Kati ya Mama na Mke nani anastahili zaidi ya 50% ya mapenzi

Kati ya Mama na Mke nani anastahili zaidi ya 50% ya mapenzi

Kwanza kabisa tuelewe majukumu ya hawa watu katika sekta zao. Heshima ya Mama haipungui kijana unapooa.

Tunajua umuhimu wa Mama toka amekubeba miezi 9 umezaliwa umekuwa na umejitambua hilo ni jukumu lake na lazima apate heahima kama Mungu alivyoagiza.

Umejitambua unataka sasa kujitegemea,umeanzisha Familia yani umeoa tunajua umuhimu wa Mke. Mke anaendeleza majukumu ya Mama alipoishia tena yakiongezeka mengine mengi zaidi. Kumbuka Mke ni ubavu wako,tukifuata kile Mungu alituambia hatuwezi kulelewa na Mama mpaka kufa kwetu.

Kulingana na migogoro ya kifamilia ya kileo ni nani anastahili upendo zaidi baada ya kujana kuoa?

Ukimpenda sana Mke wako Mama anaona umemtenga baada ya kuoa na huenda akahisi Mke ndio anafanya usimthamini kama mwanzo. Ukimpenda sana Mama Mke anaona ameporwa madaraka na Mama na anaona Mama anataka kumharibia ndoa.

Leo la mada hii ni kila muhusika kujua mipaka yake na kuepuka migogoro isiyo ya lazima.

Binafsi ukishaoa lazima mapenzi yapungue kwa Mama sababu ya majukumu ambayo Mama hawezi kukutimizia tena kwa hiyo

Mama 40% Mke 60%

Karibuni wajumbe
Mama [emoji817] %
 
nafasi ya mama haina mbadala, haizibiki, wala haina sub.
Mama 70% wife 30%.
Ye mwenyewe kamkuta na nimeishi nae miaka mingi kuliko yeye wife, yani hadi niishi na wife muda nilioishi na mama atakua keshatangulia msbele za haki.
Wife anaweza kukusaliti, kukuchukia, kukuua, hata kukufanyia ubaya wowote lakini mama kama ni yeye alikuweka tumboni miezi tisa yeye ndio final kwenye maisha yako. TAMBUA HILO

Jikite kwenye mada, umechanganya HESHIMA na MAPENZI.
 
Dawa ni simple!
Kuwa snitch kwa wote tu.

1.Sometime muoneshe mama ndio wa maana sana.

2.Muoneshe mke ndio wa maana sana. Program your wife for that.
 
Kwanza kabisa tuelewe majukumu ya hawa watu katika sekta zao. Heshima ya Mama haipungui kijana unapooa.

Tunajua umuhimu wa Mama toka amekubeba miezi 9 umezaliwa umekuwa na umejitambua hilo ni jukumu lake na lazima apate heahima kama Mungu alivyoagiza.

Umejitambua unataka sasa kujitegemea,umeanzisha Familia yani umeoa tunajua umuhimu wa Mke. Mke anaendeleza majukumu ya Mama alipoishia tena yakiongezeka mengine mengi zaidi. Kumbuka Mke ni ubavu wako,tukifuata kile Mungu alituambia hatuwezi kulelewa na Mama mpaka kufa kwetu.

Kulingana na migogoro ya kifamilia ya kileo ni nani anastahili upendo zaidi baada ya kujana kuoa?

Ukimpenda sana Mke wako Mama anaona umemtenga baada ya kuoa na huenda akahisi Mke ndio anafanya usimthamini kama mwanzo. Ukimpenda sana Mama Mke anaona ameporwa madaraka na Mama na anaona Mama anataka kumharibia ndoa.

Leo la mada hii ni kila muhusika kujua mipaka yake na kuepuka migogoro isiyo ya lazima.

Binafsi ukishaoa lazima mapenzi yapungue kwa Mama sababu ya majukumu ambayo Mama hawezi kukutimizia tena kwa hiyo

Mama 40% Mke 60%

Karibuni wajumbe
Marehem Jerry Nashon 'Dudumizi', anakupa jibu kwenye wimbo wake uitwao 'IBRAHIM', nadhani ni kutoka bendi ya Bimalee au Washirika Tanzania Stars(watu Njata Njata)! Kwa walio na umri angalau miaka 35 na kuendelea watakua wanujua huu wimbo.
Power Nguzo au Eddie Nasoro nafikiri kauweka youtube au nenda browser
 
Mama atabaki kuwa mama milele, upendo wangu kwake haufutiki, ila NIMEMCHAGUA mke wa kuishi naye, kumpenda na kutengeneza familia yetu...itoshe kusema mke na watoto wangu kwanza, kisha anafuatia mama na wengineo.

Kama alivyochaguliwa tukishindwana anasonga mbele, nachagua mwingine
 
Kuna mapenz na upendo
Jukumu la mama ni kukuzaa,kukulea na kukupa malezi bora ili uwe baba bora baadae
Upendo wa mama kwa mtoto mara nying haupungui ila upendo wa mwanaune kwa mkewe unaweza kupungua ila mapenz yakaendelea kuwepo..
Huwez mpenda mama yako kuliko mke wako
Utajidanganya nafsi tu bure na utakua unajilisha upepo..
Mume bora anatengenezwa na mama na baba,na hvyo hvyo mke bora anatengenezwa na familia yake
Mke wako ni namba moja wako,
Msaidizi wako
Mshauri wako
Msiri wako
Mzaz mwenzako
Mla vingi vyako
Mtesi wako
Mfurahia vyako
Mfurahiwa wako

Unataka kujua unampenda nani?
Mwanaume mwngine akitembea na mama yako itakuuma kdgo
Mwanaume mwingine akimtongoza tu mke wako naimani jibu unalo moyoni mwako.

ThtsY,mke ndio anashikilia uhusiano wote wa maisha halisi ya mwanaume...na sio mama.
Asante sana komenti tamu sana
Unajaribu kugawa upendo kama pesa/chungwa! Akili nyingine huwa sizielewi. Kwa nini usiwapende wote 100%?
Umepewa 100% tu uzigawe na sio 200% utagawa vp?
 
Punguza hasira mkuu...lengo la uzi huu sio kuleta mgawanyiko na ndio mana nimesema kabisa,lengo ni kila mtu kujuiona ana nafasi gani kwa mtu na sio kushindana au kushindanisha hayo makundi
Binadamu ana makundi mhm kadhaa na kimsingi hayo makundi hayatakiwi ku-compete maana itakuwa ni unfair competition

1.wazazi
2.ndugu
3.mke au wake
4.Marafiki na watu unaoshirikiana nao
Kwenye Mambo ya msingi

Sasa ni mpuuzi pekee ndo atawaza Kuweka competition Kati ya

1.Mama aliyemzaa na mke
2.Dada ake tumbo moja na mke
3.Rafiki na mama
4.Mama ake na ndugu

Yaani kifupi hayo makundi Kila kundi hapo linaumuhimu wake kivyake na kwa mda wake..

Huwezi ukaanza kushindanisha parachichi na maharage hata kama unapenda maharage sana inabidi ujue good fats utazipata kwenye parachichi.

Mpuuzi atadhani mama ni muhimu kuliko mke au mke ni muhimu kuliko marafiki au marafiki ni muhimu kuliko ndugu.ila mwerevu anajua baraka nitakazozipata kwa mama siwezi kupata kwa mke na care nitakayopata kwa mke siwezi kupata kwa mama,msaada nitakaopewa na rafiki siwezi kupata kwa mke na changamoto hizi mtu peke wa kuzibeba ni ndugu pekee.

Mjinga akioa anaachana na marafiki wote hata kupokea simu ya ndugu hataki, ana dharau mama ake lakini akipoteza tu kazi ndo anaelewa nina rafiki yangu Sehmu flani,nina ndugu yangu Sehmu flan na kumbe baraka za mama ni mhm...

Mjinga mwingine akioa anadhan Bado yupo single basi anaishi km hana mke, anajali ndugu na kumdharau mkewe,mama kwanza mke ni mtu wa kupita tu hlf akishikwa na stroke hawezi kufanya kazi, marafiki wamekata,ndugu wamechoka kuhudumia ndo anageuka pembeni nakujikuta yupo yeye na mke tu na mke yupo busy kumfulia nguo zake zenye mikojo.

Usiwe mjinga
 
Kwanini umechagua mke ambaye hupendi? Au ulichaguliwa na mama?
watoto 50%
mama 25%
mke 25%

yani mama na mke wapambane wenyewe ataemtoa mwenzake kwa knockout haya.
 
Mapenzi ni 2 ways traffic. Hivyo mapenzi ya mama/baba/watoto/ndugu/marafiki huwezi linganisha na ya mkeo. Na ukijaribu kushindanisha mapenzi kati ya mama na mkeo utafeli tuu, sababu ni kwamba unapompenda mkeo kuna vitu unavitegemea ambsvyo huwezi pata kwa mtu mwingine ila mkeo unless uwe mtu wa michepuko
 
Mke siyo ndugu yako mkuu.. ukiumwa tu aamue kubaki au kusonga lakin mama ako atakupgania hadi mwisho
Ohoo umempa dhamana ya sehemu nyeti za maisha yako...anakuandalia chakula,unalala nae,watoto then unamkana sio ndungu yako...
 
Huyo mke utakuwa umemwokota ila hujafunga nae ndoa na kuamua kuungana...mke sahihi hawez kukuacha.
Mamako anaweza kukuogesha?
Kwann mama yako asikuogeshe?
Hahaha naona kama unakurupukia mapenzi bado hujawajua vizuri binaadam wewe.
 
Mbona kila mtu ana nafasi yake tofauti kabisa na ya mwenzake na unaweza kuwajali wote bila vikwazo labda tu ukute kuna mwenye chokochoko binafsi
 
Ndio hizo mm nasemea
 
Duh!! Haya bana kumbe unaweza kuogeahwa na mamako? Nyie ndio wale mnawataguna mama zenu baada ya kuachana na mke
 
Duh!! Haya bana kumbe unaweza kuogeahwa na mamako? Nyie ndio wale mnawataguna mama zenu baada ya kuachana na mke
Umeongea jambo baya sana, unapaswa unitake radhi, kama wewe huna heshima na mama yako basi usidhani kama kila mtu hamuheshimu wa kwake,

Wewe umesema huko juu kua kama ukiumwa mama yako ataweza kukuogesha?
Na mimi nimekujibu kwanini ashindwe?
Umeumwa upo hoi na hakuna njia nyingine yaan mama yako ashindwe kukuogesha akuache udhalilike?
 
Acha maswali ya kitoto hayo. Unampa mamako mapenzi, wewe huwa unalala na mamako? Unataka ukalale na mamako siku 5 (50%) na siku 5 (50%) ukalale na mkeo, siyo? Swali la kijinga kabisa. Mpende mama yako kwa moyo wako wote (100%) na pia mpende mke wako kwa moyo wako wote (100%). Simple.
Asante sana komenti tamu sana

Umepewa 100% tu uzigawe na sio 200% utagawa vp?
 
Back
Top Bottom