Kati ya Mungu na binadamu, je ni nani ampe mwenzake pesa?

Kati ya Mungu na binadamu, je ni nani ampe mwenzake pesa?

Kati ya Mungu na binadamu ni yupi ampe mwenzake pesa?

Lama ni Mungu ndio anatakiwa ampe binadamu pesa! Kwanini mnatuambia tumtolee Mungu pesa?
Amejitosheleza wala haitaji cjchote kutoka kwetu na akisema hvo umtolee ni ktk kukujaribu kama utafanya analotakaa. Na kwa imani yangu kumtolea huko ni ktk watu nao kufurahia mfno kwa kuwapa masikini, fukara yatima nk
 
Dash!plan Paris umewaza mbali sna,Mungu hutupatia Pesa na siyo sisi kumpatia 'mfumo wa dini'yye mwenyewe anasema fedha na dhahabu ni malizake.ndo maana tunamuomba atufanikishie ktk mahitaji tumuombayo.na tunapo fanikiwa tuwapatie wenye uhitaji ili watambue MUNGU yupo na hiyo ndo sadaka ya kweli.
 
Mleta mada Mungu hana shida na pesa kwa kuwa kila kitu kimeumbwa naye hata mumeo ameumbwa naye.
Soma Zaburi 24:1
 
Basi kila mtu apambane kuwa mnyenyekevu then apewe hizo mali, na wale walionazo watumie tu bila kuwapa wengine.
 
Zile pesa apewe Mungu zinatumika kufanya Kazi ya Mungu mfano kueneza neno la Mungu, kuwalisha watenda Kazi, kusaidia yatima,wajane nk.
 
Amejitosheleza wala haitaji cjchote kutoka kwetu na akisema hvo umtolee ni ktk kukujaribu kama utafanya analotakaa. Na kwa imani yangu kumtolea huko ni ktk watu nao kufurahia mfno kwa kuwapa masikini, fukara yatima nk
Na kwa nini amjaribu kiumbe wake anayemjua kuwa ni dhaifu? Na kwa nini hao masikini, fukara na yatima asiwasaidie yeye moja kwa moja bila ushiriki wa mwanadamu?
 
Dash!plan Paris umewaza mbali sna,Mungu hutupatia Pesa na siyo sisi kumpatia 'mfumo wa dini'yye mwenyewe anasema fedha na dhahabu ni malizake.ndo maana tunamuomba atufanikishie ktk mahitaji tumuombayo.na tunapo fanikiwa tuwapatie wenye uhitaji ili watambue MUNGU yupo na hiyo ndo sadaka ya kweli.
Kama ni mali zake kuna haja gani ya sisi kumtolea? Anashindwa kuziweka kwake moja kwa moja ili binadamu waendelee na maisha bila kuhangaika na sadaka?
 
Zile pesa apewe Mungu zinatumika kufanya Kazi ya Mungu mfano kueneza neno la Mungu,kuwalisha watenda Kazi,kusaidia yatima,wajane nk.
Hapo ndipo mnapopigwa. Yeye anasindwaje kuwalisha hao watenda kazi wake mpaka watuombe sadaka kupitia jina lake na vitisho vingi?
 
Ya Kaisari muchie Kaisari..., wewe Pesa unampa anayepokea hayo mengine ni justifications tu za wapokeaji...
 
Hapo ndipo mnapopigwa. Yeye anasindwaje kuwalisha hao watenda kazi wake mpaka watuombe sadaka kupitia jina lake na vitisho vingi?
Wapo bize kueneza injili nani atawalisha.
Hivi mfano Padri akatafute vibarua Ili ale au ashinde njaa atafanyaje Kazi ya Mungu.Wao awatakiwi kufanya Kazi nje ya kueneza neno la Mungu muda wao wote yafaa wautumie kuponya roho za watu.
 
Na kwa nini amjaribu kiumbe wake anayemjua kuwa ni dhaifu? Na kwa nini hao masikini, fukara na yatima asiwasaidie yeye moja kwa moja bila ushiriki wa mwanadamu?
Anawajaribu ajue ni yupi ktk hao wanadamu ni mwenye kufanya yale aliyoamrisha na kuacha aliyokataza na hapa ndipo watakapo patikana wa peponi na wa motoni baada ya kutizamwa matendo yetu mmoja mmoja yapi yatazidi mengine kati ya mema na mabaya.
Kwa nn mwalimu anakupa mtihani ikiwa amefundisha na ana hakika mlimuelewa vema?
 
Back
Top Bottom