Hio ni kawaida sana tena wakati mwingine kwa biashara zakawaida tu,
Chukua mfano wa mtu anaedeal na nafaka mfano ufuta,gunia moja la ufuta ushuru unatozwa mpaka 4000 kutegemeana na eneo husika.Utaona kwamba semi moja ya gunia 300 ushuru ni 1,200,000/= huyu anahitaji trip 8 tu kwa mwaka kulipa kiwango tajwa ie 10m.
Semi moja ya mahindi ushuru 300,000/= huyu anahitaji trip 34 kwa mwaka kulipa kiwango tajwa,
Na ifahamike hakuna ubabaishaji kwenye ulipaji wa ushuru kwani kuna barrier kila mahali huko barabarani,
Ukipata mtu anaesafirisha mbao kutoka mafinga muulize ushuru analiapaje kwa semi moja ya mbao,
Japo mifano yangu ime base kwenye ushuru lakini bado kinacholipwa kinaingia serikalini,
Kimsingi wafanyakazi wasijione walipaji wazuri wa kodi,hawana lolote kwa wafanya biashara.