Katiba: CHADEMA mlikosea! Kubalini yaishe, Tusonge mbele!

Kipi hapo ambacho hukukisema au hakihusiani au hukuweza kukisema kwenye thread ile ile ya Pasco?
 
Thread ile ya pasco haihusiani na kikao cha CDM na rais.
Sana sana ni kuhusu kifungu cha 86 na Tundu Lissu.
Shida ikwapi?
 
jmushi huwezi kufananisha nguvu alikuwa nayo Rais unakafananisha na Bunge, Rais wa Tz ni mtu ana nguvu nyingi mno kwahiyo na ni rais sana kumshawishi mtu mmoja kuliko kundi la watu ambalo unajua wazi kuwa linaendeshwa kwa kutumia ideology badala ya principal. Rais ni mtu aliyezungukwa na wataalam mbalimbali ambao wana mshauri ambao naamini kati yao watatokea watakayoyaona mawazo ya chadema ni kitu muhimu cha kuzingatiwa kwani hapa cha msingi sana ni political legitimacy ya katiba na siyo legal legitimacy tu pekee yake kama walivyofanya wabunge wa CCM. kwahiyo naamini rais ataingalia hio componet with closer eye kuliko wanywa maji ya bendera kule bungeni kwani huwezi kuwa na hiyo component kama chama kikuuu cha upinzani nchini hakikubaliani na utaratibu mzima wa kuandaa katiba. na kama hakikataa basi CDM wanakuwa wameshajenga hoja ya kutosha kwa wananchi kwamba wamekwenda mpaka mwisho wa lami na hakuna anayejali. Spika Makinda anatumiwa na Rais sasa kuna haja gani ya kuangaika kupoteza muda wako na middle man wakati mhusika mkuu yupo kwahiyo CDM wamefanya vizuri ku bipass the middle man na kwenda moja kwa moja kwa muhusika mkuu ukitoka hapo hakuna kwa kwenda bali kuingia barabarani.
 
jmushi huwezi kufananisha nguvu alikuwa nayo Rais unakafananisha na Bunge, Rais wa Tz ni mtu ana nguvu nyingi mno kwahiyo na ni rais sana kumshawishi mtu mmoja kuliko kundi la watu ambalo unajua wazi kuwa linaendeshwa kwa kutumia ideology badala ya principal. Rais ni mtu aliyezungukwa na wataalam mbalimbali ambao wana mshauri ambao naamini kati yao watatokea watakayoyaona mawazo ya chadema ni kitu muhimu cha kuzingatiwa kwani hapa cha msingi sana ni political legitimacy ya katiba na siyo legal legitimacy tu pekee yake kama walivyofanya wabunge wa CCM. kwahiyo naamini rais ataingalia hio componet with closer eye kuliko wanywa maji ya bendera kule bungeni kwani huwezi kuwa na hiyo component kama chama kikuuu cha upinzani nchini hakikubaliani na utaratibu mzima wa kuandaa katiba. na kama hakikataa basi CDM wanakuwa wameshajenga hoja ya kutosha kwa wananchi kwamba wamekwenda mpaka mwisho wa lami na hakuna anayejali. Spika Makinda anatumiwa na Rais sasa kuna haja gani ya kuangaika na middle man wakati mhusika mkuu yupo kwahiyo CDM wamefanya vizuri kubias the middle man na kwenda kwa muhusika mkuu.
Mkuu hiyo mi mihimili miwili tofauti,they should have fought both fronts...Unless wana uhakika Rais atakubali licha ya kwamba hawakuwa na uhakika kuwa Spika atakubali.

Ndipo hapo kama it was a mistake,basi waseme tu.

Binadamu hukosea.
 
jumushi kwanini upoteze muda wako na watu wanaoshambilia watu badala ya hoja ukae bungeni uboshane na akina john komba ni kupoteza ni bora hizo nguvu zako uzipange vizuri ukampane na mkuu wa kaya kwa maana anao uwezo wa ku wa defeat hao wote kwa wakati mmoja kwahiyo bado nakubaliana nao wanaosema kuwa mapambano ndani ya bunge yangekuwa ni kupoteza muda tu unajua adui yako akitoka bungeni anaelekea wapi nenda kamsubiri huko huko umalizane naye.
 
Mkuu wangu,the only difference i could see ni kama CDM wana uhakika kuwa JK atawakubalia kuwa ajipunguzie madaraka kwenye kuunda katiba mpya.
 
jambo lingine ambalo mushi lazima ulielewe ni kwamba kitendo cha chadema kutoka nje ya ukumbi wa bunge kupinga mswaada kimeuathili sana mswaada mzima kwa maana the whole world is watching kwa kitendo chao walichokifanya na binafsi naamini kuwa endapo CDM wangekubali kupitia mlango wa 86 kama Pasco alivopendekeza hilo ndio lingekuw kaburi lao maana ccm wangesema umeleta hoja yako ukasikilizwa na spika akaamuru kura hoja yako imeanguka na sasa unalazimisha hoja mara baada ya kushindwa kwenye kura lakini kwa kitendo chao cha kukataa kushiriki kimewapa political cover ya kwenda kokote wanakotaka na huenda kama wangepitiakifungu hicho cha 86 na kushindwa huenda JK angekataa kukutana nao na angesema malalamiko yenu yalisikilizwa na spika kura zikapigwa mkashindwa kwao mnanipoteea muda.
 
Kwasababu madai ya Pasco yalikuwa ni kwanini CDM hawaku exhaust ile procedure ya kupinga muswada kwa kutumia kifungu cha 86,nimeona kama madai yake kuhusu hiyo mistake ya CDM ni ya ukweli kwakuwa wapenzi na wanachama wa CDM walipingana naye kwa kusema mwishowe Speaker ndiye mwamuzi kwani anaweza kuitisha upigaji kura miongoni mwa wabunge,na kwasababu wabunge wa CCM ni wengi zaidi,basi waka assume kuwa hawatafika mahali...Pia kuna waliosema ni jambo ambalo lilishawahi kutokea huko nyuma.

Swali linakuja,je hakuna nyakati ambazo upinzani umefanya kikao na rais?CUF walishawahi kuwa na viao vya aina hiyo pia wakati wa Mkapa...

Kwa upande mwingine,CDM wameomba kuonana na Mh Rais,je hilo lina tofauti gani na situation iliyopita ya kujaribu kuupinga muswada bungeni pale walipokuwa na opportunity hiyo bila kujali kama watafanikiwa ama la?Given ukweli wa wazi kabisa kuwa JK hawezi kula matapishi yake?

Je kama ni kweli kuna wapenzi wa CDM humu wanadai kuwa hata akikataa basi CDM itatumia nafasi hiyo kuwaambia wananchi kuwa tulimwambia ila "akaweka pamba masikioni"

Je kwanini hawakutumia standards hizo hizo wakati walipokuwa bungeni ili waje kuwaambia wananchi kuwa tulimwambia spika na bunge lakini "wakaweka pamba" masikioni?

Mimi siendi all the wa kuwaambia kwamba mkubali yaishe kama Pasco alivyosema, kwamba muwaachie CCM waandae utaratibu wa kupata katiba mpya,however nakubaliana na Pasco kwamba that was a mistake.

Kama nikizichukulia hizi issue within the same standards,then ni kweli CDM walikosea.

So Pasco was definetly right...

Kama walijuwa hoja yao haitashinda bungeni, ni nini kinawafanya wadhani kuwa itapita kwa Rais?

Ni vigezo gani?Binafsi siamini kabisa kuwa Rais atabadili mawazo kwenye kikao hicho,just kama vile ambavyo wao hawakuamini kwamba hoja yao itafanikiwa bungeni, kwani whats the diference?

Mkuu Jmushi1, nadhani pamoja na ku-anticipate matokeo ya bungeni na kutoka kwa raisi lakini hizi platform ni tofauti kabisa. Pale bungeni kama tulivyoshuhudia huko nyuma ni party politics, zomea zomea na mwisho kura and as you know kura majibu yake yanakuwaje. Lakini kwa hili la one on one na prezidaa tofauti yake ni kwamba raisi atakuja na wataalamu wake (That is what I predict), hoja baada ya hoja zitajadiliwa. Na hapa pia JK atapata nafasi ya kuona washauri wake wanavyojenga hoja dhidi ya hoja za CHADEMA. Na kama walimdanganya ili kumfurahisha hapa ndiyo itakuwa opportunity kutambua. Hapa hakuna kupiga kura wala zomea zomea ni hoja kwa hoja na hata kama JK ataamua kutozingatia ushauri wa CHADEMA itabidi ajibu hivyo kihoja tena hadharani na si tu kwa kusema ndiyooooooooo!!!!!! au hapaanaaaaaaaaaa!!!!!!!!!!! kama kule bungeni. Wananchi tutapima uzito wa majibu ya hoja za raisi dhidi ya zile za CHADEMA and I think hicho ndicho haswa CHADEMA wanachokitarajia iwapo mambo yataenda kombo.

Sidhani katika mjadala huo prezidaa anaweza kuleta watu kama akina Lusinde, Rage au Wassira. Hoja zikiwa dhaifu it will be a self defeat kwa taasisi ya uraisi. Kumbuka pia expectations za wananchi kuhusu hoja za JK, definetely kutokana na hilo licheo la uraisi the bar is set as high as possible.

Hii pia ni nafasi kwa JK akitaka kuonyesha kwamba he is the only adult in the room. Lakini pia ni opportunity kwa CHADEMA kuonyesha kwamba wana nia na dhamira ya kutetea ukweli iwe kwa maridhiano, majadiliano au maandamano. Let's wait and see.
 
Itakuwa ni "a big slap on the face to Anna Makinda na all CCM's and CUF MPs" kwa rais kutousaini mswada huo kuwa sheria! Sioni namna rais ataacha kuusaini mswada huo baada ya hutoba yake aliyoitoa wakati wakuupitasha mswada na baada ya CCM na CUF kuutetea mswada bungeni kwa nguvu zao zote! Rais asipousaini, CCM na CCM-B (CUF) watadhihirika kuwa walifanya ujuha kuutetea muswada, jambo ambalo linaweza kumletea rais uasi ndani ya CCM. Kwa sasa mambo yalivyo ndani ya CCM mwenyekiti anaonekana amedhoofika kutokana na kundi la magamba matatu kupata muda wa siku 90 wakujiimarisha.

Labda rais awaahidi Chadema some concessions kama kuunda tume itakayowashirikisha au kutoa mawazo ya watu fulani kama Zitto alivyodokeza. Lakini piga ua, kwa kiburi cha CCM, muswada lazima kusainiwa kuwa sheria hata kama baadhi ya watu watamwaga damu. Ndivyo nionavyo mimi!
 
Mkuu wangu,the only difference i could see ni kama CDM wana uhakika kuwa JK atawakubalia kuwa ajipunguzie madaraka kwenye kuunda katiba mpya.

Mkuu jmushi1, hapa naona kuna maswali mawili yanayohitaji kuzingatiwa kwa uangalifu kuhusu huu mkutano;

  • Kwanza, je haya ni majadiliano kati ya Mwenyekiti wa CCM na Mwenyekiti wa Chadema ?
  • Au pili, ni majadiliano kati ya kiongozi wa serikali na kiongozi wa chama Kikuu cha Upinzani.

Wabunge wengi wa CCM kama tunavyoshuhudia siku zote ni wanafiki ndani ya bunge na waoga ndani ya vikao vya chama. Hivyo kuna umuhimu kwa Chadema kabla hawajaenda kwa wananchi, kumfikishia ujumbe Raisi kama kiongozi wa serikali na si Mweyekiti wa CCM. Pia ni lazima wajiridhishe kuwa mengi yaliyoongelewa ndani ya bunge yalikuwa na baraka za Raisi. Hii ni kwa sababu si mara moja ama mbili tumeshuhudia Raisi akikana ama yeye binafsi au maofisa wake maneno aliyoyatamka kama pale anapokutana na wazee (wa CCM?). Hivyo Chadema watapata fursa nzuri ya kupata ushahidi katika mazungumzo ya ana kwa ana yanayojulikana kama "one on one" na kuweza kusoma "body language" yake.
 
Sorry mkuu kwanza hii nchi ina Rais??Maana naona tunaendeshwa tu na watu mbali mbali na sio RAIS
a_president.jpg

Mkuu jmushi1, hapa naona kuna maswali mawili yanayohitaji kuzingatiwa kwa uangalifu kuhusu huu mkutano;

  • Kwanza, je haya ni majadiliano kati ya Mwenyekiti wa CCM na Mwenyekiti wa Chadema ?
  • Au pili, ni majadiliano kati ya kiongozi wa serikali na kiongozi wa chama Kikuu cha Upinzani.

Wabunge wengi wa CCM kama tunavyoshuhudia siku zote ni wanafiki ndani ya bunge na waoga ndani ya vikao vya chama. Hivyo kuna umuhimu kwa Chadema kabla hawajaenda kwa wananchi, kumfikishia ujumbe Raisi kama kiongozi wa serikali na si Mweyekiti wa CCM. Pia ni lazima wajiridhishe kuwa mengi yaliyoongelewa ndani ya bunge yalikuwa na baraka za Raisi. Hii ni kwa sababu si mara moja ama mbili tumeshuhudia Raisi akikana ama yeye binafsi au maofisa wake maneno aliyoyatamka kama pale anapokutana na wazee (wa CCM?). Hivyo Chadema watapata fursa nzuri ya kupata ushahidi katika mazungumzo ya ana kwa ana yanayojulikana kama "one on one" na kuweza kusoma "body language" yake.

Wanafik ni wale wanaosusasusa, si mlimsusia Kikwete Bungeni akawaambia nini? sasa leo mnapanga kwenda kumuona nani? kama si unafik huo ni nini?
 
Itakuwa ni "a big slap on the face to Anna Makinda na all CCM's and CUF MPs" kwa rais kutousaini mswada huo kuwa sheria! Sioni namna rais ataacha kuusaini mswada huo baada ya hutoba yake aliyoitoa wakati wakuupitasha mswada na baada ya CCM na CUF kuutetea mswada bungeni kwa nguvu zao zote! Rais asipousaini, CCM na CCM-B (CUF) watadhihirika kuwa walifanya ujuha kuutetea muswada, jambo ambalo linaweza kumletea rais uasi ndani ya CCM. Kwa sasa mambo yalivyo ndani ya CCM mwenyekiti anaonekana amedhoofika kutokana na kundi la magamba matatu kupata muda wa siku 90 wakujiimarisha.

Labda rais awaahidi Chadema some concessions kama kuunda tume itakayowashirikisha au kutoa mawazo ya watu fulani kama Zitto alivyodokeza. Lakini piga ua, kwa kiburi cha CCM, muswada lazima kusainiwa kuwa sheria hata kama baadhi ya watu watamwaga damu. Ndivyo nionavyo mimi!

Hivi ndio fikra zako kuwa Rais hatousaini? umepotea step.

Muswada hauna tatizo, hao wenzako wanatafuta umaarufu tu, hawana pakutokea walisha kosea sasa hawataki kuoneka mambumbumbu. Maana kuna usomi wa mwanasheria fulani ulikuwa questioned sana. Huwezi kama mwanasheria kweli kweli ukatowa maoni ya upinzani kuhusu muswaada halafu wakati unaanza kujadiliwa ujidai huutaki unasusa, huo ni upunguani.
 
Kwasababu madai ya Pasco yalikuwa ni kwanini CDM hawaku exhaust ile procedure ya kupinga muswada kwa kutumia kifungu cha 86,nimeona kama madai yake kuhusu hiyo mistake ya CDM ni ya ukweli kwakuwa wapenzi na wanachama wa CDM walipingana naye kwa kusema mwishowe Speaker ndiye mwamuzi kwani anaweza kuitisha upigaji kura miongoni mwa wabunge,na kwasababu wabunge wa CCM ni wengi zaidi,basi waka assume kuwa hawatafika mahali...Pia kuna waliosema ni jambo ambalo lilishawahi kutokea huko nyuma.

Kwa upande mwingine,CDM wameomba kuonana na Mh Rais,je hilo lina tofauti gani na situation iliyopita ya kujaribu kuupinga muswada bungeni pale walipokuwa na opportunity hiyo bila kujali kama watafanikiwa ama la?Given ukweli wa wazi kabisa kuwa JK hawezi kula matapishi yake?

Je kama ni kweli kuna wapenzi wa CDM humu wanadai kuwa hata akikataa basi CDM itatumia nafasi hiyo kuwaambia wananchi kuwa tulimwambia ila "akaweka pamba masikioni"

Je kwanini hawakutumia standards hizo hizo wakati walipokuwa bungeni ili waje kuwaambia wananchi kuwa tulimwambia spika na bunge lakini "wakaweka pamba" masikioni?

Mimi siendi all the wa kuwaambia kwamba mkubali yaishe kama Pasco alivyosema, kwamba muwaachie CCM waandae utaratibu wa kupata katiba mpya,however nakubaliana na Pasco kwamba that was a mistake.

Kama nikizichukulia hizi issue within the same standards,then ni kweli CDM walikosea.

So Pasco was definetly right...

Kama walijuwa hoja yao haitashinda bungeni, ni nini kinawafanya wadhani kuwa itapita kwa Rais?

Ni vigezo gani?Binafsi siamini kabisa kuwa Rais atabadili mawazo kwenye kikao hicho,just kama vile ambavyo wao hawakuamini kwamba hoja yao itafanikiwa bungeni, kwani whats the diference?
Mkuu Mushi, mboni safo meku! ha ha ha
Kwanza niweke sawa kuwa thread yako imelenga kujibiwa na wapenzi na wanachama wa Chadema. Sijui sisi tusio na mrengo tunapaswa kuchangia au la. Hata hivyo natanguliza samahani kama nitakuwa nimevuka mstari wa vyama kwasababu huko sipo.

Kuhusu hoja ya Pasco mengi yameshaongelewa na kila mtu atabaki kuamini kile anachodhani ni sahihi au si sahihi na nisingependa kurejea huko. Ninachotaka kuchangia hapa ni hoja ya utaifa kwasababu naamini taifa lipo hata kama hakuna vyama vya siasa.

Ikumbukwe kwamba suala la katiba ni la taifa na si vyama. Wananchi tumevutika katika mkumbo huo kwa kudhani kipo chama kinachopaswa kuandika katiba au chama kushinikikiza uwepo wa katiba. Ndiyo maana tumeona wale vijana waliochaguliwa kwa kofia hiyo wakiwa kimya kuliko wazee na hapa ni somo kuwa ujana na usomi haumaniishi busara wala hekima. Ni lazima tufikirie njia nyingine ya kupata viongozi si kwa kutumia ujana.

Uchaguzi uliopita hali ilikuwa ni tete sana kiasi cha viongozi wa dini kumfuata Slaa kwani kauli iliyokuwa inasubiriwa ni yake moto uwake. Kwa hekima za wazee na viongozi hao pamoja na hekima za Slaa na chama chake tumeweza kuvuka mawimbi hayo tukiwa wamoja. Inaweza kuonekana ni udhaifu lakini huo ni utaifa na busara na lazima tukubali hilo.

Ikumbukwe CDM ndio waliotia shinikizo la kuandika katiba mpya, na rais alipolichukua bila ya idhini ya chama chake au serikali yake CDM walikubaliana nalo pengine kwa busara hata kama mimi sikubaliani na busara zao.

Wanachokataa CDM ni utaratibu wa kupata katiba, na hakuna mtu mwenye akili timamu anayeweza kukubali kuwa CCM wanatumia busara, hakuna! kuna shida gani ya kuongelea mambo ya kitaifa kwa upana hadi kila jambo liwe rush rush na hata mijadala kuzuiwa si bungeni tu hata kwenye hiyo katiba yenyewe! Tunachokiona ni wabunge wa CCM hasa vijana waliokaa kimya na kulisaliti taifa kwa vipande vitatu vya allowance.

Hali si nzuri na wanchokifanya CDM ni busara kama nilizoeleza hapo juu. Nakubaliana nao ingawa ni udhaifu lakini katika utaifa wana mahali pa kusimama na kusema tulijaribu hatua abcd ikishindikana.

Ninachosema ni kuwa hatua zinazochukuliwa tuziangalie kwa upana na busara zake na si katika u-yanga na u-simba.
Kama bunge lenye wasomi tena vijana limeshindwa kuwa na busara hiyo si sababu ya wengine kutokuwa na busara, na endapo rais hatatumia busara Tanzania ya leo si ya jana na awe tayari kubeba lawama zitokanazo na ukosefu wa busara zaidi ya aliyoonyesha.
 
Mkuu Mushi, mboni safo meku! ha ha ha
Kwanza niweke sawa kuwa thread yako imelenga kujibiwa na wapenzi na wanachama wa Chadema. Sijui sisi tusio na mrengo tunapaswa kuchangia au la. Hata hivyo natanguliza samahani kama nitakuwa nimevuka mstari wa vyama kwasababu huko sipo.

Kuhusu hoja ya Pasco mengi yameshaongelewa na kila mtu atabaki kuamini kile anachodhani ni sahihi au si sahihi na nisingependa kurejea huko. Ninachotaka kuchangia hapa ni hoja ya utaifa kwasababu naamini taifa lipo hata kama hakuna vyama vya siasa.

Ikumbukwe kwamba suala la katiba ni la taifa na si vyama. Wananchi tumevutika katika mkumbo huo kwa kudhani kipo chama kinachopaswa kuandika katiba au chama kushinikikiza uwepo wa katiba. Ndiyo maana tumeona wale vijana waliochaguliwa kwa kofia hiyo wakiwa kimya kuliko wazee na hapa ni somo kuwa ujana na usomi haumaniishi busara wala hekima. Ni lazima tufikirie njia nyingine ya kupata viongozi si kwa kutumia ujana.

Uchaguzi uliopita hali ilikuwa ni tete sana kiasi cha viongozi wa dini kumfuata Slaa kwani kauli iliyokuwa inasubiriwa ni yake moto uwake. Kwa hekima za wazee na viongozi hao pamoja na hekima za Slaa na chama chake tumeweza kuvuka mawimbi hayo tukiwa wamoja. Inaweza kuonekana ni udhaifu lakini huo ni utaifa na busara na lazima tukubali hilo.

Ikumbukwe CDM ndio waliotia shinikizo la kuandika katiba mpya, na rais alipolichukua bila ya idhini ya chama chake au serikali yake CDM walikubaliana nalo pengine kwa busara hata kama mimi sikubaliani na busara zao.

Wanachokataa CDM ni utaratibu wa kupata katiba, na hakuna mtu mwenye akili timamu anayeweza kukubali kuwa CCM wanatumia busara, hakuna! kuna shida gani ya kuongelea mambo ya kitaifa kwa upana hadi kila jambo liwe rush rush na hata mijadala kuzuiwa si bungeni tu hata bali kwenye hiyo katiba yenyewe! Tunachokiona ni wabunge wa CCM hasa vijana waliokaa kimya na kulisaliti taifa kwa vipande vitatu vya allowance.

Hali si nzuri na wanchokifanya CDM ni busara kama nilizoeleza hapo juu. Nakubaliana nao ingawa ni udhaifu lakini katika utaifa wana mahali pa kusimama na kusema tulijaribu hatua abcd ikishindikana.

Ninachosema ni kuwa hatua zinazochukuliwa tuziangalie kwa upana na busara zake na si katika u-yanga na u-simba.
Kama bunge lenye wasomi tena vijana limeshindwa kuwa na busara hiyo si sababu ya wengine kutokuwa na busara, na endapo rais hatatumia busara Tanzania ya leo si ya jana na awe tayari kubeba lawama zitokanazo na ukose wa busara zaidi ya aliyoonyesha.
Mkuu Nguruvi3 nimekupata na maoni yako huwa nayaheshimu sana.

Mimi wala sina shida na hatua za CDM.

Nilikuwa tu concerened kutokana na mjadala ulioanzishwa na Pasco.

Kwakuwa sikuwezakutizama yaliyoendelea,ila niligunduwa kuwa ni swali aliloulizwa Tundu Lissu na mmojawapo wa waandishi wa habari.

Pasco ndiyo akaileta issue,na kwa jinsi mjadala ulivyokuwa ukiendelea na matukio mengine pia kutokea,nimekuja kugundua the guy's argument was actually correct.

Hicho tu.
 
JMushi1, Nijuavyo mimi CDM wancxhokifanya ni wajibu wao kwa maslahi yako wewe mwananchi. Hawana ulazima kama chama kwenda kukutana na JK zaidi ya maswala ya uchaguzi ambayo kuna dalili kubwa CDM wakazizoa kura za wananchi mwaka 2015. Aws a fact CDM inawasaidia CCM kufufuka hasa pale JK atakapoweza kuwapatia wananchi katiba bora..

Kama kulikuwepo na makosa Bungeni yamefanywa na Spika kwa makusudi kabisa kukataa HOJA za wabunge ambao walitaka bunge liahirishwe na kwa jeuri alisema hakuna HOJA kwa kila aliyedai mwongozo!..Kwa hiyo, tusonge mbele kila siku huja na mema zaidi na huu sio mwisho wa kuendeleza madai yetu iwe CDM au NCCR- Mageuzi hawa wote ni watumishi wa Umma kama alivyo rais wetu.

Na muhimu kwanza tukumbuke kwamba JK ni rais wa nchi na kila analofanya ni kwa maslahi ya Taifa hata kama anakosea wenye kuathirika ni sisi sio CCM wala CDM kwa sababu hawa wote ni binadamu na maamuzi mabaya yanaweza pia athiri maisha yao wakiwa ndani ya chama au nje....
Mkuu Mkandara kwani Spika si anateuliwa na Rais?
 
Mag3 said:
Pia ni lazima wajiridhishe kuwa mengi yaliyoongelewa ndani ya bunge yalikuwa na baraka za Raisi.
Mkuu kwa uhakika kabisa?

Nasubiri nione hayo makubaliano...
 
Mkuu Mushi, mboni safo meku! ha ha ha
Kwanza niweke sawa kuwa thread yako imelenga kujibiwa na wapenzi na wanachama wa Chadema. Sijui sisi tusio na mrengo tunapaswa kuchangia au la. Hata hivyo natanguliza samahani kama nitakuwa nimevuka mstari wa vyama kwasababu huko sipo.

Kuhusu hoja ya Pasco mengi yameshaongelewa na kila mtu atabaki kuamini kile anachodhani ni sahihi au si sahihi na nisingependa kurejea huko. Ninachotaka kuchangia hapa ni hoja ya utaifa kwasababu naamini taifa lipo hata kama hakuna vyama vya siasa.

Ikumbukwe kwamba suala la katiba ni la taifa na si vyama. Wananchi tumevutika katika mkumbo huo kwa kudhani kipo chama kinachopaswa kuandika katiba au chama kushinikikiza uwepo wa katiba. Ndiyo maana tumeona wale vijana waliochaguliwa kwa kofia hiyo wakiwa kimya kuliko wazee na hapa ni somo kuwa ujana na usomi haumaniishi busara wala hekima. Ni lazima tufikirie njia nyingine ya kupata viongozi si kwa kutumia ujana.

Uchaguzi uliopita hali ilikuwa ni tete sana kiasi cha viongozi wa dini kumfuata Slaa kwani kauli iliyokuwa inasubiriwa ni yake moto uwake. Kwa hekima za wazee na viongozi hao pamoja na hekima za Slaa na chama chake tumeweza kuvuka mawimbi hayo tukiwa wamoja. Inaweza kuonekana ni udhaifu lakini huo ni utaifa na busara na lazima tukubali hilo.

Ikumbukwe CDM ndio waliotia shinikizo la kuandika katiba mpya, na rais alipolichukua bila ya idhini ya chama chake au serikali yake CDM walikubaliana nalo pengine kwa busara hata kama mimi sikubaliani na busara zao.

Wanachokataa CDM ni utaratibu wa kupata katiba, na hakuna mtu mwenye akili timamu anayeweza kukubali kuwa CCM wanatumia busara, hakuna! kuna shida gani ya kuongelea mambo ya kitaifa kwa upana hadi kila jambo liwe rush rush na hata mijadala kuzuiwa si bungeni tu hata bali kwenye hiyo katiba yenyewe! Tunachokiona ni wabunge wa CCM hasa vijana waliokaa kimya na kulisaliti taifa kwa vipande vitatu vya allowance.

Hali si nzuri na wanchokifanya CDM ni busara kama nilizoeleza hapo juu. Nakubaliana nao ingawa ni udhaifu lakini katika utaifa wana mahali pa kusimama na kusema tulijaribu hatua abcd ikishindikana.

Ninachosema ni kuwa hatua zinazochukuliwa tuziangalie kwa upana na busara zake na si katika u-yanga na u-simba.
Kama bunge lenye wasomi tena vijana limeshindwa kuwa na busara hiyo si sababu ya wengine kutokuwa na busara, na endapo rais hatatumia busara Tanzania ya leo si ya jana na awe tayari kubeba lawama zitokanazo na ukose wa busara zaidi ya aliyoonyesha.
Kwanza kabisa, sikubaliani na neutrality yako. Ni jambo la maana kuweka bayana wewe unasimamia upande gani. Hata hivyo wanaforum ndiyo watahukumu na somehow wameshajua upo upande gani.
But anyways, nimejaribu kuangalia statements zako ambazo kwa namna fulani ziko mbali na ukweli kutokana na either ushabiki kwa upande wako au ukosefu wa takwimu ambao either unatokana na serikali na taasisi nyingine za jamii kutokuwa na interest, fedha au ulimbukeni wa vielelezo vya takwimu on both your side, my side and the government and all other institutions, especially the media.
Wantanzania wengi hawaijui katiba yetu, hawana interest na kujua katiba for some reasons. Wasomi wa Tanzania nao wengi hawajui katiba yetu, hata waandishi wa habari , wanasiasa n.k wengi wao hawaifahamu katiba yetu. Kwa hiyo ukisema mabadiliko au katiba mpya, wengi wao hawatakuelewa unamaanisha nini hasa (this is open for debate).
Kuhusu statement yako kwamba hakuna mtu mwenye akili timamu anaweza kuamini kuwa CCM wanatumia busara, hizo ndio statements zinazowaweka CDM mbali na middle class ya watanzania, kwani tunajua peasants huwa hawawaelewi hata mkitumia miaka yote mitano focusing on them. Katiba mpya siyo hoja ya watanzania, hiyo propaganda ondoa kichwani mwako kabisa na nitakwambia kwanini nasema hivyo.
Kwanza kabisa, kumekuwa na articles nyingi zinazomnukuu Dr. Slaa kuhusu serikali za majimbo i.e Tanzania iwe Federated yaani iwe na states zinazotokana na kanda, nadhani unanielewa. Watanzania hawataki hii.
Pili, ukisema kwamba CDM wanakataa utaratibu wa kupata katiba, hapo pia unakuwa unatuchuuza kwa sababu CDM wana fikra zao za jinsi katiba mpya inavyotakiwa iwepo. Wanataka tuanze ku define boundaries za Jamhuri yetu, kwamba kuwe na serikali ya Tanganyika, kitu ambacho watanzania bara wengi hawaoni umuhimu wake. Ni jinsi gani serikali ya Tanganyika itatuletea maendeleo? Kwani wazanzibari wanatuzuiaje sisi watanzania bara kuwa na maendeleo just because hatuna serikali yetu? Mheshimiwa Tundu Lissu ameonyesha dhahiri interest yake ya kuua muungano, ameonyesha dhahiri interest yake ya kurudisha serikali ya Tanganyika, why/,I don't know. Kwa hiyo usitupotoshe kuwa CDM wanachogombania ni jinsi ya kuipata katiba mpya, wanachogombania ni katiba kama wanavyoitaka wao.
Swali langu kwa CDM, nani amewapa mandate ya kuunda katiba mpya? CCM wanayo mandate kutoka kwa majority of people, ndiyo maana kuna option kama wanataka katiba mpya au wanataka marekebisho. Let the people talk.
Mandate ya CCM inatokana na uchaguzi wa 2010 na uchaguzi wa serikali za mitaa ambapo CCM imewashinda wapinzani wote kwa ujumla, CCM wana bunge na LAGs pamoja na rais, kwa hiyo sioni kwanini wasomi hawaichukulii hii kama mandate ya CCM kutunga hii katiba.
Mwisho kabisa, badala ya kutumia kete ya uchakachuliwaji wa uchaguzi mkuu, naomba tubase kwenye uchaguzi wa serikali za mitaa. Je nao ulichakachuliwa? Kama hapana, can we use it as a mandate from the people of URT kwamba CCM ndio iwaamulie mambo yao? i.e iwa represent?
Just give me one credible datum (scientific with methodology and populus composition) ambayo imeonyesha kuwa watanzania wengi wanataka katiba mpya based on CDM's propositions a.k.a peoples???? propositions.

Wasalaam.
 
Magufuli sasa hivi ITV anaoneshwa akifunguwa ujenzi kwa kiwango cha lami barabara ya Mayamaya Dodoma.: Kilomita 11,600 wakati huu wa Kikwete Tanzania nzima ama zimeshaanza kujengwa ama mikataba imesha sainiwa, ni nyingi kuliko nchi yoyote ya Afrika kwa sasa, 80% ya gharama kutoka bajeti ya ndani.

Sasa hizo elfu tano zako ulizitowa wapi? Hivi kwanini mnapenda kudanganya hata kwenye ukweli? tena amesema wale wanaopenda kuandamana waandamane kwenye barabara za lami.

Una uhakika kwamba barabara ya Mayamaya Dodoma ina urefu wa km 11,600?? bila shaka umeangalia ITV kwa makengeza, ama hujui jiografia ya nchi hii!

Huyo Mwita kazi yake ni kusema uwongo...JK is above all presidents hawataki hilo...wanataka wale wenzao..

Ona huyu naye sijui kakurupushwa na nani, hapa sio uwanja wa ku-propagate udini wa gerezani, ebo!!
 
Kwanza kabisa, sikubaliani na neutrality yako. Ni jambo la maana kuweka bayana wewe unasimamia upande gani. Hata hivyo wanaforum ndiyo watahukumu na somehow wameshajua upo upande gani.
But anyways, nimejaribu kuangalia statements zako ambazo kwa namna fulani ziko mbali na ukweli kutokana na either ushabiki kwa upande wako au ukosefu wa takwimu ambao either unatokana na serikali na taasisi nyingine za jamii kutokuwa na interest, fedha au ulimbukeni wa vielelezo vya takwimu on both your side, my side and the government and all other institutions, especially the media.
Wantanzania wengi hawaijui katiba yetu, hawana interest na kujua katiba for some reasons. Wasomi wa Tanzania nao wengi hawajui katiba yetu, hata waandishi wa habari , wanasiasa n.k wengi wao hawaifahamu katiba yetu. Kwa hiyo ukisema mabadiliko au katiba mpya, wengi wao hawatakuelewa unamaanisha nini hasa (this is open for debate).
Kuhusu statement yako kwamba hakuna mtu mwenye akili timamu anaweza kuamini kuwa CCM wanatumia busara, hizo ndio statements zinazowaweka CDM mbali na middle class ya watanzania, kwani tunajua peasants huwa hawawaelewi hata mkitumia miaka yote mitano focusing on them. Katiba mpya siyo hoja ya watanzania, hiyo propaganda ondoa kichwani mwako kabisa na nitakwambia kwanini nasema hivyo.
Kwanza kabisa, kumekuwa na articles nyingi zinazomnukuu Dr. Slaa kuhusu serikali za majimbo i.e Tanzania iwe Federated yaani iwe na states zinazotokana na kanda, nadhani unanielewa. Watanzania hawataki hii.
Pili, ukisema kwamba CDM wanakataa utaratibu wa kupata katiba, hapo pia unakuwa unatuchuuza kwa sababu CDM wana fikra zao za jinsi katiba mpya inavyotakiwa iwepo. Wanataka tuanze ku define boundaries za Jamhuri yetu, kwamba kuwe na serikali ya Tanganyika, kitu ambacho watanzania bara wengi hawaoni umuhimu wake. Ni jinsi gani serikali ya Tanganyika itatuletea maendeleo? Kwani wazanzibari wanatuzuiaje sisi watanzania bara kuwa na maendeleo just because hatuna serikali yetu? Mheshimiwa Tundu Lissu ameonyesha dhahiri interest yake ya kuua muungano, ameonyesha dhahiri interest yake ya kurudisha serikali ya Tanganyika, why/,I don't know. Kwa hiyo usitupotoshe kuwa CDM wanachogombania ni jinsi ya kuipata katiba mpya, wanachogombania ni katiba kama wanavyoitaka wao.
Swali langu kwa CDM, nani amewapa mandate ya kuunda katiba mpya? CCM wanayo mandate kutoka kwa majority of people, ndiyo maana kuna option kama wanataka katiba mpya au wanataka marekebisho. Let the people talk.
Mandate ya CCM inatokana na uchaguzi wa 2010 na uchaguzi wa serikali za mitaa ambapo CCM imewashinda wapinzani wote kwa ujumla, CCM wana bunge na LAGs pamoja na rais, kwa hiyo sioni kwanini wasomi hawaichukulii hii kama mandate ya CCM kutunga hii katiba.
Mwisho kabisa, badala ya kutumia kete ya uchakachuliwaji wa uchaguzi mkuu, naomba tubase kwenye uchaguzi wa serikali za mitaa. Je nao ulichakachuliwa? Kama hapana, can we use it as a mandate from the people of URT kwamba CCM ndio iwaamulie mambo yao? i.e iwa represent?
Just give me one credible datum (scientific with methodology and populus composition) ambayo imeonyesha kuwa watanzania wengi wanataka katiba mpya based on CDM's propositions a.k.a peoples???? propositions.

Wasalaam.

Kwanza kabisa utambue kwamba hatukuwachagua wabunge kwenda kuzungumza mawazo yao binafsi bungeni, kwamba mbunge anashauriana na mke/mme wake na watoto wake halafu anakwenda bungeni kusema hayo ndio mawazo ya wapiga kura wake. Katika huu muswada wa marekebisho ya katiba hakuna mbunge hata mmoja aliyefanya mkutano wowote uwe wa ndani ama wa nje jimboni kwake na kupata maoni ya wananchi wake, hakuna!Wale wanaosema waliwakilisha mawazo ya wapiga kura wao ni waongo, wakiongozwa na anne kilango malecela.

Na pili, hata kama ccm imepata ushindi na kuunda serikali, haina uhalali wa kudictate kila jambo, kuna mambo tunaweza kukubali wakayafanya kwa niaba yetu hasa yale yaliyomo kwenye ilani yao ya uchaguzi ambayo hayana athari ya moja kwa moja na kila mwananchi mmoja mmoja. Na kwakuwa watanzania tuliokuwa na haki ya kupiga kura mwaka 2010 kwa mujibu wa sheria na NEC tulikuwa takriban milioni 20 lakini tuliopiga kura ni takribani milioni 8, ni dhahiri kwamba ccm inakosa political legitimacy ya kuiongoza nchi hii, kwani imechaguliwa na takribani watu milioni 5 kati ya wapiga kura halali milioni 20! kwahiyo hawawezi kufanya mambo na kujipiga kifua kwamba wao ndio wenye dhamana ya kila kitu, kisiasa wana pwaya kwa kukosa kuungwa mkono na watanzania wengi. Hao milioni 15 wasioipoigia kura ccm(ninamaanisha waliochagua vyama vya upinzani-milioni 3+milioni 12 wasiopiga kura huwezi kuwachukulia kirahisi namna hiyo.

Na tatu, katika maswala ambayo serikali yoyote hata iliyochaguliwa kwa ushindi wa 100% haiwezi kuyafanya bila kushirikisha wananchi wenyewe kuanzia hatua ya mwanzo ni hili la katiba. Katiba si mali ya chama wala serikali, katiba ni mali ya wananchi wenyewe na kwahali hiyo wao wenyewe ndio wanapaswa kuamua katiba yao iweje bila kuwekewa mizengwe ama kipingamizi chochote. Na hapa hakuna mtu yeyote anayeweza kujivika usemaji wa wananchi, na hapa wabunge wanalazimika kwenda kwa wananchi moja kwa moja na kupata maoni yao, na ndio hayo wanatakiwa kuyawasilisha bungeni na si vinginevyo.

Katiba inayotafutwa kutungwa hapa ni ya wananchi wenyewe, si ya ccm, chadema, cuf, nccr wala cck!! Kwahiyo wananchofanya chadema hapa ni kupaza sauti ya kuitaka ccm na serikali yake wazingatie maslahi mapana ya wananchi wote. Na kama wananchi wenyewe wataachwa watunge katiba yao, hakuna cha chadema, ccm ama cuf watakao dai hiyo ni katiba yao, itakuwa ni katiba ya wananchi wote, na chadema, ccm, cuf na wengineo watafaidika nayo kama watanzania wengine.

Na mwisho, nikukumbushe kwamba katiba mpya haikuwa agenda ya ccm, kwenye ilani yao hawakuwahi kusema habari ya katiba mpya. Waziri wa sheria na katiba Bi.Kombani na mwanasheria mkuu wa serikali walipoulizwa kuhusu madai na mahitaji ya katiba mpya wote tunakumbuka walikataa kata kata kwamba nchi hii haihitaji katiba mpya kwa sasa, lakini raisi alipotangaza kukubali kuanzisha mchakato wa katiba mpya, kitu ambacho hakikuwepo kwenye ilani ya chama chake, ni kwamba alikuwa ametambua mahitaji ya wananchi wa Tanzania, na kwahiyo watanzania wenyewe wanapaswa kuachiwa kuongoza na kuhitimisha mchakato huo.
 
Back
Top Bottom