Kati ya wafanyabishara na wafanyakazi nani mlipakodi mkubwa tena ambaye siyo msumbufu?

Sasa si utupatie taxation profile ya kiwango fulani cha investment na mshahara wa mtu equivalent, badala ya kunung'unika kuwa hatuelewi/sielewi.
 
Tujaribu kujenga hoja si kulalama tu.
Katika maelezo yangu nimesema hatuna data na hatuwezi ku-conclude. Unaweza kuwa na kodi hata 100, lakini ni nini thamani ya kiasi cha kodi kwenye investment uliyoweka?

Mfanyakazi kodi inakwenda mpaka 30% ya mshahara wake. Kuna concept kuwa kila mfanyabiashara analipa PAYE? Sina uhakika juu ya hiyo. Na kama ni hivyo sawa kwani mfanyakazi akitaka kufanya biashara pia anakutana na msururu wote wa kodi.

Nilitegemea uje na taxation profile ya mfanyakazi na equivalent investment ya mfanyabiashara. Toka hapo ufanye direct and indirect taxation. Kumbuka VAT ni ya mlaji na si mfanyabiashara.

Kama hatuwezi kufanya hivyo, tunajibu kwa feeling bila data. Hapa ndipo elimu ya mlipa kodi tunapoihitaji wote.
 
Kuna tofauti kati ya kodi na ushuru bila shaka! Mimi niliulizia kwenye suala la kodi. Ni biashara gani hiyo anayo fanya na kulipa kodi ya milioni 10 kwa mwaka!

Kuhusu ushuru, sina tatizo kabisa juu ya hizo gharama.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…