Kati ya uMagufuli na Samia ni upi umejaa wahuni zaidi? Tuorodheshe matukio ya kihuni

Kati ya uMagufuli na Samia ni upi umejaa wahuni zaidi? Tuorodheshe matukio ya kihuni

Wafuasi wa Magufuli wanaituhumu serikali ya sasa kuwa ina wahuni, wakiongozwa na yule mtu wao aliyepelekwa Malawi na hashtag yake ya #KataaWahuni

Sasa nataka tuende kwa fact na records, mimi nataka waniambie ni uhuni gani umefanyika serikali ya Samia kushinda uhuni wa Serikali ya Magufuli

Kwa kuanzia tu, Kipindi cha Magufuli ndio mbunge alipigwa risasi katika viwanja vya Bunge na watu waliompiga kung'oa CCTV Camera zilizorekodi tukio

Kipindi cha Magufuli ndio watu walitekwa kwa wingi zaidi kama akina Kinguye, Ben Saanane, azory Gwanda, Mdude Chadema, Roma Mkatoliki, Mo Dewji, Abdul Nondo n.k

Kipindi cha Magufuli ndio mkuu wa mkoa huku akirekodiwa na Camera alivamia kituo cha Tv kuamrisha habari yake isomwe na wala hakuchukuliwa hatua yoyote

Kipindi cha Magufuli ndio tulisikia mkuu wa mkoa akipiga watu marufuku kuja kwenye 'mkoa wake'

Kipindi cha Magufuli ndio mtu kama Sabaya alitamba sana, na kuna matukio kibao kama ya ubakaji, uporaji, kubambikizia kesi n.k

Achilia mbali uhuni wa kuengua asilimia 90 ya wagombea wa upinzani kwenye uchaguzi Serikali za mitaa kwa kigezo kuwa hawajui kusoma wala kuandika

Achilia mbali kulazimisha na kuhonga wapinzani kujiuzulu ubunge na udiwani kisha kugombea tena jimbo hilo hilo ili Magufuli aonekane anapendwa

Ndio kipindi tumedanganywa miradi mikubwa tunajenga kwa fedha za ndani

Achilia mbali kauli za kihuni za Magufuli kama 'Baki na mavi yako nyumbani', 'Mnataka mpanuliwe wapi', na kusifia wake za watu hadharani

Huu ni uhuni mdogo sana kati ya uhuni mwingi aliokuwa akifanya Magufuli

Haya sasa niambieni matukio ya kihuni kwenye serikali ya Samia tulinganishe
Vitu kupanda bei kiholela na serikali kusingizia Vita ya Urusi huku maisha yanakuwa Magumu.

Kula kwa kamba ya urefu wake.

Watu wachache kulamba Asali.

Wizi na ujambazi kurudi kwa kasi. Sasa hivi wenye vibanda vya mpesa na tigo pesa wanakaa kwa wasiwasi sana.

Mauwaji yameongezeka kwa hari ya juu. Watu wanauwana ni dalili ya kukosa uongozi madhubuti.

N. K
 
Aliewaroga Nyie mazwazwa waTanzania alijua kuwakomesha, kwa iyo unahalalisha ujinga unaofanywa na awamu ya 6 kwa kisingizio cha kulinganisha Na ufedhuli uliopita ndio unaona ubora wa uongozi! Tuache utaahira kosa likemewe kwa kizazi na ustawi wa Taifa letu kwa miaka ya mbele, nchii ipo hata baada ya SSH kuondoka, je wanao na wajukuu wako hushawahi kuwawazia maisha yao ya baadae? Acha upunguani kila wakati kumuwaza aliepo, mavi ya kale hayana harufu tena, tutafte tiba ya uhuni wa nyie maCCM Na walamba asali wa Chadomo Na wanafiki wa Zitto
Jibu swali la mleta mada kati ya muungwana Samia na shetani magu nani ana ubaya zaidi?
 
Kwani mimi nimesema ni malaika?

Ndio alikuwa makamu wa Rais, kila Rais aliyewahi kutokea nchi hii alikuwa sehemu ya serikali ya Rais aliyepita, lakini kila uongozi unakuwa na tofauti zake
Hivi unaifahamu maana ya "collective responsibility" hasa pale ilipotumika ili kulinda maslahi ya CCM?
 
Vitu kupanda bei kiholela na serikali kusingizia Vita ya Urusi huku maisha yanakuwa Magumu.

Kula kwa kamba ya urefu wake.

Watu wachache kulamba Asali.

Wizi na ujambazi kurudi kwa kasi. Sasa hivi wenye vibanda vya mpesa na tigo pesa wanakaa kwa wasiwasi sana.

Mauwaji yameongezeka kwa hari ya juu. Watu wanauwana ni dalili ya kukosa uongozi madhubuti.

N. K
Very minor and irrelevant. Kwani hujui chanzo cha bei za vitu kupanda bei? Dunia nzima inahaha, kote huko kapandisha Samia?
 
Sasa wewe vitu kupanda bei, mbona ni nchi zote? Unafuatilia siasa za Kenya? Sasa hivi wapo kwenye kampeni mfumuko wa bei ndio ajenda kuu sasa
Mvua kuwa chache, kupanda kwa bei ya mafuta duniani ndio imechangia kwa kiasi kikubwa
Hayo ya kula kwa urefu wa kamba sijui kulamba asali ni kauli tu ambazo watu wame twist maana

Mimi nataka unitajie matendo ya kihuni yaliyofanywa na serikali
 
Hii siyo hoja, ni haja kubwa!

Mleta mada, hii mada yako inasaidia nini maisha ya watanzania?

Jinga kabisa
 
Samia anaruhusu wazi wazi watu kula kwa urefu wa kamba zao na wakati huo huo ile nidhamu ambayo walikuwa nayo kaita ni nidhamu ya uoga na huku yeye hafanyi lolote kujenga nidhamu kwa watumishi wa serikali na matokeo yake sasa hakuna tena hata hiyo nidhamu ya uoga na watu wanakula tu kwa urefu wa kamba zao bila hofu.
Kuruhusu watu kula kwa urefu wa kamba kwani maana yake ni nini? Wewe ndio umeamua kuipa maana unayotaka wewe ili ulaumu lakini ina maanisha mtu kuishi kutokana na kipato chake

Ukosefu wa nidhamu kwa watumishi ni tatizo sugu la enzi hata kwa Magufuli lilikuwepo
 
Hii siyo hoja, ni haja kubwa!

Mleta mada, hii mada yako inasaidia nini maisha ya watanzania?

Jinga kabisa
Kajinyonge ukazikwe Chato kama imekuuma, wewe kumsifia Magufuli kila siku kunasaidiaje watanzania
 
Kesi iliandaliwa kipindi cha
Magufuli na ushahidi pia ulitengenezwq kipindi hicho
Hapa Samia anawajibika lakini
pia Magufuli ana mchango
wake, nawapa wote 50/50
Ukileta issue za 50/50 basi pia huyo Samia nae achukue 50 kwa uhuni wote wa awamu ambayo yeye ndio alikuwa makamu wa rais wa utawala wa Magufuli. We kubali tu aliyemkamata Mbowe na kumuwela ndani kwa tuhuma za ugaidi ni Samia na uzuri alishaeleza msimamo wake juu ya hiyo kesi ya Mbowe pale alipohojiwa na bbc.
 
Kuruhusu watu kula kwa urefu
wa kamba kwani maana yake ni nini? Wewe ndio umeamua
kuipa maana unayotaka wewe
ili ulaumu lakini ina maanisha
mtu kuishi kutokana na kipato
chake
Ukosefu wa nidhamu kwa
watumishi ni tatizo sugu la enzi
hata kwa Magufuli lilikuwepo
Nilidhani ulitaka uambiwe uhuni wa awamu hii, kumbe haupo hapa kukubaliana na hilo na ndio maana unajaribu kutetea ili kupinga kwamba awamu hii hakuna uhuni.

Kama unadhani nilivyomuelewa mimi sio sahihi na cha ajabu ndio tumemuelewa hivyo, je yeye mwenyewe Samia mbona hajarekebisha kwa kutoa ufafanuzi wa kauli yake ya kula kwa urefu wa kamba? We wewe dalili gani ya kuthibitisha kwamba ulivyomuelewa wewe ndio sahihi katika awamu hii ya watoto wa mjini?

Magufuli alijaribu kuweka nidhamu kwa kiwango alichoweza hata kama ilikuwa ni nidhamu za hofu ila zilisaidia kwa kiasi chake, sasa niambie Samia yeye toka aseme ni nidhamu za uoga yeye kafanya nini kujenga nidhamu ya za hiari?
 
Very minor and irrelevant. Kwani hujui chanzo cha bei za vitu kupanda bei? Dunia nzima inahaha, kote huko kapandisha Samia?
Mawazo yenu yanaishia kumsikiliza Rais Wala hamjui kutumia bongo zunu. Itabidi mzigawe kwa wengine hizo bongo wazitumie.
 
Sasa wewe vitu kupanda bei, mbona ni nchi zote? Unafuatilia siasa za Kenya? Sasa hivi wapo kwenye kampeni mfumuko wa bei ndio ajenda kuu sasa
Mvua kuwa chache, kupanda kwa bei ya mafuta duniani ndio imechangia kwa kiasi kikubwa
Hayo ya kula kwa urefu wa kamba sijui kulamba asali ni kauli tu ambazo watu wame twist maana

Mimi nataka unitajie matendo ya kihuni yaliyofanywa na serikali
Kwa wewe unamacho?

Akili si umeweka juu ya mti?
 
Kinachoitwa uwekezaji ni kukaribisha wezi kuiba rasilimali zetu.

Hakuna unyama uliofanyika kama kuwaondoa wamasai kwa kutumia majeshi yetu kwenye ardhi yao na kumpa mwekezaji.

Ni jambo la aibu mno kusitisha mradi wa Bwawa la Nyerere na kuanzisha mwingine wa Gesi.

Wizi na ubadhirifu wa fedha za miradi na huduma mbovu ni jambo la kawaida kabisa kwa sasa.

Kuruhusu wafanyabiashara kupandisha bei wanavyojisikia ni kitendo cha kuwaumiza wananchi ambacho serikali imekibariki.

Kwa ufupi ni kwamba awamu hii imejaa uovu mwingi kuwahi kutokea katika historia ya Taifa letu.
 
Mawazo yenu yanaishia kumsikiliza Rais Wala hamjui kutumia bongo zunu. Itabidi mzigawe kwa wengine hizo bongo wazitumie.
Nimekuuliza swali nilitegemea unipe majibu. Mfano Uingereza huko wananchi wanaandamana bei za vitu zimepanda sana nako ni Samia amepandisha?
 
Upuuzitu umeandika hapa. Mkiambiwa vijana wa chadema ni malofa mnabisha. Hivi tundu lisu Anapigwa risasi Alafu mpata dereva wake anaenda kujificha nae hawataki atoe ushirikiano na polisi hivi mpaka hapo Mjajua tu kwamba tukio lile lilipangwa na chadema wenyewe?

Tumieni Akili Hata kidogo basi yakufikiria. Na sio ushabiki wakijinga mwenzenu Mwenyekiti kashalambishwa Asali nyie mnabaki kuropoka tu mitandaoni.
 
Back
Top Bottom