Kati ya uMagufuli na Samia ni upi umejaa wahuni zaidi? Tuorodheshe matukio ya kihuni

Kati ya uMagufuli na Samia ni upi umejaa wahuni zaidi? Tuorodheshe matukio ya kihuni

Hakika umenena vema. Awamu
ya 5 ilizidiwa ustaarabu hata na maisha ya wanyama. Fisi
pamoja na tabia zake za ajabu,
lakini hatafuni watoto wake, ila
hapa tulikuwa na Rais anasikia
faraja kuondoa uhai wa wale
aliorakiwa kuwalinda.
Nitajie watu watano tu waliyouliwa na Magufuli kama kweli alikuwa anauwa raia wake.
 
Nimekuuliza swali nilitegemea unipe majibu. Mfano Uingereza huko wananchi wanaandamana bei za vitu zimepanda sana nako ni Samia amepandisha?
Uingereza gesi imepanda. Ni kwa Sababu gesi ya Urusi.

Sisi tunanunua kila kitu Urusi?
 
Mleta mada, naamini anataka
hoja halisia, mambo
yanayoenekana wazi. Kupigwa
risasi Tundu Lisu, utalinganisha
na kauli ya kila mmoja ale kwa
urefu wa kamba yake?
Kuwasweka ndani watu
aluowaita wahujumu uchumi
kumbe nia yake ni kuwapora
pesa zao ili apate utajiri yeye
binafsi, utalinganisha na
mfumko wa bei ambao ni
matokea ya mambo
mbalimbali ya ndani na nje ya
nchi?
Hatukawahi kuwa serikali ya
kihuni, kishetani, na yenye
ubaradhuli wa kiwango
kisichoelezeka, kama ile ya
marehemu Magufuli. Mambo
aliyokuwa akifanya ni mambo
ya kishetani kabisa: kuua watu,
kuteka, kuwabambikia watu
kesi za uhujumu uchumi,
kwapumbaza watu wenye akili
ndogo waobe kuwa nchi
inapaa ilihali ilikuwa
ikiporomoka kila kukicha.
Mleta mada kataja hadi suala la Magufuli kusifia wake za watu, hilo nalo kalitaja kama moja ya mambo ya kihuni kwenye awamu ya tano ila wewe nadhani hukuona.
Sasa mimi nataja uhuni wa Samia kuruhusu ufisadi wazi wazi kwa kuwaambia wajipimie wasiibe sana ila wewe unaona ni jambo dogo rais wa nchi kuongea hivyo.
 
Ubaya ni ubaya tu, na wote hautakiwi kufanyiwa mwanadamu, haijalishi uwe wa large scale au small scale.

Hii tabia yenu ya kuendelea kulinganisha ubaya wa serikali iliyopita na hii ya sasa unawadumaza wengi kiakili, hamuoni ubaya wa serikali iliyopo madarakani, na ndio maana mnajikuta mnageuka kuwa chawa bila kujitambua.

Lakini pia mnaidumaza serikali iliyopo madarakani, iendelee kujiona ni ya malaika wakati nayo imejaa mabaya yake, uvunjifu wa sheria wa wazi inayoukumbatia kwenu mnaona ni jambo la kawaida, na kwa ujinga wenu mnachangia kuiendeleza tabia hiyo.

Kabisa; uchawa ndiyo cancer ya hii nchi.
 
Ni dhahiri awamu ya 5 ilizidi kuwa wahuni na hawakupaswa kabisa kupewa madaraka ya juu kabisa ndani ya nchi hii.
 
Jonny,
Matukio gani mapya ambayo hayakuwepo kabla ya Magufuli? Wewe hujaona hata kidogo hicho kiini macho cha CAG? CCM ni CCM, walikaa na kujua wampakazie vipi JPM. Wewe unaamini zile ndege hazikununuliwa? Lile bwawa la umeme ni baya kwa nchi? SGR ? Hujaona EPA, IPTL, Singasinga, Simba Trust etc etc etc huwa mnasahau mapema sana.
CAG aliandika ile Kwa maelekezo, uwe unachanganya na zako
Kipindi kipi mkuu ambacho mbunge aliwahi kupigwa risasi maeneo ya Bunge?
Ni kipindi kipi mkuu wa mkoa amewahi kuvamia kituo cha Tv na walinzi wa Ikulu akiamrisha habari zake zitangazwe?
Ni kipindi kipi wagombea wa upinzani walienguliwa kwa asilimia 90 kwa kuwa hawajui kusoma?

Anyway mimi sikumbuki labda vilikuwepo, lakini haswa mimi nalinganiha utawala wa Samia ambao unatajwa kujaa wahuni na utawala wa Magufuli, upi zaidi?
 
Mbona unakuwa mzito kukubali tu moja kwa moja uhuni wa Samia hadi umuhusishe na Magufuli? Hili limeisha kuwa ni uhuni wa Samia.
Mkuu ulikuwa ukifuatilia ile kesi? Kama hukuwa unafuatilia ni kuwa watuhumiwa wote na mashahidi wote walikuwa wameshaandaliwa mwaka 2020 na ushahidi wao ukimu implicate Mbowe kama mtuhumiwa mkuu

Samia ana Makosa ila Magufuli anayo pia
 
Samia anasema kabisa wajipimie wasivimbiwe, maelezo ya Samia yapo wazi kwamba sawa wanaiba inajulikana ila wasipitilize hadi kuathiri miradi na hadi mfano alitoa. Kwahiyo mkuu ni wewe ndio unajaribu kutaka kupindisha alichokikusudia Samia.

Na ndio maana hawezi kuja kutolea ufafanuzi hiyo kauli, ni uhuni ambao unataka kuukataa.
Kauli ya Samia naikumbuka vizuri na sio ulichoandika hapo
 
Mleta mada, ana hoja kubwa kwa watu wenye akili.

Utawala wa kihuni wa awamu ya 5, utafanyiwa rejea kwa miaka mingi kama mfano mbaya wa utawala ambao nchi iliwahi kutumbukia.

Ulikuwa utawala wa kishetani, kwa kioimo chochote kile, kwa mtu aliye na akili timamu.
Uko sawa mkuu, uhuni waliofanyiwa vyeti feki, wanufaika wa wafanya kazi hewa, wauza ngada, wezi, mafisadi kina singasinga+

Ni vigumu kusahaulika kwa sababu hata wewe unakuhusu, utasahauje kwa mfano.?

Kwa hiyo watajwa hapo juu ndio unawaita wenye akili kubwa, siyo??

Ujinga mwingine muwe mnakataa kuzaliwa nao
 
Mkuu ulikuwa ukifuatilia ile kesi?
Kama hukuwa unafuatilia ni kuwa watuhumiwa wote na
mashahidi wote walikuwa
wameshaandaliwa mwaka
2020 na ushahidi wao ukimu
implicate Mbowe kama
mtuhumiwa mkuu
Samia ana Makosa ila Magufuli
anayo pia
Mkuu tunazungumzia kukamatwa na kuwekwa ndani kwa Mbowe, ambalo ni tukio lililotokea awamu ya Samia.
 
Wafuasi wa Magufuli wanaituhumu serikali ya sasa kuwa ina wahuni, wakiongozwa na yule mtu wao aliyepelekwa Malawi na hashtag yake ya #KataaWahuni

Sasa nataka tuende kwa fact na records, mimi nataka waniambie ni uhuni gani umefanyika serikali ya Samia kushinda uhuni wa Serikali ya Magufuli

Kwa kuanzia tu, Kipindi cha Magufuli ndio mbunge alipigwa risasi katika viwanja vya Bunge na watu waliompiga kung'oa CCTV Camera zilizorekodi tukio

Kipindi cha Magufuli ndio watu walitekwa kwa wingi zaidi kama akina Kinguye, Ben Saanane, azory Gwanda, Mdude Chadema, Roma Mkatoliki, Mo Dewji, Abdul Nondo n.k

Kipindi cha Magufuli ndio mkuu wa mkoa huku akirekodiwa na Camera alivamia kituo cha Tv kuamrisha habari yake isomwe na wala hakuchukuliwa hatua yoyote

Kipindi cha Magufuli ndio tulisikia mkuu wa mkoa akipiga watu marufuku kuja kwenye 'mkoa wake'

Kipindi cha Magufuli ndio mtu kama Sabaya alitamba sana, na kuna matukio kibao kama ya ubakaji, uporaji, kubambikizia kesi n.k

Achilia mbali uhuni wa kuengua asilimia 90 ya wagombea wa upinzani kwenye uchaguzi Serikali za mitaa kwa kigezo kuwa hawajui kusoma wala kuandika

Achilia mbali kulazimisha na kuhonga wapinzani kujiuzulu ubunge na udiwani kisha kugombea tena jimbo hilo hilo ili Magufuli aonekane anapendwa

Ndio kipindi tumedanganywa miradi mikubwa tunajenga kwa fedha za ndani

Achilia mbali kauli za kihuni za Magufuli kama 'Baki na mavi yako nyumbani', 'Mnataka mpanuliwe wapi', na kusifia wake za watu hadharani

Huu ni uhuni mdogo sana kati ya uhuni mwingi aliokuwa akifanya Magufuli

Haya sasa niambieni matukio ya kihuni kwenye serikali ya Samia tulinganishe
Wote ni wahuni kwani Samia alikuwa makamu wa rais, baada ya kushika madaraka kawarudisha mafisadi wote na sasa wanaitafuna nchi kwa raha zao huku wananchi tukipandishiwa bei ya kila kitu. CCM wote majizi
 
Awamu zote, kuna makosa Serikali hufanya lakini yale ya awamu ya 5 hayakuwa makosa bali ni ushetani. Shetani aliishi ikulu, akafanya kazi ya kuliangamiza Taifa, akawapata mashetani wadogo wa kusaidia kuangiza Taifa, wale wa kumwimbia sifa kwa nia ya kuwapumbaza waliokuwa na uelewa duni.
Propaganda tu hizo mkuu.

Kama wewe sio mhusika basi umedanganyika.

Magu alipambana kulinda nchi.

Wezi hawakumtaka ili kumuondoa ilipaswa watengeneze uongo na moja wapo ya uongo wenyewe ndio huo unaousema.

If you want to remove the Dog just give it a bad name.

Ndio walichofanya.
 
Wafuasi wa Magufuli wanaituhumu serikali ya sasa kuwa ina wahuni, wakiongozwa na yule mtu wao aliyepelekwa Malawi na hashtag yake ya #KataaWahuni

Sasa nataka tuende kwa fact na records, mimi nataka waniambie ni uhuni gani umefanyika serikali ya Samia kushinda uhuni wa Serikali ya Magufuli

Kwa kuanzia tu, Kipindi cha Magufuli ndio mbunge alipigwa risasi katika viwanja vya Bunge na watu waliompiga kung'oa CCTV Camera zilizorekodi tukio

Kipindi cha Magufuli ndio watu walitekwa kwa wingi zaidi kama akina Kinguye, Ben Saanane, azory Gwanda, Mdude Chadema, Roma Mkatoliki, Mo Dewji, Abdul Nondo n.k

Kipindi cha Magufuli ndio mkuu wa mkoa huku akirekodiwa na Camera alivamia kituo cha Tv kuamrisha habari yake isomwe na wala hakuchukuliwa hatua yoyote

Kipindi cha Magufuli ndio tulisikia mkuu wa mkoa akipiga watu marufuku kuja kwenye 'mkoa wake'

Kipindi cha Magufuli ndio mtu kama Sabaya alitamba sana, na kuna matukio kibao kama ya ubakaji, uporaji, kubambikizia kesi n.k

Achilia mbali uhuni wa kuengua asilimia 90 ya wagombea wa upinzani kwenye uchaguzi Serikali za mitaa kwa kigezo kuwa hawajui kusoma wala kuandika

Achilia mbali kulazimisha na kuhonga wapinzani kujiuzulu ubunge na udiwani kisha kugombea tena jimbo hilo hilo ili Magufuli aonekane anapendwa

Ndio kipindi tumedanganywa miradi mikubwa tunajenga kwa fedha za ndani

Achilia mbali kauli za kihuni za Magufuli kama 'Baki na mavi yako nyumbani', 'Mnataka mpanuliwe wapi', na kusifia wake za watu hadharani

Huu ni uhuni mdogo sana kati ya uhuni mwingi aliokuwa akifanya Magufuli

Haya sasa niambieni matukio ya kihuni kwenye serikali ya Samia tulinganishe
Mm sijawahi kuipenda ccm. Ila nampenda sasmkia huyu ni raisi mwema na muungwana. Hatutaki kuongozwa KIFASHIST. KWA KISINGIZIO CHA KUJENGEWA MADARAJA.
MAISHA YA BNADAMU CO MADARAJA
MUNGU FUNDI
 
Back
Top Bottom