Ila ile awamu ya 5, awamu ya Jiwe, ilikuwa awamu ya uongozi wa kibaradhuli.
Uongozi unaoua wanaokosoa, ni uongozi wa kishetani, ambao hauwezi kupata nafasi ya kuoshwa kwa namna yoyote ile.
Marehemu Magufuli ataendelea kukumbukwa kwa vizazi vingi kama mtawala baradhuli, muuaji, mtesaji na ambaye hakukubali kukosolewa kutokana na uuaji, utekaji na utesaji watu. Makosa mengine yote, kama uwongo na kuharibu uchumi, kuvunja haki za uhuru wa watu, udikteta, kutapanya pesa ya umma, uporaji wa pesa za watu na kuwabambikia watu kesi, ataweza kusamehewa lakini ushetani ule wa kuua na kuteka watu, kamwe hautasahaulika. Alijipa mamlaka ya kuondoa uhai wa watu, kama vile yeye ndiye anayeugawa, hakujua kabisa, shetani alimpumbaza, hata asijue kuwa hata yeye hawezi kukikwepa kifo.
Watawala na sisi sote tulio hai leo, tuogope kutenda maovu, tuogope na tusisogelee wala kuwaza kuwaua wanadamu wenzetu. Uhai wa mtu ni mali ya Mungu, ndiye aliyetupatia, na ndiye mwenye uwezo wa kuundoa.