Dear Mama - 2 Pack
 
Back
Top Bottom