Kati ya Simba na Yanga ni nani amepangiwa kundi gumu Klabu Bingwa?

Kati ya Simba na Yanga ni nani amepangiwa kundi gumu Klabu Bingwa?

Mr Lukwaro

JF-Expert Member
Joined
Jun 3, 2023
Posts
359
Reaction score
629
IMG-20240312-WA0073.jpg
Baada Ya hatua ya Makundi kwa sasa ni Robo Fainali, Timu zetu mbili za Tanzania zimepangwa na Wababe wa soka la Afrika.

Wengine wanasema hii ndo ilipangwa kuziangusha Tumu za Tanzania, Japo hakuna uthibitisho.

Wengine wamekuwa na mtizamo chanya na kuona kama Soka la Tanzania limekuwa, na Kuzifunga timu hizo , Italeta furaha mara Dufu.

Kwako wewe Mdau, Bila kujali Itikadi za kishabiki.

Simba vs Al Ahly
Yanga vs Mamelodi

Nani mwenye Posibility ya kupita hatua ya Robo fainali CAF?
 
Simba timu zote ameshacheza nazo anazifahamu vizuri ila yanga hakuna hata timu moja aliyowahi kucheza nayo hivyo yanga ndo ana kundi gumu.
 
Mgeni ndie mwenye alama ya kamba mguuni.
Uto ajitahidi sana,ugeni wake uwe wenyeji wa hiyo miamba atakayo kutana nao.
SIMBA HAO WOTE ANAWAJUA.
 
simba timu zote ameshacheza nazo anazifahamu vizuri ila yanga hakuna hata timu moja aliyowahi kucheza nayo hivyo yanga ndo ana kundi gumu
Una maanisha nini mkuu? Hivi Simba na Mamelod walitokaje?
Yanga na Ahly je? hawajawahi kucheza??
 
simba timu zote ameshacheza nazo anazifahamu vizuri ila yanga hakuna hata timu moja aliyowahi kucheza nayo hivyo yanga ndo ana kundi gumu
Yanga mwenyewe pia kwenye kundi hilo ni mgumu na huenda ndiye anaongoza kwa ugumu.
Record hizi ni za mechi za Premia league na mashindano ya CAF mdimu huu, kabla ya mechi zilizochezwa hapo jana.
1.
Screenshot_20231008-130513_Samsung Internet.jpg

2.
Screenshot_20231008-130600_Samsung Internet.jpg

3.
Screenshot_20231008-130646_Samsung Internet.jpg



Goup la Simba
1.
Screenshot_20231008-131407_Chrome.jpg

2.
Screenshot_20231008-131340_Chrome.jpg

3.
Screenshot_20231008-131312_Chrome.jpg
 
Wote waliopangwa na Simba hawalali wanawazia kwa mkapa machinjioni wakati waliopangwa na yanga wanalala na hawana hofu na machinjio ya mkapa
 
simba timu zote ameshacheza nazo anazifahamu vizuri ila yanga hakuna hata timu moja aliyowahi kucheza nayo hivyo yanga ndo ana kundi gumu
Mawazo finyu.
Vikosi vinabadilika. Juwaneng iliyomtoa Simba siyo ya Sasa hivi na Wydad pia imebadilika na itabadilika dirisha dogo.
Hata Yanga anaweza kuchukua striker wa milioni 70 kwa mwezi kwa mkataba wa mwaka moja, Simba nae hivyohivyo.

Sasa hivi utasikia Yanga kaingia udhamini wa 2bn akatumia kununua striker.
Siku hizi hata timu za Tanzania zinaogopewa kwa sababu Kuna mashabiki wengi na mashabiki huvutia uwekezaji. Usishangae mchina akaweka mzigo wa kufa mtu watu wakachukua vyombo December.
 
Mawazo finyu.
Vikosi vinabadilika. Juwaneng iliyomtoa Simba siyo ya Sasa hivi na Wydad pia imebadilika na itabadiluka dirisha dogo. Hata Yanga anaweza kuchukua striker wa milioni 70 kwa mwezi kwa mkataba wa mwaka moja, Simba nae hivyohivyo.
Sasa hivi utasikia Yanga kaingia ushamini wa 2bn akatumia kununua striker. Siku hizi hata timu za Tanzania zinaogopewa kwa sababu Kuna mashabiki wengi na mashabiki huvutia uwekezaji. Usishamgae mchina akaweka mzigo wa kufanya mtu watu wakachukua vyombo December.
Seconded

Watu wanamjadili Yanga wa sasa Kwa rekodi zilizopita

Halafu akiwaprove wrong wanaanza siasa mara ooh kacheza na kibonde
 
Uwanjani mambo huwa ni tofauti kabisa ila kwenye karatasi yanga yupo kundi gumu zaidi ya Simba, sababu ni moja nayo ni rank za ubora wa timu. Yanga sidhani kama yupo juu ya wale waaljeria, hivyo Kuna milima miwili ya kupanda Kwa nguvu, waarabu wawili tena ni timu nzuri tu zenye ubora, al ahly na cr belouzdad then yanga. Simba yeye anaweza akajipapatua akashika kuanzia nafasi ya pili, timu mbili kwenye kundi la Simba hazipo juu ya Simba kwenye rank za ubora, hivyo on paper ni afuheni. The higher you go, the better you are, theoretically...lakini kwenye ground hayo mambo huwa tofauti anytime
 
Back
Top Bottom