FJM, suala la utii wa sheria halina mjadala, nakuhakikishia baada ya muswada ule kutiwa saini na kuwa sheria, no one can do anything!. Hata hao Chadema wala wanaharakati hawawezi kufanya lolote, nothing, nil!, ndio maana nilishauri tuvunje kambi, tuipe tume ushirikiano!.
Sheria za nchi sio msaafu, zinabadilishwa, na Tanzania tunayo mifano iliyo wazi. Mmoja ni sheria ya gharama za uchaguzi (correct me if I am wrong), kuna mambo yaliingizwa kinyemela tofauti na bunge lilivyopitisha, na mtu wa kwanza kupiga kelele alikuwa Dr Slaa. Mwanzoni wakubwa wakakataa lakini baadaye walikubali na marekebesho yalifanyika.
Hoja ya utii wa sheria kwa Tanzania ni sawa na maji na mafuta. Sheria za nchi hii zinatumika kwa wezi wa kuku. Sijui unaongelea utii gani hapa? Kama kweli sheria haina mjadala ni kifungu gani kilichotumika kuhalalisha mazungumzo kati ya vyombo vya dola na watuhumiwa wa EPA? Nijuavyo mimi anyone is presumed innocent until priven otherwise in the court of law. Hivyo kama kuna mtuhumiwa yoyote awe wa EPA etc etc ni mahakama ndiyo yenye mamalka ya kusema guilty or not guilty.
Nisingetaka kuchangia tena kwenye huu mjadala maana sidhani kama cha kujadili tena hapa. Ila naomba kusema hivi
(na sio kama naku-attack wewe Pasco kama Pasco, ila nataka nitoe maoni juu ya hoja zako Pasco), kwamba mtu akizisoma hoja zako na kama sio strong atayumba vibaya sana. Hoja zako zinakatisha tamaa mno, na inawezekana wewe ni mtu wa ku-give easily. Sitoshangaa kama umekuwa unaancha kazi sehemu mbalimbali kwa sababu tu kuna mitego. Inawezekana hujatambua hili. Huwezi kukimbia kwa sababu sheria inasema hivi au vile, sheria zinatungwa na malaika? Ni kweli sheria hazibadilishwi? watu 300 hata 400 ni kitu gani mbele ya watu millioni 40?.
In life you have to stand up for things you believe in! Nelson Mandela amekaa jela kwa miaka 27, watoto wake wamekuwa bila malezi ya baba yao. Angekuwa ni mtu wa kukata tamaa angekubali yaishe, na leo tungukuwa tunaongea vitu vingine.
If you have nothing to fight for you have nothing to life for. Ukweli siku zote utasimama, watawala na watu wengine wowote wanaweza kutumia nguvu walizonazo leo kufanya kinyume na matarajio ya wanaowatawala, lakini wakae wakijua mbinu zote hizo ni short-term lived. Zitadumu kwa wakati fulani tu lakini sio kwa siku zote. Iko siku sio leo na pengine sio kesho lakini iko siku mizani itaegemea upande wa ukweli.
Na ili mizani iegemee upande wa ukweli ni vizuri wale wanaojua ukweli wakaupigania kwa kuaanza kuujaza upande huo bila kukata tamaa ili kuifanya mizani kurudi upande wa ukweli. Kwa mtazamamo wangu CHADEMA wameanza kujaza mizani ya ukweli, ni safari ndefu, yenye matatizo mengi, lakini safari yenye manufaa kwa watanzania wengi kama sio wote. Kama CHADEMA hawataanza kazi ya kujaza mizani ya kweli nani afanye? Na kama CHADEMA hawataanza hiyo kazi sasa waanze lini? Na kama CHADEMA wanajaza mizani kwa njia ya mijadala bungeni bila mafanikio wafanye nini?
Nimalizie, kwa mara ya kwanza katika historia ya nchi yetu watanzania tuna choice. Mzani uko mbele yetu, upande mmoja ni CCM na washirika wake na upande wa pili ni CHADEMA na washirika wake. Mtanzania yoyote sasa anaweza kuchagua ama CCM au CHADEMA.
If you have nothing to fight for you have nothing to life for.