Kati ya uMagufuli na Samia ni upi umejaa wahuni zaidi? Tuorodheshe matukio ya kihuni

1. Wakati wa JPM bei zilikuwa za kawaida lakini sasa bei za vitu zimepanda kwa zaidi ya 130%.

2. Wakati wa JPM watu walipata huduma katika Ofisi za umma bila rushwa lakini sasa ni taabu tupu.

3. Wakati wa JPM hakukuwa na ajali nyingi lakini sasa Ajali zimekuwa kama wimbo.

4. Wakati wa JPM wezi, vibaka, Panyaroads walifutiliwa mbali lakini sasa wametapakaa kila kona.
 
Haya ni baadhi,
Tutazidi kujazia kadri miaka inavyokwenda, hadi atimize mitano Kama Magu!
 
Ikumbukwe kuwa ufananisho wa haki Ni Hadi Samia aongoze miaka tano!
Kwa Sasa hayo maovu yake yanawekwa benki
 
Wale wa wamu ya 5 walikuwa zaidi ya wapigaji maana walitutangazia wamethibiti ufisadi na makusanyo ya mapato lakini fedha wakajigawa wenyewe kama akina Sabaya! Fikiria mpaka leo hatuwi ile Trilion 1.5 iliko! Hatujui katika unuuzi wa ndege zetu chenji zilibaki ngapi na nani anazo!???
 

..kesi ya mbowe ilitengenezwa na Ssh.

..alipoona kesi inakwenda vibaya, polisi, serikali,na mahakama, wanaadhirika, akaona waifute.

..nadhani hata huko nje anakotembelea mabeberu watakuwa wamemnong'oneza asiige ukatili wa waziwazi wa awamu ya 5.
 
Mtoa mada anadhani kupigwa risasi TL Ni Jambo zito zaidi ya kupigwa risasi raia wengine!
Uovu wa polisi kumpiga risasi raia yoyote kwa issue zozote zikiwemo issue za kiusalama, Ni uzito ule ule sawa sawa kwa ilivyotokea kwa TL

Kama mtoa mada anamind Sana issue ya risasi kwa TL na atupa lawama kwa utawala wa sukuma gang, ingawa Hana uthibitisho, hata sisi sukuma gang tunatupa lawama kwa wahuni wa utawala wa SSH kwa kumuua JPM,
 
Kwa sasa karibu wote whni...........................
 
..kesi ya mbowe ilitengenezwa na Ssh.

..alipoona kesi inakwenda vibaya, polisi, serikali,na mahakama, wanaadhirika, akaona waifute.

..nadhani hata huko nje anakotembelea mabeberu watakuwa wamemnong'oneza asiige ukatili wa waziwazi wa awamu ya 5.
Ni kweli kisha wakajidai ku-back date tarehe za faili kuandaliwa eti akisubiriwa kizito wa Bomang'ombe huku aliyepisha kiti na hayupo kujitetea akisingiziwa ndiye aliianzisha..................dunia itawaumbua mpaka basi. Kweli yule jamaa kama alinuia kumweka nyuma ya nondo angekamata wadogo amwache mkubwa? Hapana ni uongo ambao walioshiriki hawakujipanga kitaaluma
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…