Bwana weeeh mbona unahamisha sana topic na hoja yangu, binafsi nashindwa nikujibu nini maana kila ukijibu uleta jibu na hoja ambayo sijaizungumzia na sijui unazitoa wapi, na hicho ndo kinafanya nione kama uko hapa kubishana ili uonekane unajua sana, HAUTAKIWI KUWA HIVYO.
hakuna sehemu nimesema tofali imara sio kitu kikubwa cha kuzingatiwa kwenye ujenzi wa ghorofa, nakubali ni kikubwa ila sio "cha kwanza" kama ulivyojaribu kisema huko juu (rejea comment zako).
Sasa hiyo hoja ya uliyoanza nayo kwa kusema ("..Unaweza kuanza na vyote then tofali zikawa hovyo litakuwa ghorofa hilo..?") UMEITOA WAPI.? Nionyeshe ni wapi nimesema unaweza kujenga ghorofa kwa kuanza na vingine halafu tofali ziwe hovyo...
HOJA YANGU NI KWAMBA, mimi kama Civil Engineer mzoefu najua umuhimu wa tofali imara ila SIWEZI kusema kwamba tofali imara ndio kitu cha kwanza nitawaza kama nitakuwa na tender ya ujenzi wa ghorofa.
Wewe kama unaona CHA KWANZA ni tofali, basi utakuwa ni Engineer wa kipekee sana kwenye hii game ya Construction.