Tafuta clip ya Moses Kurola kuna kitu utakipata
Sasa hapo ametabiri nn,hivi mnasoma biblia kweli, urus ya kisoviet ilishakuwa taifa kubwa ikasambaratishwa
biblia inatabiri super power ni USA
unabii kuhus urusi kwenye bibli soma daniel na ezekiel ,na bado haujatimia
ndicho alichoeleza moses kolola
Neno
Gogu na Magogu limeonekana sehemu mbili katika biblia, Sehemu ya kwanza ni katika kitabu cha
Ezekieli 38:2, na katika
Ufunuo 20:8.
Tunalisoma hilo vizuri katika Ezekieli..
Ezekieli 38:1 “Neno la Bwana likanijia, kusema,
2 Mwanadamu, kaza uso wako, umwelekee GOGU, wa NCHI YA MAGOGU, mkuu wa Roshi, Mesheki, na Tubali, ukatabiri juu yake”,
Na nchi hiyo lilikuwa upande wa kaskazini mwa Asia na Ulaya, ambayo sasahivi ni Maeneo ya nchi ya Urusi. Hatima ya hilo Taifa la Magogu, biblia haijaieleza, lakini ni wazi kuwa lilikuja kupotea kama yalivyopotea mataifa mengine yaliyokuwa hodari kama Babeli.
Sasa baada ya kujua hilo, twende kipengele cha pili, cha GOGU. Kama tulivyotangulia kusema Magogu sio wingi wa Gogu. Bali Gogu ni kiongozi wa Taifa la Magogu. Yaani mfalme wa taifa la Magogu. Kwahiyo tunaposoma, neno Gogu na Magogu, Ni sawa na kusema Farao na Misri, au Sulemani na Israeli.
Ndio maana tunasoma hapo katika
Ezekieli 38:3… “useme, Bwana MUNGU asema hivi; Tazama, mimi ni juu yako, Ewe GOGU, mkuu wa Roshi, na Mesheki, na Tubali;”
Umeona hapo mstari wa 2, unasema Gogu mkuu wa…. Neno
“mkuu wa” linaashiria ni kiongozi, hivyo Gogu ni jina la kiuongozi kama vile Farao, au Sultani. Na Magogu ni Taifa hilo lenye nguvu ambalo linatawala mataifa mengine madogo madogo
(Tubali, Mesheki na Roshi)
Sasa kama tulivyotangulia kusema huo mji wa Magogu haupo tena wala mkuu wake Gogu hayupo…Lilikuwepo enzi hizo, lakini sasa halipo tena, lakini huo unabii wa
Ezekieli 38 bado haujatimia.. Ambapo ukisoma hiyo
Ezekieli 38 yote, utaona inazungumzia Habari za vita vitakavyopiganwa Israeli, ambapo Mataifa mengi katika nchi ya mashariki ya kati
(kwasasa ni mataifa ya kiarabu), yataungana pamoja na Gogu na Magogu, atakayekuwepo kipindi hicho kuja kuivamia Israeli, lakini biblia inasema Gogu atashindwa vibaya sana Pamoja na mataifa hayo aliyoshirikiana naye.
Sasa huyo Gogu na Magogu, atakuwa ni nani, kama mji huo ulishapotea kitambo?..
Gogu atakayeasisi vita hivyo vya
Ezekieli 38, Uthibitisho wote unaonyesha kuwa atakuwa si mwingine Zaidi ya Mkuu wa Taifa la URUSI .