Kati ya wafanyabishara na wafanyakazi nani mlipakodi mkubwa tena ambaye siyo msumbufu?

Kati ya wafanyabishara na wafanyakazi nani mlipakodi mkubwa tena ambaye siyo msumbufu?

Nimemsikiliza sana Mh Rais Samia akisema kuwa TRA watanue wigo wa walipa kodi na wasitumie nguvu Kudai kodi. Hili ni jema sana.
Lakini Huwa najiuliza kuwa kati ya wafanyabiashara na mfanyakazi aliyejiriwa nani mlipa kodi mkubwa tena ambaye siyo msumbufu au mlalamikaji na mpiga makelele sana?

Kuna kinachoitwa PAYE(pay as you earn) kwa mwajiriwa. Hii inakatwa automatically na mwajiri na kutakuwa kuiwasilisha TRA. Hii PAYE ni kodi au ni kitu gani? Maana kama ni kodi basi wajiriwa wanalipa zaidi ya kodi.

Kuna kinachoitwa VAT( value added Tax) ambayo ni 18 % kwa kila unachonunua sokoni. Hii ndiyo kodi ambayo wafanyabiasha kama vile waajiri wanavyokusanya PAYE na kutakiwa kuiwasiliasha TRA ,wanatakiwa kuikusanya kwa walaji na kuiwasilisha kwa TRA.sasa ugomvi wa wafanyabiashara uko hapa. Hawataki kukusanya Hii VAT na kuiwasilisha TRA kama waajiri wanavyofanya.Hapa ndipo TRA inaikosesha serikali mapato.

Nirudi Kwenye point ya kuonyesha kuwa wajiriwa wanalipa Kodi zaidi ya mara 100 kwa mwezi ikiwa ile PAYE nayo ni aina ya kodi.mfanyakazi huyu anakatwa PAYE,then akienda sokoni kununua NGUO.

,chumvi,kiberiti,chupi,sahani,kikombe,karamu,kimodoli,shuka,blanketi, nyama, Samaki, dagaa, petrol yani kila anachonunua analipa VAT 18%. qNdiyo maana nasema mfanyakazi analipia zaidi ya kodi kama wafanyabiashara watakuwa waaminifu kukusanya VAT na kuipeleka TRA .

Kwa nini wafanyabiashara wanalalamika wanapokadiriwa kodi ya mapato( PAYE) ? Je formula inayotumika kukadiria hiyo kodi haiko sawa? Au ni makelele tu ? Mbona sisi wafanyakazi hatupigi makelele?For example ,mfanyakazi ambaye analipwa 4.7 million ,PAYE ni zaidi ya milioni moja kila mwezi.

Sehemu Nyengine ambapo serikalikali inakosa mapato na kuendelea kuwaumiza walaji ni Kwenye makampuni binafsi ambayo mishahara yao ni midogo. Yani mfanyakazi anakatwa kidogo( PAYE) lakini sokoni anaendelea kulipa VAT.Hii kampuni yenye kulipa mishahara midogo inajikusanyia mapato mengi kwa sababu kaajiri watu kiduchu na mshahara kiduchu. Hapa ndipo TRA na serikali inatakiwa kutumia akili na maarifa. Serikali inatakiwa ihakikishe makampuni yote yako audited .serikali isaidie upatikanaji wa mifumo ya kuthibiti mapato kwa gharama nafuu.mfano wewe unataka VAT wakati machine za EFD unauza gharama kubwa.kwa nini TRA isigawe bure hizo EFD machine kama nyenzo ya ukusanyaji mapato na kuwabana wafanyabiashara?

TRA itumia akili na maarifa kukusanya kodi

Nawatakia Pasaka njema
Kwa mwaka nalipa zaidi ya 10,000,000/= wewe mfanyakazi unaedai unalipa kodi kubwa unalipa kiasi gani?
 
Mkuu wafanyabiashara wanalipa kodi zaidi kuliko wafanyakazi- Tazama
mwenyekiwanda cha soda kwa mfano
1. anatumia sukari na mwahiriwa naye anatumia ila angalia kiasi mfanyabiashara ananunua tani kadhaa dhidi ya kilo kadhaa za mwajiriwa. mfanyabiashara anatumia sukari pia nyumbani kwake ikiwa ziada ya ile anayotumia kiwandani kutengezea soda
2. mfanyabiashara analipa PAYE kama mwajiriwa anavyolipa
3. mnyabiashara analipa kodi ya mapato au makampuni hii mwajiriwa halipi.
Kwa ujumla kwenye kodi za ulaji wote tunalipa ISIPOKUWA kuna dodi za mija kwa moja wafanyabiashara wabalipa kodi zaidi kuliko waajiriwa.

Mkuu nisikilize hata kama hukubaliani na mimi na sema hivyo kwa sababu ya uzeefu na uzoefu.
Kuhusu mfumo wa kodi hapo nakubaliana na wewe kuwa kunahitajika marekebisho kuondoa utitiri na kiwango
Ni kweli mkuu, ila bila data mezani inabaki kuwa speculation.
Ila, tunahitaji wazalendo wa kweli kufanyia kazi haya na kufanya mlinganyo na pia kusimamia vyema kinachovunwa.
 
Mimi naona na Serikali yenyewe nayoioneshe uaminifu katika matumizi ya kodi zetu. Haiwezekani watu wanalipa kodi, halafu wanawashuhudia wenye dhamana (Serikali) wakizitumia kodi hizo kulipana wenyewe kwa wenyewe mishahara na posho nono, mfano Wabunge!

Kununulia wapinzani na baadae kurudia uchaguzi kwa kigezo cha kuunga mkono juhudi, kuendesha uchaguzi mkuu kwa hela zetu huku wakiwa na matokeo yao mfukoni, kununua magari lukuki ya kifahari ya kutembelea kama Ma V8, nk.
Alafu polepole anajitokeza anakuuliza unijua vieite wewe? [emoji1787][emoji1787]
 
Mfanyakazi ni punda bin donkey wa Serikali, punda afe mzigo ufike. Bila rushwa na wizi, mfanyakazi kamwe hawezi kutoboa kwa kutegemea mshahara
Huu ni ukweli mchungu
 
Kwa mwaka nalipa zaidi ya 10,000,000/= wewe mfanyakazi unaedai unalipa kodi kubwa unalipa kiasi gani?

Hapa ndio shida huanzia, unalipa hiyo kwa basic investments kiasi gani?

Soma bandiko namba 38.
 
Kwa mwaka nalipa zaidi ya 10,000,000/= wewe mfanyakazi unaedai unalipa kodi kubwa unalipa kiasi gani?
Unamiliki ni Bwashee mpaka ulipe kodi zaidi ya milioni 10 kwa mwaka? Wenzako wanalipa kodi ya laki ngapi tu kwa mwaka, na hata milioni 1 tu hawafiki! Halafu wewe unalipa zaidi ya milioni 10!

Labda kama unamiliki kampuni kubwa, au vituo vya mafuta!
 
Umuhimu wa wafanyabiashara ni kuwa wanaongeza waajiriwa maana wanaajiri. Wakiwalipa mishahara ndio hao wanalipa kodi za aina zote. Baada ya hapo na wao wanalipa kodi.
 
Milioni kumi huyo bado ni mfanyabiashara wa kati si mkubwa. Yaani ni 3.3m per qtr. Inamaana anatengeneza faida M33 au 34 kwa mwaka. Ni wa kawaida.
 
Ni kweli mkuu, ila bila data mezani inabaki kuwa speculation.
Ila, tunahitaji wazalendo wa kweli kufanyia kazi haya na kufanya mlinganyo na pia kusimamia vyema kinachovunwa.
kodi ikusanywe kwa weledi na itumike kwa tija
 
Umuhimu wa wafanyabiashara ni kuwa wanaongeza waajiriwa maana wanaajiri. Wakiwalipa mishahara ndio hao wanalipa kodi za aina zote. Baada ya hapo na wao wanalipa kodi.
MKUU uko sahihi kwa kifupi ni hivi:-
1. bila kodi hakuna serikali;
2. bila biashara hakuna kodi- kuna tozo tu; kwa hiyo
3. biashara ndiyo serikali- TANBIHI- nimesema biashara sijasema wafanyabiashara
 
Nimemsikiliza sana Mh Rais Samia akisema kuwa TRA watanue wigo wa walipa kodi na wasitumie nguvu Kudai kodi. Hili ni jema sana.
Lakini Huwa najiuliza kuwa kati ya wafanyabiashara na mfanyakazi aliyejiriwa nani mlipa kodi mkubwa tena ambaye siyo msumbufu au mlalamikaji na mpiga makelele sana?

Kuna kinachoitwa PAYE(pay as you earn) kwa mwajiriwa. Hii inakatwa automatically na mwajiri na kutakuwa kuiwasilisha TRA. Hii PAYE ni kodi au ni kitu gani? Maana kama ni kodi basi wajiriwa wanalipa zaidi ya kodi.

Kuna kinachoitwa VAT( value added Tax) ambayo ni 18 % kwa kila unachonunua sokoni. Hii ndiyo kodi ambayo wafanyabiasha kama vile waajiri wanavyokusanya PAYE na kutakiwa kuiwasiliasha TRA ,wanatakiwa kuikusanya kwa walaji na kuiwasilisha kwa TRA.sasa ugomvi wa wafanyabiashara uko hapa. Hawataki kukusanya Hii VAT na kuiwasilisha TRA kama waajiri wanavyofanya.Hapa ndipo TRA inaikosesha serikali mapato.

Nirudi Kwenye point ya kuonyesha kuwa wajiriwa wanalipa Kodi zaidi ya mara 100 kwa mwezi ikiwa ile PAYE nayo ni aina ya kodi.mfanyakazi huyu anakatwa PAYE,then akienda sokoni kununua NGUO.

,chumvi,kiberiti,chupi,sahani,kikombe,karamu,kimodoli,shuka,blanketi, nyama, Samaki, dagaa, petrol yani kila anachonunua analipa VAT 18%. qNdiyo maana nasema mfanyakazi analipia zaidi ya kodi kama wafanyabiashara watakuwa waaminifu kukusanya VAT na kuipeleka TRA .

Kwa nini wafanyabiashara wanalalamika wanapokadiriwa kodi ya mapato( PAYE) ? Je formula inayotumika kukadiria hiyo kodi haiko sawa? Au ni makelele tu ? Mbona sisi wafanyakazi hatupigi makelele?For example ,mfanyakazi ambaye analipwa 4.7 million ,PAYE ni zaidi ya milioni moja kila mwezi.

Sehemu Nyengine ambapo serikalikali inakosa mapato na kuendelea kuwaumiza walaji ni Kwenye makampuni binafsi ambayo mishahara yao ni midogo. Yani mfanyakazi anakatwa kidogo( PAYE) lakini sokoni anaendelea kulipa VAT.Hii kampuni yenye kulipa mishahara midogo inajikusanyia mapato mengi kwa sababu kaajiri watu kiduchu na mshahara kiduchu. Hapa ndipo TRA na serikali inatakiwa kutumia akili na maarifa. Serikali inatakiwa ihakikishe makampuni yote yako audited .serikali isaidie upatikanaji wa mifumo ya kuthibiti mapato kwa gharama nafuu.mfano wewe unataka VAT wakati machine za EFD unauza gharama kubwa.kwa nini TRA isigawe bure hizo EFD machine kama nyenzo ya ukusanyaji mapato na kuwabana wafanyabiashara?

TRA itumia akili na maarifa kukusanya kodi

Nawatakia Pasaka njema
Siku ukianza kufanya biashara au kuanzisha kampuni inayojihusisha na biashara utaelewa. Kwa sasa elewa hivyohivyo.
 
Mimi naona na Serikali yenyewe nayoioneshe uaminifu katika matumizi ya kodi zetu. Haiwezekani watu wanalipa kodi, halafu wanawashuhudia wenye dhamana (Serikali) wakizitumia kodi hizo kulipana wenyewe kwa wenyewe mishahara na posho nono, mfano Wabunge!
Natamani hii iwafikie walengwa!!

Tunataka Kodi tunazolipa, zisiwe za kulipana maposho na kuongezeana mishahara makundi makundi na wengine wakiendelea kubaki na vimishahara vya ajabu ajabu

Kama tumeamua kubana Matumizi, miposho ya wabunge ipuruniwe na mishahara Yao pia ipunguzwe, pensheni zao pia ziko juu Sana ukilinganisha na watumishi wengine wanaokaa miaka mingi kwenye utumishi,
 
Kuna vitu vinafikirisha:
1: Mfanyakazi
A: Unalipwa mshahara, unakatwa mpaka 30% ya mshahara.
B: Unaenda kununua chochote, unakutana na 18% VAT
C: Ukitaka kufanya biashara yoyote, unalipa sawa na mfanyabiasha mwingine yeyote???
D: Makusanyo mengine mbalimbali
E: Mfanyabiashara halisi/kodi
F: Mikopo halisi vs nafuu.
G: Misaada/ si chanzo cha mapato cha msingi

2: Mfanyabiashara pure
Sina uhakika wa kodi zote zinazoweza kumwandama mmojamoja.

Ila, ili kuthibitisha hiyo ni mpaka wahusika wafanye analysis. Hili ni swali la kutafiti. Ingawa nadhani wao ndo wana mwanya wa kukwepa kidogo kuliko wafanyakazi.

Unaipa serikali hiyo 48% +C+D+E ili ifanye pamoja na mambo mengine ni shughuli za maendeleo. Inaenda kuishi kifahari? na inasusua kutekeleza mambo??

1: Unaenda hospitali, dawa hakuna za kutosheleza au uwepo wa zile za kununua.

2: Unaenda shule, madawati hakuna, walimu hakuna wa kutosha, vitendeakazi hakuna/ havitoshelezi.

3: Miundimbinu??

Hakuna kisingizio cha serikali ina mambo mengi, hiki ni kichaka tu.

Tutumie pesa kulingana na uwezo wetu, tuwekeze kwenye miradi kulingana na uwezo wetu/hatuwezi kubadili mambo overnight.

Tusiwakamue wananchi zaidi ya uwezo wao na tuwe waaminifu kwa kile kile kidogo tukipatacho, tutasonga mbele.

Hatuwezi kusimamisha maisha ya mtu/watu, kwa sababu tunajenga mradi huu, tubalansi issues/priority matters.

Nafikiri kuna haja ya kutafakari mipango yetu ya matumizi binafsi vs maendeleo.
Ili, maendeleo yetu yaendane na kiasi cha pesa tunachokusanya na yule mchangiaji aone anachokichangia kinaleta impact na hapo UZALENDO hautahitaji mapambio.

Pia, nichukue fursa hii kuishauri serikali. Kuna taasisi au kitengo nadhani ni think tank/ kitu kama hicho. Ni vyema kuanzisha utaratibu wa kupokea maoni mbalimbali toka kwa watu wengine nje ya serikali na ndani ya serikali.

Kwa sababu, si kwa walioajiriwa tu ndo huwa na mawazo bora BALI kuwe na fursa ya watu kuchangia mawazo kwa utaratibu kwa kufuata nyanja mbalimbali walizobibea kama: afya, uchumi, siasa nk. Hii inaweza kufanyika kwa kuwa na online system au njia nyingine na umma uwe na taarifa juu ya hilo.

Wakishapokea, wafanyie kazi ya kuchanganua na kuboresha na kuyafanyia kazi kwa maendeleo ya taifa na watu kwa ujumla bila ku-victimize mtu yeyote.

"HAPO TUTAKUWA NA SERIKALI YA WATU NA HASA WANYONGE"
Mnaachwa mueneze uongo wenu kwasababu ya kisomo chenu huwezi linganisha mfanya biashara na mfanyakazi,mimi ni mfanya biashara najilipa 3m baadaya waikato yote unayo sema nimeajiri watu 16 ambao nawalipa kodi kupitiashahara ninao lips mtu wahuni anachukua 560000 baada ya mapato,kampuni inajilipia corporate tax fee zingine,bila mini mfanyabiashara kusimamia kidete maono yangu huyo mfanyakazi atalipa mini,when things went wrong somewhere unajua tabu inayo nikuta wakati nyingine kiafya,unajua mfanyakazi hashiriki chochote when things went wrong yeye atasubiri jioni akagonge combo,msidharau entrepreneurs ni engine ya uchumi
 
Sina uhakika kama umesoma ukiwa na mawazo huru au na msongo wa mawazo.

Suala hapa si kueneza uongo bali kutafakari na kama wewe una data za kweli na uhakika ni suala la kuweka wazi tu. Jieleze ueleweke.

Nimekuwa huru katika maoni yangu na nimesema wazi, sina data za mfanyabiashara na ni mchakato wa kisayansi kuyajua haya. Pia, usichukue tu kuwa nalipa 1000,0000,000/= Tsh, its under which base.

Mfano:
A: Tuna mtumishi X, analipwa Tsh 2,000,000/= kwa mwezi. Anakatwa Tsh. 500,000/= kila mwezi. Kwa mwaka anakatwa 6,000,000/=
B: Kuna mfanyabiashara ya hardware, amewekeza 20,000,000/=. Anafanya return ya makadirio ya 500,000/= kila robo mwaka. Jumla 2,000,000/=
Sasa, tungekuja na vikodi vyote vingine wanavyokutana navyo, ili kuwalinganisha hawa watu. Hapo ndo utakuwa umewatendea haki. Kwa kuwa mimi si mtaalamu wa mambo ya kodi ndio maana nikachelea kusema nani hulioa zaidi. Ila tunahitaji analysis ya kisayansi.

Unapowalipa wafanyakazi uliowaajiri ni baada ya kuzalisha mali kwenye kampuni yako na si fadhila. Na uwepo wa mfanyakazi yeyote utategemea justfied human resource demand. Na wafanyakazi wanajilipa kwa kazi wanayoifanya.

Wewe msingi wako ni direct impact ya kodi kama kampuni inahitajika kufanya nini ili kampuni yako iwepo katika mifumo ya kodi?
Sioni haja ya kupaniki.

Kumbuka kutafakari pia hata popote, aliyetoa sh2 katika mshahara wa Tsh10 yake, si sawa na Tsh100 katika mtaji wa Tsh 1000.
 
Unamiliki ni Bwashee mpaka ulipe kodi zaidi ya milioni 10 kwa mwaka? Wenzako wanalipa kodi ya laki ngapi tu kwa mwaka, na hata milioni 1 tu hawafiki! Halafu wewe unalipa zaidi ya milioni 10!

Labda kama unamiliki kampuni kubwa, au vituo vya mafuta!
Hio ni kawaida sana tena wakati mwingine kwa biashara zakawaida tu,
Chukua mfano wa mtu anaedeal na nafaka mfano ufuta,gunia moja la ufuta ushuru unatozwa mpaka 4000 kutegemeana na eneo husika.Utaona kwamba semi moja ya gunia 300 ushuru ni 1,200,000/= huyu anahitaji trip 8 tu kwa mwaka kulipa kiwango tajwa ie 10m.
Semi moja ya mahindi ushuru 300,000/= huyu anahitaji trip 34 kwa mwaka kulipa kiwango tajwa,
Na ifahamike hakuna ubabaishaji kwenye ulipaji wa ushuru kwani kuna barrier kila mahali huko barabarani,
Ukipata mtu anaesafirisha mbao kutoka mafinga muulize ushuru analiapaje kwa semi moja ya mbao,
Japo mifano yangu ime base kwenye ushuru lakini bado kinacholipwa kinaingia serikalini,
Kimsingi wafanyakazi wasijione walipaji wazuri wa kodi,hawana lolote kwa wafanya biashara.
 
Wafanyabiashara wanalipa kodi zaidi japo ni wasumbufu
Wafanyakazi wanalipa kwa uaminifu kutokana na kwamba pesa ya mshahara wao inafanyiwa makato kabla haijafika mkononi
 
Ni kweli mkuu, ila bila data mezani inabaki kuwa speculation.
Ila, tunahitaji wazalendo wa kweli kufanyia kazi haya na kufanya mlinganyo na pia kusimamia vyema kinachovunwa.
Hivi nyie watu kwanini hamuelewi? Yaani tumeorodhesha kodi zaidi ya kumi ambazo zinamhusu mfanyabiasha peke yake na bado mnaleta ubishi kulinganisha na PAYE na VAT za mtumishi...!! Hivi bado tu hamjui kwamba hata hizo PAYE na VAT ambazo mnazosema ni za mfanyakazi zinamhusu mfanyabiasha!
 
Back
Top Bottom