Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
We unadhan unapoambiwa uchague mke sahihi maana yake nn... Shida tunaongozwa na hisia ndo maana hayo yote yanatukumba, tunadharau vitu vidogo vidogo na vya msingi. Jamaa alichoeleza ni mtazamo ambao wengi hawatoelewa sababu ya hisia ila ule ndo uhalisia.Mama huwa ni moja tu huku Duniani.
Mama ndiye anayeweza kukupenda bila masharti yoyote.
Nasema anaweza sababu sio mama wote wanawapenda watoto wao , wengine ni ilimradi na Kama akiwa mchawi akiamua anakuua tu ni swala la muda!
Mke hutegemea kukupenda hutegemea na mwandamo wa mwezi.
Ni wachache sana atakupenda bila masharti.
Matharani :
Kosa kuwa na kazi uwe huna hata shilingi 100 uone kama huyo mkeo ataendelea kukupenda na kukustahamilia kwa miaka mingi.
Lakini mama yako hata ukiwa dhoofulhali lofa wa kutupa atakupenda tu na kukuombea. (Ingawa sio mama wote wanapenda watoto wao wengine ni ilimradi tu kajikuta amekuzaa basi ).
Wacha upuuzi wewe kwani kukaa nyuma ni kutomheshimu? Kwanza ukiona mama anadai kukaa mbele ilhali mkwewe akiwepo basi huyo mama busara hana. Mm bimkubwa wangu hata nikiwa naye yeye na watoto. Atataka mtoto akae mbele au akae nao huko nyuma. Yani hajajiweka mtu wa mbele mbele kiivo.Hili ni swali pana sana na halina jibu la moja kwa moja. Inategemea mama yupo na baba au yupo peke yake, kama yupo peke yake kiheshima mnapaswa kumpa offer ya kukaa mbele coz kiafrica kiti cha mbele ni cha heshima yeye mwenyewe ndio akatae aseme atakaa nyuma.
Pia inategemea na mchango wa mama mwenyewe jamani kuna watu bila mama usingekuwa wewe na hata huyo mke asingekutazama mara mbili so kama mama yupo peke yake bila baba apewe nafasi ya kuchagua kama Baba yupo baba anakaa mbele mama na mke nyuma
Basi senior aachiwe gari aendeshe [emoji28][emoji28]Among the two, wife and mother; who's senior to the other?
Huna mke na huna gari vipate kwanza ndo useme hivyoMama yangu atakaa mbele na mke atakaa nyuma.....labda mama akatae kukaa mbele......
Sawa Mungu mgawa ridhiki....ukitaka nitapata tu
Au abaki home amwagilizie kuku pumba.Mwanzo 2:24
"Kwa hiyo mwanamume atamwacha baba yake na mama yake naye ataambatana na mkewe, nao watakuwa mwili mmoja."
Mama yangu naye aende akaambatane na mumewe(baba) na kama hayupo inapaswa aheshimu maana unapokuwa na mke mama inapaswa ajue ni muda wako na mke wako kuwa kitu kimoja,hivyo itabidi akae siti za nyuma.
Among the two, the driver and the driven; who's senior to the other?Basi senior aachiwe gari aendeshe [emoji28][emoji28]
Tusio na magari tunacomment wapi?KATI YA MAMA NA MKE NANI ANAPASWA KUKAA SITI YA MBELE WAKATI UNAENDESHA GARI?
Anaandika, Robert Heriel
Rafiki yangu Hosea amenipigia simu akaniuliza hivi; Kati ya Mama yake na MKE wake Nani anastahili kukaa SITI ya MBELE ya GARI wakati yeye(Hosea) anaendesha Gari? Nikaona niilete mada Hii kwenu. Ili tujifunze wote.
Imekuwa ni kawaida ya Watu kutaka kuwalinganisha MAMA na MKE kuwa Nani zaidi ya mwenzake.
Nataka kusema kuwa ni makosa makubwa kulinganisha vitu au Watu wasiolingana. Mke ni daraja jingine na Mama ni Daraja jingine.
Pili, Kati ya MKE na Mama hakuna aliyebora zaidi ya mwenzake isipokuwa ubora wao utapimwa Kwa namna watakavyo au walivyotekeleza majukumu yao Kwa nafasi zao. Mama kuzaa pekee yake haimfanyi kuwa Bora isipokuwa yapo majukumu mengine kama malezi. Halikadhalika MKE kukuzalia Watoto pekeake haitoshi kumfanya awe Bora kwako isipokuwa majukumu yake Kwa Watoto pamoja na wewe kama mumewe.
Kama utapima uzito wa majukumu ya MKE na Mama bila kujali madaraja Yao basi utagundua MKE ni zaidi ya Mama, na hapo nazungumzia kimajukumu na kiwajibu. Hata hivyo hiyo haimfanyi MKE kuwa Bora zaidi ya Mama.
Asubuhi nilitoka kuelezea mada isemayo Watu Maskini na wajinga hupenda kuongozwa na Mitazamo na Maoni ya Watu zaidi kuliko Kanuni na sheria. Kama tungefuata Kanuni na sheria Hilo swali lisingekuwepo na haya mambo ya kulinganisha MKE na Mama yasingekuwepo. Kwa sababu Kanuni na sheria zipo wazi kabisa.
Rafiki yangu Hosea aliponiuliza swali hilo nilimjibu Kwa kumuuliza maswali yafuatayo;
1. Nikamuuliza; Kitandani mwako unalala na Nani?
Mbona haukuniuliza Kati ya MKE na Mama yako Nani ambaye utalala naye kitanda kimoja?
Akaguna, akasema hayo mambo ni tofauti na mambo ya SITI za magari.
2. Nikamuuliza, Kati ya Mama na MKE wako Nani anaitwa Mrs. Hosea? Akajibu MKE wangu.
3. Nikamuuliza, Wakati Mama yako anakaa SITI ya MBELE na wewe, je Mkeo atakaa nyuma na Baba yako(mkwewe)? Yaani Wakati Mama yako anang'ang'ania kukaa SITI ya mbele, Baba yako anakuwa yupo wapi au mumewe anakuwa yupo wapi?
4. Nikamuuliza, Watoto wako watakubali Mama Yao(Mkeo) umuweke Nyuma ilhali wewe ndiye mume wake(Baba Yao)? Huoni utajenga kitu kwa Watoto kuwa humpendi Mama Yao na umemuweka katika nafasi ya pili?
Huoni hiyo itakuathiri Huko baadaye Watoto wakikua?
Hata hivyo mtu yeyote anaweza kukaa SITI ya MBELE iwe Mama au MKE au mtoto itategemea Kwa maana hayo ni mambo madpfp ila kama kuna mazingira ya kuonyesha Nani anastahili kukaa MBELE basi MKE ndiye anayestahili. Maana kuna Wamama wengine wanachokochoko Sana. Kumzaa MTU hakukupi Haki ya kuvunja itifaki ya nature na kumfanya MTu uliyemzaa kuwa mtumwa. Nafasi lazima ziheshimiwe.
Kisheria na kikanuni, kwenye familia mama na Baba anashika nafasi ya tatu Huko kama sio ya nne. Kwa mtiririko huu.
1. Mume na MKE.
Hawa ndio nafasi ya Kwanza. Yaani MKE lazima Ampe mumewe nafasi ya Kwanza halikadhalika na Mwanaume/mume lazima Ampe Mkewe nafasi ya Kwanza katika familia.
2. Watoto
Hawa ndio wanashika nafasi ya Pili. mume na MKE huhangaika Kwa Ajili ya Watoto wao kuwalea mpaka wakikua.
3. Wazazi
Baba na Mama. Hawa ndio hushika nafasi ya tatu katika mahusiano ya familia. Baba na Mama yako ni familia nyingine yenye uhusiano wa karibu wa kidamu na ninyi. Ila haina maana wao ndio wawe namba moja.
4. Ndugu
Hawa ni wale mliozaliwa pamoja iwe Baba mmoja, Mama mmoja, mtoto wa Mama mkubwa au mdogo, wajomba, mashangazi n.k.
5. Jamaa
Hawa ni wale wenye undugu wa mbali, undugu wa Tochi.
6. Marafiki.
Hawa ni wale ambao hamna undugu lakini mnaukaribu na mahusiano mazuri.
Zingatia Watoto utakaowazaa wewe kwako ni namba mbili lakini wakishakua na kuanzisha familia wao watakuweka namba tatu. Na wajukuu watakuwa nafasi ya nne Huko, hivyo unakosa mamlaka ya kuingilia familia zao labda wakuombe ushauri.
Jukumu kubwa la mzazi ni kuwalea Watoto wake katika miaka yote ya uhai wake. Lakini sio kudai nafasi zisizo zako. Jukumu la mtoto ni kuwaheshimu wazazi wake, kwa kusikiliza mashauri Mema.
Kama Mama yako anakupenda Sana basi atapaswa aonyeshe upendo huo Kwa Baba yako mzazi. Yaani abaki kwenye nafasi yake. Nafasi ya mume wake asikupe wewe. Wala wewe usimpoke Baba yako nafasi yake Kwa Mama yako. Kila mmoja abaki kwenye nafasi yake.
Baba yako ndio anapaswa kumfanya Mama yako namba moja na sio wewe. Kumfanya Mama yako namba moja ni kutomheshimu Baba yako na kutokumpa heshima Mkeo.
Ni Sawa na Mkeo asikupe nafasi ya Kwanza kama mumewe, lazima ujihisi kudharaulika.
Hujawahi sikia Watu wakilalamika Wake zao hawawasikilizi ila wanasikiliza Wazazi wao.
Ukiona Mkeo hakusikilizi na hakupi nafasi ya Kwanza, fukuza mapema, Huko mbeleni sio salama. Ukiona Mumeo anajifanya anawapenda Ndugu au wazazi wake kuliko wewe kimbia, Achana naye huyo Hana Akili na hajitambui. Mwambie akalale na hao Ndugu zake. Wala usimuonee aibu wala usimfiche, mpe makavu.
Ni hatari kuoa au kuolewa na MTU asiyejua kutenganisha mipaka na makundi ya Watu.
Robert Heriel
Taikon wa Fasihi
Kwa sasa Dar es salaam
Mama mkwe wako anafanana mama mkwe wa mama yangu, (bibi) tabia za kisirani, mfano kuna siku alimwambia mkamwana ampishe ana maongezi na mwanae yani kwenye chumba chake mkamwana, hebu fikiria mamkwe kama huyo,, hata kwenye gari anapenda seat ya mbele balaa ni wale mama wakwe wenye gubu la mwendokasi, ndo hivyo maza alishampuuzaKabisaaa yaani Mimi akae mbele aendeshe whatever yeye itampa faraja afanye,Mimi mama mkwe alikua anaingia chumbaniii kabisa kwetu asubuhi na Wala sijawahi kuchukia niliona tu Hana mwiko na hawana maadili ya kwetu baasii...
Yaani wanatoka na mwanawe miye Wala sijali,Wanakaa wanaongea miye nalala habari sipati...mpk leo ananipendaga yule mama
Sent from my Infinix X657 using JamiiForums mobile app
Dyadya.. umemaliza..big upNgoja nikuulize kitu,hivi Kuna tofauti kati ya mama mzazi na mama mkwe?
Km amezaa Mume Kwa Nini nisimheshimu?kuchokozaje Kwa mfano? as a wife mama angu mzazi akinichokoza narespond vipi?km namjibu au nagombana nae baaasi I will do the same to mama mkwe but if not I won't dare to quarrel with her,siwezi shindana na Pepo ya Mume wangu maana mwanaume Pepo yake Iko chini ya nyayo za mama yake na Mimi peoi yangu Iko chini ya Mume wangu.
Shida Moja tu wengi wengu hatunaga adabu kwa watu wasotuzaa na Kwa kesi ya mkwe tunamchukulia km outsiders while not yule ni mama wa Mume wangu hvyo ni mzazi wangu pia...
Sent from my Infinix X657 using JamiiForums mobile app
Kumbe ishu za kugombea siti zipo, ila watu wanajifanya kucrash km hazipo... Lakini all in all nimemuelewa mtoa mada kwamba hizi ishu sio tatizo... Tatizo ni uhalisia wa itifaki za kifamilia... Kiukweli nimemuelewa...Me naona inategemea na misingi tu mlio wekeana mimi nilinunua gari mke wangu akiwa na mtoto mdogo mwanzo alipenda sana kukaa mbele na mtoto wetu ila nilikuja kumshauri na akaelewa mpka leo siti ya mbele kwake labda tukiwa tunaenda sehemu ambapo tutabeba watu wengine na mama yangu pia sio mpenzi wa siti ya mbele hivyo hujikuta wamekaa nyuma wote wamejificha na tinted kaliiiiii na wanapiga stor zao. Maisha ni jinsi utakavyo yapeleka kukaa mbele kukaa nyuma haijalishi kinachojaliwa ni upendo na moyo wa kuwaweka karibu wale uwapendao.
Alikuja kunishangaza shangazi yangu kunilalamikia kwamba sijamjali eti kisa sikumfanya akae mbele na sikuvumilia nilimtolea uvivu kwa point kadhaa na toka siku hiyo hatamani hata kupanda gari langu maana hukuwepo nikitafuta iweje ulete mazingzong wakati wa kutumia tena nafanya hisani tu
Sent using Jamii Forums mobile app