Kati ya Spika mstaafu Pius Msekwa na Spika Dkt. Tulia nani anasema ukweli kuhusu Ubunge wa Halima Mdee na wenzake 18?

Kati ya Spika mstaafu Pius Msekwa na Spika Dkt. Tulia nani anasema ukweli kuhusu Ubunge wa Halima Mdee na wenzake 18?

Mzee Msekwa: Halima James Mdee na wenzake 18 walifukuzwa uanachama wa Chadema kwahiyo hawana chama. Uwepo wao bungeni ni kinyume cha katiba ya JMT ya 1977 niliyoshiriki kuitengeneza...

Katiba haitegemei Speaker! Hakuna mabadiliko ya Katiba yaliyotokea kati ya 2020 na 2022. Hivyo, Tulia (kama Speaker sasa) hana kipya cha kusema kuhusu ubunge wa kina Mdee.
 
Mmoja anaweza nisaidia barua ya chadema ikionesha wamefukuzwa chamani.

Pia angesaidia kuonesha maamuzi ya rufaa waliyokataa hado wabunge 19

Hi kitu inaonesha kama chama pia wamekubiliana nayo.
 
Mmoja anaweza nisaidia barua ya chadema ikionesha wamefukuzwa chamani.

Pia angesaidia kuonesha maamuzi ya rufaa waliyokataa hado wabunge 19

Hi kitu inaonesha kama chama pia wamekubiliana nayo.
Rufaa wamekata wabunge 6 tu.

Wabunge 13 waliridhika wamefukuzwa kihalali ndipo Ndugai akawaita gerejeni na kuwabatiza kwa maziwa na asali!
 
Tulia yuko sahihi linasubiri maamuzi ya Chadema

Mkutano mkuu wa Chadema ndio wenye mamlaka ya mwisho kuwahusu huo mkutano haujawahi itishwa

Mimi ni mmoja nikiyeongelea sana swala hili kuwa kama hao wabunge wa Chadema si halali kwa nini Chadema haiitishi mkutano mkuu utoe maamuzi kama katiba ya chadema inavyotaka?

Mimi mwenyewe nasubiri maamuzi ya mkutano mkuu wa Chadema kuhusu swala la akina Halima mdee na wenzie

Pius msekwa yuko wrong hajasoma katiba ya Chadema inasemaje kuhusu mamlaka ya mwisho ya mtu kufukukuzwa uanachama

Kama hawezi kuisoma sababu umri umeenda nashauri mtu mwingine aende akamsomee kwa sauti katiba ya Chadema mzee Msekwa

Tulia yuko sahihi mia kwa mia
 
Bwashee ujue tu kuwa hatuna Bunge Bali kuna kikao cha CCM pale mjengoni. Tulia ni Speaker tu radio iko Magogoni jumba jeupe.
Katika uzi huu wewe ndiyo umeainisha ukweli jinsi ulivyo, hako ka Tulia na takataka wenzake pale mjengoni ni toothless kwani wanaendeshwa kwa remote control na bi Urojo kutokea Magogoni.
 
Pius Msekwa anaijua katiba ya JMT kuliko mtanzania mwingine yoyote!
Katiba ya chadema ni sifuri haijui kabisa alitakiwa asome na katiba ya chadema inasemaje

Katiba ya chadema inatamka wazi kuwa mkutano mkuu ndio highest organ yenye uwezo wa kumfukuza mtu uanachama

Mkutano mkuu wa Chadema haujawahi kaa kuamua swala la akina mdee
 
Labda mzee Msekwa hajaisoma katiba ya Chadema!
 
Uanachama wao ulikoma tangu siku waliyofukuzwa uanachama, hapo hapahitajiki sababu za ziada. Muhimu ni kuwa walifukuzwa uanachama.

Ukumbuke chama kinafata sheria za inchi, sio mambo ya kuua Mtoto wako just because ww ndio umemzaa so Una mamlaka nae hapana,

Uwez Tu kuamka asubuh ukaanza kufukuza watu hakuna hayo mambo
 
Tulia yuko sahihi linasubiri maamuzi ya Chadema

Mkutano mkuu wa Chadema ndio wenye mamlaka ya mwisho kuwahusu huo mkutano haujawahi itishwa....

Hata tungesema kila kitu anachosema Mzee Msekwa ni sahihi, strategy ya CHADEMA ni ya kimbumbumbu sana!

Hakimu au judge akishaamua kesi fulani ndiyo imetoka. Kama hujaridhika, unapaswa kukata rufaa kwenye mahakama ya juu yake. Sio unasubiri hakimu au judge (kwenye ile ile mahakama iliyoamua hiyo kesi) abadilike ili wewe ufufue tena kesi yako pale. That’s nonsense!
 
Back
Top Bottom