Kati ya uMagufuli na Samia ni upi umejaa wahuni zaidi? Tuorodheshe matukio ya kihuni

Kati ya uMagufuli na Samia ni upi umejaa wahuni zaidi? Tuorodheshe matukio ya kihuni

1. Wakati wa JPM bei zilikuwa za kawaida lakini sasa bei za vitu zimepanda kwa zaidi ya 130%.

2. Wakati wa JPM watu walipata huduma katika Ofisi za umma bila rushwa lakini sasa ni taabu tupu.

3. Wakati wa JPM hakukuwa na ajali nyingi lakini sasa Ajali zimekuwa kama wimbo.

4. Wakati wa JPM wezi, vibaka, Panyaroads walifutiliwa mbali lakini sasa wametapakaa kila kona.
 
Vitu kupanda bei kiholela na serikali kusingizia Vita ya Urusi huku maisha yanakuwa Magumu.

Kula kwa kamba ya urefu wake.

Watu wachache kulamba Asali.

Wizi na ujambazi kurudi kwa kasi. Sasa hivi wenye vibanda vya mpesa na tigo pesa wanakaa kwa wasiwasi sana.

Mauwaji yameongezeka kwa hari ya juu. Watu wanauwana ni dalili ya kukosa uongozi madhubuti.

N. K
Haya ni baadhi,
Tutazidi kujazia kadri miaka inavyokwenda, hadi atimize mitano Kama Magu!
 
Kinachoitwa uwekezaji ni kukaribisha wezi kuiba rasilimali zetu.

Hakuna unyama uliofanyika kama kuwaondoa wamasai kwa kutumia majeshi yetu kwenye ardhi yao na kumpa mwekezaji.

Ni jambo la aibu mno kusitisha mradi wa Bwawa la Nyerere na kuanzisha mwingine wa Gesi.

Wizi na ubadhirifu wa fedha za miradi na huduma mbovu ni jambo la kawaida kabisa kwa sasa.

Kuruhusu wafanyabiashara kupandisha bei wanavyojisikia ni kitendo cha kuwaumiza wananchi ambacho serikali imekibariki.

Kwa ufupi ni kwamba awamu hii imejaa uovu mwingi kuwahi kutokea katika historia ya Taifa letu.
Ikumbukwe kuwa ufananisho wa haki Ni Hadi Samia aongoze miaka tano!
Kwa Sasa hayo maovu yake yanawekwa benki
 
Wale wa wamu ya 5 walikuwa zaidi ya wapigaji maana walitutangazia wamethibiti ufisadi na makusanyo ya mapato lakini fedha wakajigawa wenyewe kama akina Sabaya! Fikiria mpaka leo hatuwi ile Trilion 1.5 iliko! Hatujui katika unuuzi wa ndege zetu chenji zilibaki ngapi na nani anazo!???
 
Mnadanganywa sana nyie watu. Mnatumia nguvu kubwa kumchafua jpm. Tuseme ushahidi ulishaandaliwa kumshitaki Mbowe, tena mbona awamu hii ikaamua kuendelea nayo hiyo kesi? Si wangeacha tu. Hampendi sana kuambiwa kwamba Mbowe alishitakiwa na Serikali hii iliyopo. Mnaona kama ni doa siyo?

Sent from my TECNO PR651H using JamiiForums mobile app

..kesi ya mbowe ilitengenezwa na Ssh.

..alipoona kesi inakwenda vibaya, polisi, serikali,na mahakama, wanaadhirika, akaona waifute.

..nadhani hata huko nje anakotembelea mabeberu watakuwa wamemnong'oneza asiige ukatili wa waziwazi wa awamu ya 5.
 
Mtoa mada anadhani kupigwa risasi TL Ni Jambo zito zaidi ya kupigwa risasi raia wengine!
Uovu wa polisi kumpiga risasi raia yoyote kwa issue zozote zikiwemo issue za kiusalama, Ni uzito ule ule sawa sawa kwa ilivyotokea kwa TL

Kama mtoa mada anamind Sana issue ya risasi kwa TL na atupa lawama kwa utawala wa sukuma gang, ingawa Hana uthibitisho, hata sisi sukuma gang tunatupa lawama kwa wahuni wa utawala wa SSH kwa kumuua JPM,
 
Wafuasi wa Magufuli wanaituhumu serikali ya sasa kuwa ina wahuni, wakiongozwa na yule mtu wao aliyepelekwa Malawi na hashtag yake ya #KataaWahuni

Sasa nataka tuende kwa fact na records, mimi nataka waniambie ni uhuni gani umefanyika serikali ya Samia kushinda uhuni wa Serikali ya Magufuli

Kwa kuanzia tu, Kipindi cha Magufuli ndio mbunge alipigwa risasi katika viwanja vya Bunge na watu waliompiga kung'oa CCTV Camera zilizorekodi tukio

Kipindi cha Magufuli ndio watu walitekwa kwa wingi zaidi kama akina Kinguye, Ben Saanane, azory Gwanda, Mdude Chadema, Roma Mkatoliki, Mo Dewji, Abdul Nondo n.k

Kipindi cha Magufuli ndio mkuu wa mkoa huku akirekodiwa na Camera alivamia kituo cha Tv kuamrisha habari yake isomwe na wala hakuchukuliwa hatua yoyote

Kipindi cha Magufuli ndio tulisikia mkuu wa mkoa akipiga watu marufuku kuja kwenye 'mkoa wake'

Kipindi cha Magufuli ndio mtu kama Sabaya alitamba sana, na kuna matukio kibao kama ya ubakaji, uporaji, kubambikizia kesi n.k

Achilia mbali uhuni wa kuengua asilimia 90 ya wagombea wa upinzani kwenye uchaguzi Serikali za mitaa kwa kigezo kuwa hawajui kusoma wala kuandika

Achilia mbali kulazimisha na kuhonga wapinzani kujiuzulu ubunge na udiwani kisha kugombea tena jimbo hilo hilo ili Magufuli aonekane anapendwa

Ndio kipindi tumedanganywa miradi mikubwa tunajenga kwa fedha za ndani

Achilia mbali kauli za kihuni za Magufuli kama 'Baki na mavi yako nyumbani', 'Mnataka mpanuliwe wapi', na kusifia wake za watu hadharani

Huu ni uhuni mdogo sana kati ya uhuni mwingi aliokuwa akifanya Magufuli

Haya sasa niambieni matukio ya kihuni kwenye serikali ya Samia tulinganishe
Kwa sasa karibu wote whni...........................
 
..kesi ya mbowe ilitengenezwa na Ssh.

..alipoona kesi inakwenda vibaya, polisi, serikali,na mahakama, wanaadhirika, akaona waifute.

..nadhani hata huko nje anakotembelea mabeberu watakuwa wamemnong'oneza asiige ukatili wa waziwazi wa awamu ya 5.
Ni kweli kisha wakajidai ku-back date tarehe za faili kuandaliwa eti akisubiriwa kizito wa Bomang'ombe huku aliyepisha kiti na hayupo kujitetea akisingiziwa ndiye aliianzisha..................dunia itawaumbua mpaka basi. Kweli yule jamaa kama alinuia kumweka nyuma ya nondo angekamata wadogo amwache mkubwa? Hapana ni uongo ambao walioshiriki hawakujipanga kitaaluma
 
Back
Top Bottom