Kati ya wafanyabishara na wafanyakazi nani mlipakodi mkubwa tena ambaye siyo msumbufu?

Kwa mwaka nalipa zaidi ya 10,000,000/= wewe mfanyakazi unaedai unalipa kodi kubwa unalipa kiasi gani?
 
Ni kweli mkuu, ila bila data mezani inabaki kuwa speculation.
Ila, tunahitaji wazalendo wa kweli kufanyia kazi haya na kufanya mlinganyo na pia kusimamia vyema kinachovunwa.
 
Alafu polepole anajitokeza anakuuliza unijua vieite wewe? [emoji1787][emoji1787]
 
Mfanyakazi ni punda bin donkey wa Serikali, punda afe mzigo ufike. Bila rushwa na wizi, mfanyakazi kamwe hawezi kutoboa kwa kutegemea mshahara
Huu ni ukweli mchungu
 
Kwa mwaka nalipa zaidi ya 10,000,000/= wewe mfanyakazi unaedai unalipa kodi kubwa unalipa kiasi gani?

Hapa ndio shida huanzia, unalipa hiyo kwa basic investments kiasi gani?

Soma bandiko namba 38.
 
Kwa mwaka nalipa zaidi ya 10,000,000/= wewe mfanyakazi unaedai unalipa kodi kubwa unalipa kiasi gani?
Unamiliki ni Bwashee mpaka ulipe kodi zaidi ya milioni 10 kwa mwaka? Wenzako wanalipa kodi ya laki ngapi tu kwa mwaka, na hata milioni 1 tu hawafiki! Halafu wewe unalipa zaidi ya milioni 10!

Labda kama unamiliki kampuni kubwa, au vituo vya mafuta!
 
Umuhimu wa wafanyabiashara ni kuwa wanaongeza waajiriwa maana wanaajiri. Wakiwalipa mishahara ndio hao wanalipa kodi za aina zote. Baada ya hapo na wao wanalipa kodi.
 
Milioni kumi huyo bado ni mfanyabiashara wa kati si mkubwa. Yaani ni 3.3m per qtr. Inamaana anatengeneza faida M33 au 34 kwa mwaka. Ni wa kawaida.
 
Ni kweli mkuu, ila bila data mezani inabaki kuwa speculation.
Ila, tunahitaji wazalendo wa kweli kufanyia kazi haya na kufanya mlinganyo na pia kusimamia vyema kinachovunwa.
kodi ikusanywe kwa weledi na itumike kwa tija
 
Umuhimu wa wafanyabiashara ni kuwa wanaongeza waajiriwa maana wanaajiri. Wakiwalipa mishahara ndio hao wanalipa kodi za aina zote. Baada ya hapo na wao wanalipa kodi.
MKUU uko sahihi kwa kifupi ni hivi:-
1. bila kodi hakuna serikali;
2. bila biashara hakuna kodi- kuna tozo tu; kwa hiyo
3. biashara ndiyo serikali- TANBIHI- nimesema biashara sijasema wafanyabiashara
 
Siku ukianza kufanya biashara au kuanzisha kampuni inayojihusisha na biashara utaelewa. Kwa sasa elewa hivyohivyo.
 
Natamani hii iwafikie walengwa!!

Tunataka Kodi tunazolipa, zisiwe za kulipana maposho na kuongezeana mishahara makundi makundi na wengine wakiendelea kubaki na vimishahara vya ajabu ajabu

Kama tumeamua kubana Matumizi, miposho ya wabunge ipuruniwe na mishahara Yao pia ipunguzwe, pensheni zao pia ziko juu Sana ukilinganisha na watumishi wengine wanaokaa miaka mingi kwenye utumishi,
 
Mnaachwa mueneze uongo wenu kwasababu ya kisomo chenu huwezi linganisha mfanya biashara na mfanyakazi,mimi ni mfanya biashara najilipa 3m baadaya waikato yote unayo sema nimeajiri watu 16 ambao nawalipa kodi kupitiashahara ninao lips mtu wahuni anachukua 560000 baada ya mapato,kampuni inajilipia corporate tax fee zingine,bila mini mfanyabiashara kusimamia kidete maono yangu huyo mfanyakazi atalipa mini,when things went wrong somewhere unajua tabu inayo nikuta wakati nyingine kiafya,unajua mfanyakazi hashiriki chochote when things went wrong yeye atasubiri jioni akagonge combo,msidharau entrepreneurs ni engine ya uchumi
 
Sina uhakika kama umesoma ukiwa na mawazo huru au na msongo wa mawazo.

Suala hapa si kueneza uongo bali kutafakari na kama wewe una data za kweli na uhakika ni suala la kuweka wazi tu. Jieleze ueleweke.

Nimekuwa huru katika maoni yangu na nimesema wazi, sina data za mfanyabiashara na ni mchakato wa kisayansi kuyajua haya. Pia, usichukue tu kuwa nalipa 1000,0000,000/= Tsh, its under which base.

Mfano:
A: Tuna mtumishi X, analipwa Tsh 2,000,000/= kwa mwezi. Anakatwa Tsh. 500,000/= kila mwezi. Kwa mwaka anakatwa 6,000,000/=
B: Kuna mfanyabiashara ya hardware, amewekeza 20,000,000/=. Anafanya return ya makadirio ya 500,000/= kila robo mwaka. Jumla 2,000,000/=
Sasa, tungekuja na vikodi vyote vingine wanavyokutana navyo, ili kuwalinganisha hawa watu. Hapo ndo utakuwa umewatendea haki. Kwa kuwa mimi si mtaalamu wa mambo ya kodi ndio maana nikachelea kusema nani hulioa zaidi. Ila tunahitaji analysis ya kisayansi.

Unapowalipa wafanyakazi uliowaajiri ni baada ya kuzalisha mali kwenye kampuni yako na si fadhila. Na uwepo wa mfanyakazi yeyote utategemea justfied human resource demand. Na wafanyakazi wanajilipa kwa kazi wanayoifanya.

Wewe msingi wako ni direct impact ya kodi kama kampuni inahitajika kufanya nini ili kampuni yako iwepo katika mifumo ya kodi?
Sioni haja ya kupaniki.

Kumbuka kutafakari pia hata popote, aliyetoa sh2 katika mshahara wa Tsh10 yake, si sawa na Tsh100 katika mtaji wa Tsh 1000.
 
Unamiliki ni Bwashee mpaka ulipe kodi zaidi ya milioni 10 kwa mwaka? Wenzako wanalipa kodi ya laki ngapi tu kwa mwaka, na hata milioni 1 tu hawafiki! Halafu wewe unalipa zaidi ya milioni 10!

Labda kama unamiliki kampuni kubwa, au vituo vya mafuta!
Hio ni kawaida sana tena wakati mwingine kwa biashara zakawaida tu,
Chukua mfano wa mtu anaedeal na nafaka mfano ufuta,gunia moja la ufuta ushuru unatozwa mpaka 4000 kutegemeana na eneo husika.Utaona kwamba semi moja ya gunia 300 ushuru ni 1,200,000/= huyu anahitaji trip 8 tu kwa mwaka kulipa kiwango tajwa ie 10m.
Semi moja ya mahindi ushuru 300,000/= huyu anahitaji trip 34 kwa mwaka kulipa kiwango tajwa,
Na ifahamike hakuna ubabaishaji kwenye ulipaji wa ushuru kwani kuna barrier kila mahali huko barabarani,
Ukipata mtu anaesafirisha mbao kutoka mafinga muulize ushuru analiapaje kwa semi moja ya mbao,
Japo mifano yangu ime base kwenye ushuru lakini bado kinacholipwa kinaingia serikalini,
Kimsingi wafanyakazi wasijione walipaji wazuri wa kodi,hawana lolote kwa wafanya biashara.
 
Wafanyabiashara wanalipa kodi zaidi japo ni wasumbufu
Wafanyakazi wanalipa kwa uaminifu kutokana na kwamba pesa ya mshahara wao inafanyiwa makato kabla haijafika mkononi
 
Ni kweli mkuu, ila bila data mezani inabaki kuwa speculation.
Ila, tunahitaji wazalendo wa kweli kufanyia kazi haya na kufanya mlinganyo na pia kusimamia vyema kinachovunwa.
Hivi nyie watu kwanini hamuelewi? Yaani tumeorodhesha kodi zaidi ya kumi ambazo zinamhusu mfanyabiasha peke yake na bado mnaleta ubishi kulinganisha na PAYE na VAT za mtumishi...!! Hivi bado tu hamjui kwamba hata hizo PAYE na VAT ambazo mnazosema ni za mfanyakazi zinamhusu mfanyabiasha!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…