Kati ya Waziri January Makamba na Rais Samia, nani alimteua Maharage kuwa Mkurugenzi Tanesco?

kipumbwi

JF-Expert Member
Joined
Feb 3, 2015
Posts
3,162
Reaction score
9,073

Your browser is not able to display this video.


Salam wakuu.

Naomba kwanza kupandisha clip ya January Makamba akiwa Waziri wa Nishati na pia kuweka barua ya Ikulu ya teuzi.

Baada ya kumsikiliza January Makamba na kurejea barua ya Ikulu, je ni nani haswa alihusika na anahusika na hizi teuzi zinazotangazwa kutoka Ikulu?

Kwa sasa tumeona Maharage Chande kapelekwa TTCL, je huko amefanyiwa usaili na?

Alichoongea January, ni kudhihirisha kuwa mengi ya Tanesco Rais Samia hahusiki na wapo wanaohusika ama ndio kuwa huko kwenye teuzi mambo ni zigzag kila mtu na don wake na barua zinazotoka ni ceremonial tu za kiitifaki?

Updates:

Tarehe 25 September (siku 2 baada ya kuteuliwa) Maharage Chande amehamishiwa posta na kua PostaMasta.


NB- kuruka ruka kwa Maharage ndio kuiva kwake,Maharage yanaruka ruka mpaka yaive,mpishi wa maharagwe ndio anajua umuhimu wake baadala ya samaki ama nyama!!!
 
Duh!.
P
 
Katika teuzi anazofanya Rais Rais hupelekewa majina matatu na yeye Rais huteua baada ya kupata ushauri kwa watu wake akiwemo waziri muhusika!
 
Alichoongea January, ni kudhihirisha kuwa mengi ya Tanesco Rais Samia hahusiki na wapo wanaohusika ama ndio kuwa huko kwenye teuzi mambo ni zigzag kila mtu na don wake na barua zinazotoka ni ceremonial tu za kiitifaki?![emoji419][emoji375]

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Changamoto za Tanesco hazijaanza leo na hazitaisha kesho kama bunge/raisi hatotenganisha production na transmission/distribution. Tanesco ibaki kwenye transmission na distribution tu. Production ya umeme ifanywe na serikali kupitia separate company, pia sector binafsi iendelee zalisha umeme kama sasa ila iwekewe sheria wezeshi.

Yakifanyika hayo basi hata hizi lawama tunazowapa wakurugenzi zitapungua.
 
Maharage Chande ni great failure
 

Rais anapewa mapendekezo na Waziri ila siyo lazima ayafuate. Lakini kwa hili la Maharage, Makamba ndiye aliyemtafuta na kumpigia debe kwa Samia.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…