Katiba inakupa uhuru wa kukosoa/kutoa maoni haikupi uhuru wa kutoa lugha za kuudhi na kuchonganisha

Kila mtanzania ana uhuru wa kutoa Mawazo.Rais mstaafu Mwinyi alitoa mawazo kama mtanzania mwingine.Rais Mkapa aliwaita wapumbavu wale wasiojua kuwa Tanzania ilisha kombolewa toka mikononi mwa wakoloni.Angalia kamusi ya uone mtu ambae haui kitu na hataki kuelimishwa anaitwa nani?
 
Kasome kiswahili kwanza...Hauluhusiwi=Hauruhusiwi.
 
N
Kwa mantiki yake hata raisi alivyosema atachomoa mwingine mwenye akili na sio wale VILAZA,,,nayo ni lugha ya kuuzi?

Sent using Jamii Forums mobile app
Rafiki unaonekana kazi ya kufikiri umemuachia Lisu to an extent kwamba kila anachoongea unapigia makofi,,,Rekebisha kiswahili chako kwanza ndio urudi hapa ''lugha ya kuuzi=lugha ya kuudhi''
 
Lisu kapelekwa chuo kama alivyopelekwa Lema ili awe ana "THINK WIDELY BEFORE SHOUT"
Akitoka Segerea atakuwa ni Great thinker"
 
Lisu kapelekwa chuo kama alivyopelekwa Lema ili awe ana "THINK WIDELY BEFORE SHOUT"
Akitoka Segerea atakuwa ni Great thinker"
Sana tu, waambie akitoka atakuwa kanyooka.Yule muota ndoto haoti tena siku hizi
 
nitaendelea kuchomoa wenye akili, vilaza nawaacha huko huko.....
Naona hii ina lugha ya kufurahisha
 
Na kuwaita watu vilaza siyo lugha ya kuudhi? Au kusema kale "kabunge ka chadema" nayo imekaaje?
 

1. Tundu lisu alioposema wahisani wasusie, kwa mwenye akili fupi hawezi kuona usahihi wa Lisu.

Haiwezekani tuendelee kubebeshwa mizigo ya madeni ambayo tutalipa sisi walipa kodi, au kuhesabiwa tumepokea misaada ambayo matumizi yake hayafanyiki kwa mujibu wa vipaumbele na kanuni za taifa.

Nakupa mifano hii hapa chini.
a) Ninaomba useme hapa, ni lini bunge lilipitisha badgeti ya kujenga uwanja wa ndege wa kimataifa chato?
b) Lini bunge lilipitisha budget ya kununua ndege zinazonunuliwa kwa cash huku watu wakifa hosptailni kwa kukosa oxygen?
c) Ni wataalamu gani walifanya maamuzi ya kuweka vipaumbele vya kiuchumi na kjamii katika hayo masuala?
d) Wewe unaona ni halali Tanzania izidi kuingia katika madeni na matumizi ya raslimali yasiyokuwa na tija lakini sisi na watoto wetu waendelee kubeba zigo la kodi kulipa hayo madeni?
Nimtu mwenye ufahamu tu ndiye anaweze kuona upeo wa Lisu.

2. Ujinga ni kukosa ufahamu, maarifa ama taarifa sahihi. No one is informed in everything. Mwinyi aliposema alionyesha kukosa ufahamu.

Mtu mjinga anaondolewa ujinga kupewa taarifa sahihi na si kwa kutokuambiwa kwamba hajui.

Huwezi kulazimisha watu wote wasikie mtu anafurunda halafu eti waseme hayo ndiyo maarifa haswa na kupiga makofi. Unaweze kupongeza ujinga ukiwa mjinga na wewe ama mnafiki. Lakini waache wenye uelewa na wasio wanafiki wamsahihishe ili aondokane na ujinga. Tatizo liko kwapi?

a) Tunaposema adui wa Tanzania ni umaskini, maradhi, rushwa na ujinga, huwa tunawatukana Watanzania? Naomba uwe serious .

b) Lisu amesema Mwniy amenena ujinga. Nani mlalamikaji katika hilo shauri la mwingi kuambiwa kanena ujinga?

Wasaidie wasiotaka kuambiwa wamenena ujinga wasinene ujinga.

Ni yupi anayetahili kukamatwa kwa uahrifu wa maneno kati ya mtu anayesema "MTU ANAYETETEA UAHRIFU NI MJINGA", na ule anayesema " WATU WANAOTETEA SHERIA, HAKI NA UHURU WA BINADAMU, DEMOKSRASIA , RASLIMALI NA MAENDELEO YA TAIFA NI MALOFA NA MPAUMBAVU"????

3. Kwa hiyo wewe unataka watu wawe na uhuru wa kukosoa kikatiba lakini hutaki raisi akosolewe?

Anapoambiwa aangalie tribalism na nepotism zinaligawa taifa anakuwa anatukanwa?

Nyerere alipoambiwa anapendelea watu wa Kazkazini aliwatukana na kuwakamata walalamikaji na kuwatia ndani?

Unapashwa kuelewa kwamba "image analysis", ni strength kwa kila kiongozi makini?

Ukituhumiwa, angalia hilo eneo na ama alitolee ufafanuzi ama arekebishe. Kuwatia watu pingu kwa kuwa wamekukosoa tena kwa nji aza amani ni dalili ya tatizo kubwa kuliko lililoko mezani kwa saas.

Kushabikia suppression za feelings za watu na kuendesha mambo kwa ubabe mkitegemea bunduki, zinaweza kuleta machafuko makubwa sana hapa nchini.

MATUMIZI YA BUNDUKI HAJAWAHI KUJENGA MTANGAMANO WA KIJAMII NA WALA HAYAJAWAHI KUWA SIASA SAFI WALA UONGOZI BORA.
 
Waloitwa itwa wapumbavu ni wale ambao hawajui kuwa Tanzania ilisha kombolewa toka kwa wakoloni,,,,soma kamusi ya kiswahili uone mtu ambae hajui kitu na hataki kuelimishwa anaitwaje?
Wapumbavu ni nyinyi mliovalishwa miwani ya mbao na ccm

In God we trust
 
Jesus Christ was human being 100% and God at the same time 100% You cant equate human being with jesus
Tangu lini Bashite akajua kizungu?

In God we trust
 
Kama mnalijua hilo kwanini mnawakamata wapinzani kwa kutoa mawazo yao?

In God we trust
 
Ni sawa kabisa ndio maana misamiati ifuatayo si lugha za kuudhi "MALOFA WAPUMBAVU... VILAZA... MATUMBILI... WAKALALIE NA WAKE ZAO... NK."
Au Katiba inaangalia upande mmoja TUVUMILIANE TU MAANA WATANZANIA HATUPIGANI KWA MAKONDE BALI MANENO!!
 
N

Rafiki unaonekana kazi ya kufikiri umemuachia Lisu to an extent kwamba kila anachoongea unapigia makofi,,,Rekebisha kiswahili chako kwanza ndio urudi hapa ''lugha ya kuuzi=lugha ya kuudhi''
Umesha laaniwa

In God we trust
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…