Hayati Magu alipunguza wajumbe wa NEC wa CCM, Samia kaongeza idadi, nani aliyeona kwa jicho la makengeza kati ya hawa Wenyeviti wawili?
Vijana wa sasa hivi hawajui CCM imetoka wapi, iko wapi na inaelekea wapi.
Kwa wasiyoijua CCM wanahoji na kupima uwezo wa uongozi wa Marais katika Awamu mbalimbali. Lakini ukweli hawaujui au kama wanaujua wanaifunika kwa sababu zao binafsi.
CCM imepita katika nyakati mbalimbali na muhimu kulingana na kundi linaloongoza chama, kama ifuatavyo:
1)
Kabla ya Uhuru: Viongozi wa TAA (1929) ikiongozwa na Ali Saidi, ikabadilishwa kuwa TANU (1954) na Nyerere, walishughulikia Uhuru na kufanikiwa. Hawa viongozi, chini ya Mwl Nyerere, Kawawa nk walisukumwa na uzalendo.
2)
Baada ya Uhuru: Viongozi walioanzisha TANU, walijenga jumuiya za chama ikiwemo ya Vijana (TANU Youth League) kwa madhumuni ya kuandaa viongozi wa kesho. Hawa vijana walipelekwa Jeshini kupata mafunzo ya uongozi na ushupavu. Baadhi yao ni Marehemu Moses Nnauye, Yusuf Makamba, Kinana, na wengine walifuatia km Jakaya kikwete.
Kundi hili la vijana lilitaka utawala wa Dola baada ya Mwl Nyerere, lakini kwa Awamu 2 (ya Mwinyi na Mkapa) halikufanikiwa. Hivyo lilibaki na kinyongo. Hili kundi dhamira yake kuu ni kujitajirisha kupitia "political power". Ni kundi la watu linaloamini siasa ndio mtaji mkuu wa mafanikio.
Kwa sababu hiyo, juhudi zikafanyika hadi likafanikiwa kumweka JMK kutawala ambapo pia kulikuwa na makubaliano ya siri ya kurithishana. Haikutokea hivyo kwa kuwa uchu wao wa madaraka ulimwezesha Magufuli kupata fursa ya kuwa Rais.
Matarajio ya kundi hilo la vijana wa TANU kuendelea kutawala Chama na Serikali kulizimwa kwenye Utawala wa Magufuli. Hivyo zikafanyika kila njama kumwondoa Magufuli. Hivyo basi, kuondoka kwa Magufuli, hatima ya Chama imerudi mikononi mwa waliokuwa Vijana wa TANU. Kwa kuwa tayari umri wao umeenda, wanachokifanya ni kuhakikisha watoto wao wako madarakani, katika chama na Serikali.
Kujibu swali la mada kuu, ni dhahiri Chama na Serikali, kwa sasa, uongozi wake uko kwa Watoto wa Vijana wa TANU. Vijana wa CCM wamewekwa kando kwa sababu hawana msingi kichama.