Kati ya Pesa, Mawasiliano na Wivu, kipi hasa kinasababisha ndoa kuvunjika?

Kipi hasa kinasababisha ndoa kuvunjika?

  • A. Pesa

    Votes: 2 28.6%
  • B. Mawasiliano

    Votes: 0 0.0%
  • C. Wivu

    Votes: 1 14.3%
  • D. Vyote hapo juu

    Votes: 4 57.1%

  • Total voters
    7

PAYE

JF-Expert Member
Joined
Jun 19, 2025
Posts
459
Reaction score
644
Wakuu

Katika mihangaiko yangu, nimejikuta nimepita kwenye kijiwe nongwa kimoja. Kimekolea! Watu wamekaa wamezunguka, kila mmoja ameshikilia upande wake, na mjadala uliokuwa unaendelea ulikuwa kuhusu migogoro ya ndoa.

Mmoja anasema, “Ndoa nyingi zinavunjwa na pesa. Bila pesa, mapenzi yanageuka kuwa mateso.” Mwingine akapinga, “Sio pesa, tatizo ni mawasiliano. Watu wanaishi nyumba moja lakini hawaongei tena.” Wa tatu akacheka na kusema, “Nyie mnajidanganya, tatizo kubwa ni Wivu. Kila mtu anataka awe sahihi, hakuna anayetaka kushuka chini.”

Mjadala ukazidi kuwa mkali, kila mmoja akitoa mifano na kusimamia hoja yake.

Sasa naomba pia kujua kati ya Pesa, Mawasiliano na Wivu, kipi hasa kinasababisha ndoa kuvunjika?
 
Uwaminifu.....

Watu wana pesa na wanachapiwa,ndoa zinakufa.

Hata uwe na pesa za kukopesha serikali,kama mweza wako siyo mwaminifu utachapiwa tu
 
Wakuu

Katika mihangaiko yangu, nimejikuta nimepita kwenye kijiwe nongwa kimoja. Kimekolea! Watu wamekaa wamezunguka, kila mmoja ameshikilia upande wake, na mjadala uliokuwa unaendelea ulikuwa kuhusu migogoro ya ndoa.

Mmoja anasema, “Ndoa nyingi zinavunjwa na pesa. Bila pesa, mapenzi yanageuka kuwa mateso.” Mwingine akapinga, “Sio pesa, tatizo ni mawasiliano. Watu wanaishi nyumba moja lakini hawaongei tena.” Wa tatu akacheka na kusema, “Nyie mnajidanganya, tatizo kubwa ni Wivu. Kila mtu anataka awe sahihi, hakuna anayetaka kushuka chini.”

Mjadala ukazidi kuwa mkali, kila mmoja akitoa mifano na kusimamia hoja yake.

Sasa naomba pia kujua kati ya Pesa, Mawasiliano na Wivu, kipi hasa kinasababisha ndoa kuvunjika?
ndoa ikikolea tu vizuri matokeo yake ni kusambaratika 🐒
 
Ni ujinga tu, wa kutaka maisha ghali na wakati utaishia mavumbini
 
wanawake hawaelewiki wanataka nini kilichobaki ni kuishi nao kwa akili tu. Onyo usije ukajisahau ukawekeza akili huko ukidhani utaweza mridhisha litaja kukuta jambo simamia misingi yako ka mwanaume inatosha.
 
Wakuu

Katika mihangaiko yangu, nimejikuta nimepita kwenye kijiwe nongwa kimoja. Kimekolea! Watu wamekaa wamezunguka, kila mmoja ameshikilia upande wake, na mjadala uliokuwa unaendelea ulikuwa kuhusu migogoro ya ndoa.

Mmoja anasema, “Ndoa nyingi zinavunjwa na pesa. Bila pesa, mapenzi yanageuka kuwa mateso.” Mwingine akapinga, “Sio pesa, tatizo ni mawasiliano. Watu wanaishi nyumba moja lakini hawaongei tena.” Wa tatu akacheka na kusema, “Nyie mnajidanganya, tatizo kubwa ni Wivu. Kila mtu anataka awe sahihi, hakuna anayetaka kushuka chini.”

Mjadala ukazidi kuwa mkali, kila mmoja akitoa mifano na kusimamia hoja yake.

Sasa naomba pia kujua kati ya Pesa, Mawasiliano na Wivu, kipi hasa kinasababisha ndoa kuvunjika?
UBINAFSI. Kujiona bora kuliko mwenzako!
 
Back
Top Bottom