Kati ya Mama na Mke Nani anapaswa kukaa Siti ya mbele wakati unaendesha Gari?

Kati ya Mama na Mke Nani anapaswa kukaa Siti ya mbele wakati unaendesha Gari?

Wote Wakae Hapo Mbele Iwapo Busara Imeshindwa Kutumika Kwenye Jambo Dogo
 
Huwa tuna wadharau wake zetu wakati wao ndo hutuzalia watoto. Wanawake huambukiza upumbavu kwa watoto hivyo hutathaminiwa.

Tutafute hela

Wazazi watafute hela
 
Zamani mama mkwe alikuwa anajileta mbele mi kimya silalamiki..
Now kapata akili anakaaa zake nyuma hata ukimwambia akae mbele hataki.
 
KATI YA MAMA NA MKE NANI ANAPASWA KUKAA SITI YA MBELE WAKATI UNAENDESHA GARI?

Anaandika, Robert Heriel

Rafiki yangu Hosea amenipigia simu akaniuliza hivi; Kati ya Mama yake na MKE wake Nani anastahili kukaa SITI ya MBELE ya GARI wakati yeye(Hosea) anaendesha Gari? Nikaona niilete mada Hii kwenu. Ili tujifunze wote.

Imekuwa ni kawaida ya Watu kutaka kuwalinganisha MAMA na MKE kuwa Nani zaidi ya mwenzake.
Nataka kusema kuwa ni makosa makubwa kulinganisha vitu au Watu wasiolingana. Mke ni daraja jingine na Mama ni Daraja jingine.

Pili, Kati ya MKE na Mama hakuna aliyebora zaidi ya mwenzake isipokuwa ubora wao utapimwa Kwa namna watakavyo au walivyotekeleza majukumu yao Kwa nafasi zao. Mama kuzaa pekee yake haimfanyi kuwa Bora isipokuwa yapo majukumu mengine kama malezi. Halikadhalika MKE kukuzalia Watoto pekeake haitoshi kumfanya awe Bora kwako isipokuwa majukumu yake Kwa Watoto pamoja na wewe kama mumewe.

Kama utapima uzito wa majukumu ya MKE na Mama bila kujali madaraja Yao basi utagundua MKE ni zaidi ya Mama, na hapo nazungumzia kimajukumu na kiwajibu. Hata hivyo hiyo haimfanyi MKE kuwa Bora zaidi ya Mama.

Asubuhi nilitoka kuelezea mada isemayo Watu Maskini na wajinga hupenda kuongozwa na Mitazamo na Maoni ya Watu zaidi kuliko Kanuni na sheria. Kama tungefuata Kanuni na sheria Hilo swali lisingekuwepo na haya mambo ya kulinganisha MKE na Mama yasingekuwepo. Kwa sababu Kanuni na sheria zipo wazi kabisa.

Rafiki yangu Hosea aliponiuliza swali hilo nilimjibu Kwa kumuuliza maswali yafuatayo;

1. Nikamuuliza; Kitandani mwako unalala na Nani?
Mbona haukuniuliza Kati ya MKE na Mama yako Nani ambaye utalala naye kitanda kimoja?
Akaguna, akasema hayo mambo ni tofauti na mambo ya SITI za magari.

2. Nikamuuliza, Kati ya Mama na MKE wako Nani anaitwa Mrs. Hosea? Akajibu MKE wangu.

3. Nikamuuliza, Wakati Mama yako anakaa SITI ya MBELE na wewe, je Mkeo atakaa nyuma na Baba yako(mkwewe)? Yaani Wakati Mama yako anang'ang'ania kukaa SITI ya mbele, Baba yako anakuwa yupo wapi au mumewe anakuwa yupo wapi?

4. Nikamuuliza, Watoto wako watakubali Mama Yao(Mkeo) umuweke Nyuma ilhali wewe ndiye mume wake(Baba Yao)? Huoni utajenga kitu kwa Watoto kuwa humpendi Mama Yao na umemuweka katika nafasi ya pili?
Huoni hiyo itakuathiri Huko baadaye Watoto wakikua?

Hata hivyo mtu yeyote anaweza kukaa SITI ya MBELE iwe Mama au MKE au mtoto itategemea Kwa maana hayo ni mambo madpfp ila kama kuna mazingira ya kuonyesha Nani anastahili kukaa MBELE basi MKE ndiye anayestahili. Maana kuna Wamama wengine wanachokochoko Sana. Kumzaa MTU hakukupi Haki ya kuvunja itifaki ya nature na kumfanya MTu uliyemzaa kuwa mtumwa. Nafasi lazima ziheshimiwe.

Kisheria na kikanuni, kwenye familia mama na Baba anashika nafasi ya tatu Huko kama sio ya nne. Kwa mtiririko huu.

1. Mume na MKE.
Hawa ndio nafasi ya Kwanza. Yaani MKE lazima Ampe mumewe nafasi ya Kwanza halikadhalika na Mwanaume/mume lazima Ampe Mkewe nafasi ya Kwanza katika familia.

2. Watoto
Hawa ndio wanashika nafasi ya Pili. mume na MKE huhangaika Kwa Ajili ya Watoto wao kuwalea mpaka wakikua.

3. Wazazi
Baba na Mama. Hawa ndio hushika nafasi ya tatu katika mahusiano ya familia. Baba na Mama yako ni familia nyingine yenye uhusiano wa karibu wa kidamu na ninyi. Ila haina maana wao ndio wawe namba moja.

4. Ndugu
Hawa ni wale mliozaliwa pamoja iwe Baba mmoja, Mama mmoja, mtoto wa Mama mkubwa au mdogo, wajomba, mashangazi n.k.

5. Jamaa
Hawa ni wale wenye undugu wa mbali, undugu wa Tochi.

6. Marafiki.
Hawa ni wale ambao hamna undugu lakini mnaukaribu na mahusiano mazuri.

Zingatia Watoto utakaowazaa wewe kwako ni namba mbili lakini wakishakua na kuanzisha familia wao watakuweka namba tatu. Na wajukuu watakuwa nafasi ya nne Huko, hivyo unakosa mamlaka ya kuingilia familia zao labda wakuombe ushauri.

Jukumu kubwa la mzazi ni kuwalea Watoto wake katika miaka yote ya uhai wake. Lakini sio kudai nafasi zisizo zako. Jukumu la mtoto ni kuwaheshimu wazazi wake, kwa kusikiliza mashauri Mema.

Kama Mama yako anakupenda Sana basi atapaswa aonyeshe upendo huo Kwa Baba yako mzazi. Yaani abaki kwenye nafasi yake. Nafasi ya mume wake asikupe wewe. Wala wewe usimpoke Baba yako nafasi yake Kwa Mama yako. Kila mmoja abaki kwenye nafasi yake.

Baba yako ndio anapaswa kumfanya Mama yako namba moja na sio wewe. Kumfanya Mama yako namba moja ni kutomheshimu Baba yako na kutokumpa heshima Mkeo.

Ni Sawa na Mkeo asikupe nafasi ya Kwanza kama mumewe, lazima ujihisi kudharaulika.
Hujawahi sikia Watu wakilalamika Wake zao hawawasikilizi ila wanasikiliza Wazazi wao.

Ukiona Mkeo hakusikilizi na hakupi nafasi ya Kwanza, fukuza mapema, Huko mbeleni sio salama. Ukiona Mumeo anajifanya anawapenda Ndugu au wazazi wake kuliko wewe kimbia, Achana naye huyo Hana Akili na hajitambui. Mwambie akalale na hao Ndugu zake. Wala usimuonee aibu wala usimfiche, mpe makavu.

Ni hatari kuoa au kuolewa na MTU asiyejua kutenganisha mipaka na makundi ya Watu.

Robert Heriel
Taikon wa Fasihi
Kwa sasa Dar es salaam
Mke wako
 
Mama anakaa mbele maana sipo naye siku zote ila mke niko nae mda Mwingi. Simple
 
Hili ni swali pana sana na halina jibu la moja kwa moja. Inategemea mama yupo na baba au yupo peke yake, kama yupo peke yake kiheshima mnapaswa kumpa offer ya kukaa mbele coz kiafrica kiti cha mbele ni cha heshima yeye mwenyewe ndio akatae aseme atakaa nyuma.

Pia inategemea na mchango wa mama mwenyewe jamani kuna watu bila mama usingekuwa wewe na hata huyo mke asingekutazama mara mbili so kama mama yupo peke yake bila baba apewe nafasi ya kuchagua kama Baba yupo baba anakaa mbele mama na mke nyuma
ina jibu hata kama hana mme akae nyuma na wajukuu zake,binafsi siwezagi kushindana na mtu ata akitaka aendeshe yeye gari namuacha,
wamama wetu wa vijijini hawana hizo habari za ujuaji
 
Maisha ya kimaskini ndo tunawaza hayo mara siti sijui Nini bla bla kibao lakin ukweli wapemba au waarabu wanaishi na wazazi wao Mwanzo mwisho Mama au Mtu yoyote anakaa popote anapojisikia ndo maana ngozi nyeusi tupo nyuma Sana kwa ajili ya ujinga ujinga kama uo
 
Miaka 5 nyuma ilitokea scenario kama hiyo nikajiongeza kukaa nyuma mama mkwe akaniondoa akaniambai siti yako huko mbele na mume wako yeye akakaa nyuma. Fast foward mwaka huu nikiwa na binti tayari mama mkwe alimfungulia binti mlango akae mbele na baba yake mimi na yeye tukakaa siti ya nyuma. ( ingawa sipo na mwanae tena). So mke anatakiwa akae mbele na ubavu wake.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ngoja nikuulize kitu,hivi Kuna tofauti kati ya mama mzazi na mama mkwe?
Km amezaa Mume Kwa Nini nisimheshimu?kuchokozaje Kwa mfano? as a wife mama angu mzazi akinichokoza narespond vipi?km namjibu au nagombana nae baaasi I will do the same to mama mkwe but if not I won't dare to quarrel with her,siwezi shindana na Pepo ya Mume wangu maana mwanaume Pepo yake Iko chini ya nyayo za mama yake na Mimi peoi yangu Iko chini ya Mume wangu.

Shida Moja tu wengi wengu hatunaga adabu kwa watu wasotuzaa na Kwa kesi ya mkwe tunamchukulia km outsiders while not yule ni mama wa Mume wangu hvyo ni mzazi wangu pia...

Sent from my Infinix X657 using JamiiForums mobile app
Umenena vyema sana
Kongole na Mumeo huko
Alipo kapata Mke.

Huyo jamaa anakwambia familia
Ni baba, Mama na Watoto
Bibi na Babu haiwahusu
Mpaka hapo nikamchukulia hamnazo

Hakuna mnachoshindania
Wanawake aina yako
Ndio tunaowatafutaga

Tambua nafasi yako
Mama hawezi kumreplace Mke
Na Mke hawezi kuwa Mama

Mwache afurahi akuachie baraka ya wewe na Ndoa yako.
Na kizazi chako
Wengine hurithishwa mpaka Mali
Hupewa vya Uvunguni na vya ukoo

Kama ambavyo wake humfurahisha baba mkwe
Basi wafanye pia kwa mama Wakwe.

Hii Dunia tu, nasi ni wapitaji[emoji120][emoji120][emoji120][emoji120][emoji120][emoji120][emoji120][emoji120][emoji120][emoji120][emoji120][emoji120][emoji120][emoji120][emoji120][emoji120]
 
Huna akili, kwa hiyo mama yako ndo utakuwa unamtomba?

Watu wengine hamna akili

Mama yako ni mke wa mtu
Ulizaliwa mara moja tu.
Kwani utatomba mara moja tu
Utamtomba huyo huyo tu
Daraja la Mama si la Mke
 
Mama huwa ni moja tu huku Duniani.

Mama ndiye anayeweza kukupenda bila masharti yoyote.

Nasema anaweza sababu sio mama wote wanawapenda watoto wao , wengine ni ilimradi na Kama akiwa mchawi akiamua anakuua tu ni swala la muda!

Mke hutegemea kukupenda hutegemea na mwandamo wa mwezi.

Ni wachache sana atakupenda bila masharti.

Matharani :

Kosa kuwa na kazi uwe huna hata shilingi 100 uone kama huyo mkeo ataendelea kukupenda na kukustahamilia kwa miaka mingi.

Lakini mama yako hata ukiwa dhoofulhali lofa wa kutupa atakupenda tu na kukuombea. (Ingawa sio mama wote wanapenda watoto wao wengine ni ilimradi tu kajikuta amekuzaa basi ).
 
Ulizaliwa mara moja tu.
Kwani utatomba mara moja tu
Utamtomba huyo huyo tu
Daraja la Mama si la Mke
Hawajui thamani ya mama haswa wangejua wasingesema Lau kama viongozi wa dini wangempa mama nafasi yake,asingetokea mwanadamu kucheza na nafasi ya mama yake!
Mama ana daraja la juu kabisa kwa Mungu...!!na mwanamke akikupenda atampenda mzazi wako na kumheshimu tu

Sent from my Infinix X657 using JamiiForums mobile app
 
Back
Top Bottom