Kati ya Mama na Mke Nani anapaswa kukaa Siti ya mbele wakati unaendesha Gari?

Hakuna jibu la moja kwa moja, mfano mke mwenye heshima huacha kwanza mama mkwe wake apande gari na humfungulia mlango wa mbele...

Wakati huo huo mama mkwe mwenye heshima, humpisha mkwewe akae mbele...
Anapaswaa kukaa mke. Hakuna pingamizi.
 
Wakikujibu nitag.
 
Umefurahi wa kunyumba[emoji16][emoji16][emoji16]
Watu hawajui hata wanacho kiandikaaaa. [emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]

Kuna mtu aliwahi kumjibu mumewe "km mama ako ni kila kitu na unyumba akupe yeye mbna uke anao kwann ulinitafuta mie kunioa, c unge muoa yeye"

Na imeandikwa "utaacha baba na mama, utaambatana na mkewe/mumewe'

Bado watu hawaelewi tyuuh, seat ya mbelee ni ya mke.
 
Nani anatakiwa kukaa wapi ni jambo la heshima na uhusiano. Kiti cha mbele ni cha mke wako maana wakatri mwingine mkno unateleza na kushika paja, sasa utaruhusu vipi mama mzazi/mkwe akae mbele mwishowe ukosee umshike paja kwa bahati mbayo. Kiofisi mheshimiwa hukaa kiti cha kati au nyuma kwenye gari. Mheshimiwa hakai mbele. Mama ni mheshimiwa na heshima yake inakamilika kwa kumuweka kiti cha nyuma/katikati na wala siyo kutomheshimu. Hata kwenye safari mazungumzo mengi yatakuwa na mkeo, kwa hiyo akikaa mbele inakuwa rahisi kuongea. Kama mnasafiri na gari anaendesha dereva, basi mnaweza kumuweka mama mbele, wewe na mkero mkakaa nyuma au katikati. Ila sisi Waswahili tuna kasumba ya kupenda kukaa mbele kwa kudhani kile ndiyo kiti cha heshima. Hiyo siyo kweli.
 
huyu mama atakuwa na lake yaani akiwa kwa mmewe akae kiti cha mbele gari la mmewe akija kwa mwanae tena akae kiti cha mbele kwenye gari ya mtoto wake haya bana
 
Je, utafanyaje?

Uko na familia yako, wewe mkeo/mumeo mnatoka out dereva ni Mume/mke, bahati nzuri ni kwamba mzazi {mama} wako yupo hapo kwaajili ya kuja kuwasalimia.

Mnataka kutoka kwenda outing mkiwa na gari yenu, Je nani anastahili kukaa siti ya mbele sambamba na wewe mkeo, Mumeo au Mama yako mzazi!?
 
Swali ni kwamba nani kwako atakaa siti ya mbele sambamba na wewe, tupe kipaumbele chako!?
Kuna kiongozi umewahi kumuona anakaa seat ya mbele kwenye gari?

Je wedding? Kuna maharusi wanakaa seat ya mbele? Ukiweza kujijibu maswali haya utaelewa wazi tunadiscuss hoja za kitoto tu hapa.
 
Kuna kiongozi umewahi kumuona anakaa seat ya mbele kwenye gari?

Je wedding? Kuna maharusi wanakaa seat ya mbele? Ukiweza kujijibu maswali haya utaelewa wazi tunadiscuss hoja za kitoto tu hapa.
Tunazungumzia issue za kifamilia, sio issue za kiutawala au sherehe
Issue za kifamilia as africans zina mambo mengi. Lets discuss the reality of our family life
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…