Kati ya Viongozi hawa Tumuamini nani , mbona wanatufanya Watanzania ni wajinga kiasi hiki?

Kati ya Viongozi hawa Tumuamini nani , mbona wanatufanya Watanzania ni wajinga kiasi hiki?

Erythrocyte

JF-Expert Member
Joined
Nov 6, 2012
Posts
128,308
Reaction score
245,426
Inawezekana ni kweli kwamba Watanzania ni wajinga na hawatunzi kumbukumbu kutokana na ujinga wao , lakini siamini kama watu hawa ni mbumbumbu kiasi cha kudanganywa kibwege namna hii.

John_Heche._on_Instagram:_“Sasa_hapa_tumuamini_nani?_Hivi_kuna_mtu_ana_matumaini_na_viongozi_w...jpg
 
Inawezekana ni kweli kwamba Watanzania ni wajinga na hawatunzi kumbukumbu kutokana na ujinga wao , lakini siamini kama watu hawa ni mbumbumbu kiasi cha kudanganywa kibwege namna hii

View attachment 1770962
Ili kubalansi story yako ingependeza kwenye uzi huu na Magufuli angekuwa hai ,kwa sasa hii ni porojo tu
 
Inawezekana ni kweli kwamba Watanzania ni wajinga na hawatunzi kumbukumbu kutokana na ujinga wao , lakini siamini kama watu hawa ni mbumbumbu kiasi cha kudanganywa kibwege namna hii

View attachment 1770962
Tunafanya rating kwa kuangalia kwenye kauli zao za nyuma. Jitu lipi limekuwa libabe likiongea mauongo tuuu na lisilopenda watu wakweli vs mtu mkweli asiyependa uongo na ambaye huko nyuma kauli zake hazina mawaaa.

Mitano tena kwa Samia
 
Hayo ni maswala ya kisekta. Naamini Mama Samia amezungumzia ajira za moja kwa moja toka serikalini. Za Magufuli itakuwa pamoja na zinazoletwa na miradi mikubwa ya uwekezaji, viwanda kilimo nk. Changamsha akili acha kuwa tegemezi hadi ktk kufikiri mambo madogo madogo.
 
Inawezekana ni kweli kwamba Watanzania ni wajinga na hawatunzi kumbukumbu kutokana na ujinga wao , lakini siamini kama watu hawa ni mbumbumbu kiasi cha kudanganywa kibwege namna hii

View attachment 1770962
Itatuchukua muda kuzoea, lakini mama Samia ameamua kuivua Tanzania gwanda la uwongo na kuivika nguo ya ukweli.

Magufuli alikuwa anaishi kwenye dunia ya UWONGO. Angalia hapa;
  • Alidanganya PhD yake
  • Alidanganya Makainikia kuwa tunapata Tsh Trilion 450
  • Alidanganya kukua kwa uchumi kuwa unakuwa kwa 7.9% wakati Ni 4.2%
  • Alidanganya kuwa tunajenga miradi mikubwa kwa fedha zetu wakati anakopa Benki za kimataifa
-Alidanganya uchaguzi wa Serikali za Mitaa 2019
  • Alidanganya uchaguzi Mkuu 2020
  • Alidanganya kuwa COVID 19 haiko Tanzania

Hata alipokufa;
-Majaliwa aliendelea kudanganya kuwa Rais anapitia mafaili

LAKINI:
Ni SSH aliyetuhabarisha kwa mara ya kwanza kuwa Mwendazake anaumwa na anakaguliwa. Hatimaye akatutangazia kuwa Mwendazake HATUNAYE

Na hapo ndiyo mwanzo wa Tanzania kuanza kuishi kwenye Dunia ya UKWELI, tumzoee Mama Samia
 
Kila mtu hupewa talanta kulingana na uwezo wake. Wengine tano, wengine mbili na wengine moja. Muda, nafasi na maono mtu aliyonayo ndio hasa vinavyoleta matokeo tarajiwa. Wakati wanasema, walikuwa wanaona.
 
Kuna mmoja hapo alishawahi pia kudanganya bungeni kuhusu ajira elfu 5000 za walimu! Eti waliajiriwa wiki mbili zilizopita!! Wizi mtupu!! 😞
 
Back
Top Bottom