Kati ya wafanyabishara na wafanyakazi nani mlipakodi mkubwa tena ambaye siyo msumbufu?

Unalipwa milioni 4 Paye ni zaidi ya milioni 1 na hampigi makelele.unadhani serikali ikibadilisha utaratibu na kila mfanyakazi apeleke PAYE yake mwenyewe TRA hakutakuwa na kelele plus defaulters wa kutosha?.kimsingi wafanyakazi wanalipa kodi sana kwasababu hayo makato hawayaoni inakuja net pay tu.
 
Ila awamu ya tano ilichezea sana kodi zetu katika project ya kuua upinzani. Wakina Chakubanga na Kipua ndiyo walitajirikia hapo katika manunuzi ya wapinzani uchwara na kurudia chaguzi,kwa kweli matumizi haya ya kodi zetu yalikuwa sawa na uhaini kabisa.
 
Mfanya kazi ndio analipa kodi zaidi maana yeye anakutana nayo directly na indirect
 
H
Hahahahaaa.umenichekesha.so wafanyabiashara nao wakatwe kodi??
wafanyabiashara wanajikata na kwenda kulipa kwa uzalendo kabisa. Walioajiriwa hawana moyo huo wa kujikata na kwenda kulipa maana wengine wanakwapua hata asprin kabla hazijafika kwa mgonjwa sembuse hela-wewe chezea hela wewe.
 
Unalipa au unakatwa ni lugha tu, athari ya faida au hasara ni ileile kama hatutendei haki malipo au makato husika.
Siyo lugha mkuu kukatwa na kulipa siyo maneno na dhana zinazofanana hata kidogo.
 
Mkuu kwa taarifa yako hata wafanyabiashara nao kama watu waliojiajiri wanalipa PAYE sasa sioni kwa nini mnajimwambafy kuwa manlipa PAYE
 
Siyo lugha mkuu kukatwa na kulipa siyo maneno na dhana zinazofanana hata kidogo.
Sina uhakika na unachojaribu kukieleza labda utoe ufafanuzi.

Wazo langu ilikuwa:
1: Uende kulipa binafsi kwa mjibu wa sheria
2: Mtu au taasisi ipewe jukumu la kuchukua hela toka kwenye kipato chako na kupeleka kwa mujibu wa sheria

Suala ni malipo yamefanyika.
 
Mkuu kwa taarifa yako hata wafanyabiashara nao kama watu waliojiajiri wanalipa PAYE sasa sioni kwa nini mnajimwambafy kuwa manlipa PAYE

Mwajiri atalipa PAYE kama tu ni sehemu ya waajiliwa kwenye uwekezaji wake. Hii ni kwa mujibu wa chimbuko la PAYE.

Ingawa kama mwajiri pia, ana kodi zake nyingi, leseni/vibali na zinazomwandama.
 
Mkuu tukifata wazo lako swali la mleta mada halina maana maana kila mtu analipa kodi kwa mjibu wa sheria; isipokuwa mfanyabiashara anajikata kodi na anaenda kulipa mwenyewe ikwemo kodi ya PAYE. Mwajiriwa anakatwa ila hakuna uhakika kama hicho anachokatwa kinaenda kulipwa- hiyo ndiyo tofauti na ndilo wazo langu ninalotaka ulisikie.
 
Mwajiri atalipa PAYE kama tu ni sehemu ya waajiliwa kwenye uwekezaji wake. Hii ni kwa mujibu wa chimbuko la PAYE.

Ingawa kama mwajiri pia, ana kodi zake nyingi, leseni/vibali na zinazomwandama.
Mkuu kila mfanyabiashara ni mwajiriwa wa hiyo biashara- ukijitoa TRA wanakuingiza kwa mjibu wa sheria-
 

Nadhani suala la msingi lilikuwa:

A:Kwa utaratibu tuliojiwekea kulipa kodi, je ni nani analipa zaidi?
Jibu tunahitaji analysis ya kisayansi itakayounganisha mfumo wetu wa maisha na mifumo ya kodi zote.

B: Ni utaratibu upi haumpi nafasi mlipaji kukwepa kulipa kodi? Pia tunahitaji analysis kwani kila mtu atajibu kulingana na exposure ndogo aliyonayo.

C: Athari ya kodi kwa mlipaji
Inabaki palepale hata kama kodi husika imefika au haijafika ilikokusudia ilimradi tu ilikatwa haijalishwi ni kwa njia gani.
 
Mkuu kila mfanyabiashara ni mwajiriwa wa hiyo biashara- ukijitoa TRA wanakuingiza kwa mjibu wa sheria-
Kwa msingi huo sawa.

Lakini, sina uhakika kama mmiliki wa hardware anatakiwa kupeleka return ya miezi mitatu na atakuwa na makato ya kulingana na mshahara wake kwenye mradi wake huo huo wa hardware.
 
Mkuu wafanyabiashara wanalipa kodi zaidi kuliko wafanyakazi- Tazama
mwenyekiwanda cha soda kwa mfano
1. anatumia sukari na mwajiriwa naye anatumia ila angalia kiasi mfanyabiashara ananunua tani kadhaa dhidi ya kilo kadhaa za mwajiriwa. mfanyabiashara anatumia sukari pia nyumbani kwake ikiwa ziada ya ile anayotumia kiwandani kutengezea soda
2. mfanyabiashara analipa PAYE kama mwajiriwa anavyolipa
3. mfanyabiashara analipa kodi ya mapato au makampuni hii mwajiriwa halipi.
Kwa ujumla kwenye kodi za ulaji wote tunalipa ISIPOKUWA kuna kodi za moja kwa moja wafanyabiashara wanalipa kodi zaidi kuliko waajiriwa.
 
Kwenye izo tozo za biashara umesahau kuna service levy pia mkuu
 
Mwajiri analipa kodi. Mwajiriwa anakatwa kodi.

Uko sahihi
Kwasababu mfanya biashara kuna mda anafile return of income mwenyewe na commissioner ndioa anafanya adjustment kutokana na uelewa wke wa ulipaji kodi
 

Ni kweli au si kweli ni mpaka ufanye breakdown ya haya yote. Ufanye utafiti wa thamani ya kila kimoja si kwa ujazo tu.

Mfano:
A: Naweza kulipa kodi ya shilingi 5 kwa mshahara wa shilingi 100
B: Ukalipa kodi ya shilingi 50 kwa mtaji wa shilingi 10,000/=

Hawa watu wawili hawalipi sawa.
Ndiyo maana mimi nachelea kumpa yeyote kura yangu. Tunahitaji wachumi kuingia ndani na kufanya analysis na kuja na majibu. Pia hii inaweza kusaidia kuondoa baadhi ya kodi ambazo zinakuwa zinajirudia rudia kwa mifumo tofauti na hatimaye:
A: Kumdumaza mfanyakazi vs mfanyabiashara
B: Kufanya gharama za maisha kupanda
C: Kufanya gharama za uzalishaji kuwa juu
E: Wananchi kwa ujumla kusota
 
Mkuu wafanyabiashara wanalipa kodi zaidi kuliko wafanyakazi- Tazama
mwenyekiwanda cha soda kwa mfano
1. anatumia sukari na mwahiriwa naye anatumia ila angalia kiasi mfanyabiashara ananunua tani kadhaa dhidi ya kilo kadhaa za mwajiriwa. mfanyabiashara anatumia sukari pia nyumbani kwake ikiwa ziada ya ile anayotumia kiwandani kutengezea soda
2. mfanyabiashara analipa PAYE kama mwajiriwa anavyolipa
3. mnyabiashara analipa kodi ya mapato au makampuni hii mwajiriwa halipi.
Kwa ujumla kwenye kodi za ulaji wote tunalipa ISIPOKUWA kuna dodi za mija kwa moja wafanyabiashara wabalipa kodi zaidi kuliko waajiriwa.
Mkuu nisikilize hata kama hukubaliani na mimi na sema hivyo kwa sababu ya uzeefu na uzoefu.
Kuhusu mfumo wa kodi hapo nakubaliana na wewe kuwa kunahitajika marekebisho kuondoa utitiri na kiwango
 
Nilikuwa najiuliza kwa nini kwenye PAYE hatoa kwanza matumizi.maana mtu anamatumizi yake yanayomletea ule mshahara.Mfano nauli ya kwenda na kurudi kazini na chakula cha mchana n.k

Lakini wao wanatoa 10% Social security inayobaki wanajichukulia kama yao hivi.huu nao ni unyang'anyi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…