Kati ya Mama na Mke nani anastahili zaidi ya 50% ya mapenzi

Kati ya Mama na Mke nani anastahili zaidi ya 50% ya mapenzi

Umeongea jambo baya sana, unapaswa unitake radhi, kama wewe huna heshima na mama yako basi usidhani kama kila mtu hamuheshimu wa kwake,

Wewe umesema huko juu kua kama ukiumwa mama yako ataweza kukuogesha?
Na mimi nimekujibu kwanini ashindwe?
Umeumwa upo hoi na hakuna njia nyingine yaan mama yako ashindwe kukuogesha akuache udhalilike?
Hakuna njia nyingine basi utakuwa na tatizo na ndugu jamaa na marafiki. Labda ukute dunia nzima tumebak mimi na mama tu. Kama ilivyokuwa kwa Loti na wanaye
 
biblia ipo clear...lazima uache wazazi uambatane na Mwenzio
 
Unapokuwa na mke haina maana unaanza kumchukia mama yako. Kila mmoja ana nafasi yake, na kwa mama muelewa hatakusumbua kutaka umpe nafasi ya kumjali zaidi yeye bali mkeo.
 
Mtoa mada, mke na mama ni watu wawili wenye nafasi tofauti. Hawalinganishwi kwa asilimia wala muda. Ni sawa na kuuliza INI na FIGO kipi muhimu kweny mwili.... hakuna jibu.

Mwanaume uko katikati yao na haswa ukiwa umeoa tambua nafasi ya mke wako na umpe anachostahili kma mke, na kwa mama hvyo hvyo utambue nafasi yake. Usimfanye mkeo ajiskie kma mama yako ni mke mwingine na usimfanye mama yako ahisi kapoteza baraka ya mwanae.

Ukishaanza tu kuwa na fikra za kujiuliza umpe yupi favor zaidi shida ipo kwako, hujitambui vyema.
 
Mke akifa unaoa mwingine ila mama akiondoka hakuna tena mama, sasa pima upendo kati ya mke na mama

Sent from my TECNO-N2 using JamiiForums mobile app

Mkuu ushawahi kuwaza kuwa once upon a time, mama yako alikuwa kwenye nafasi ya mke na aliwaza kama yeye ni wa muhimu kuliko bibi yako? Hivi baba yako angemfikiria mama yako kama ulivyoandika hapo juu je? Mama hana mbadala na vile vile mke hana mbadala. Hujafiwa na mama wala mke tulia ndugu yangu hakuna maumivu yenye afadhali.
 
Unapokuwa na mke haina maana unaanza kumchukia mama yako. Kila mmoja ana nafasi yake, na kwa mama muelewa hatakusumbua kutaka umpe nafasi ya kumjali zaidi yeye bali mkeo.
Yan kati ya wachache walionielewa ww ni mmoja wapo👏👏
 
  • Thanks
Reactions: Auz
Mtoa mada, mke na mama ni watu wawili wenye nafasi tofauti. Hawalinganishwi kwa asilimia wala muda. Ni sawa na kuuliza INI na FIGO kipi muhimu kweny mwili.... hakuna jibu.

Mwanaume uko katikati yao na haswa ukiwa umeoa tambua nafasi ya mke wako na umpe anachostahili kma mke, na kwa mama hvyo hvyo utambue nafasi yake. Usimfanye mkeo ajiskie kma mama yako ni mke mwingine na usimfanye mama yako ahisi kapoteza baraka ya mwanae.

Ukishaanza tu kuwa na fikra za kujiuliza umpe yupi favor zaidi shida ipo kwako, hujitambui vyema.
Hujanielewa au hujasoma makala umesoma kichwa tu
 
Back
Top Bottom