Katiba mbovu, sheria mbovu, mikataba mibovu. Leo tumetozwa zaidi ya Tsh. Bilioni 260. Kufanywa kichwa cha Mwendawazimu hadi lini?

Katiba mbovu, sheria mbovu, mikataba mibovu. Leo tumetozwa zaidi ya Tsh. Bilioni 260. Kufanywa kichwa cha Mwendawazimu hadi lini?

Bwana Mayala: haya yooooote unaweza kuyasema kwa neno moja: RULE OF LAW, i mean maneno matatu.

Sheria ya zamani ilikuwa na RETENTION LICENSE, yaani wakati unachimbachimba kutafuta dhahabu ulipewa miaka 5, unachukua RETENTION LICENSE kwa miaka mingine mitano ujaribu tena. Usipopata ndiyo basi. Huyu alikuwa na haki zote, kafanya kama ilivyotakiwa na sheria, kaja mtu mmoja akamnyanganya eneo lake, just like that. Huo si uzalendo, ni uvunjifu wa sheria tu.

Inawezekana huyo ndiyo alikuwa na maslahi yake binafsi, aulizwe - hii haihotaji tumehuru. Rais yuko Magogoni machimbo tako Makongolosi Chunya, atajuaje? Ni huo ushauri mbovu, si katiba mpya. Nakumbuka wote mlishangilia hiyo sheria isiyo sheria ilipopitishwa uweje sasa mnatupa crocodile tears?

Kuna wazalendu uchwara hawajui kama na wenzao nao ni wazalendo kwa nchi zao. Bomba la Mafuta linatoka Uganda ni maliasili yao watataka watumie sheria za Uganda.

Bomba linapita Katoma na Ng'wakitolyo hadi Chumbageni Tanga hiyo ni Nji yetu turataka tutumie sheria yetu. Nani ashinde? Nani ashindwe? Ndiyo maana wapuuzi kina Shivji Marxist na Slaa Msaliti wanagangania tutumie Jaji wa Kisutu wakati Mwarabu naye HELA zake ni mali ya Mfalme wake.

Katika hali hii tunatumia Geneva Convention inayotaka muende kwenye Nchi ya tatu lakini hawa wapumbavu hawataki kusikiliza. Mimi nakushauri soma Ilani ya CUF ilisemaje kuhusu bandari na ya CHADEMA halafu linganisha na ta CCM.

Mwaka 2020 ni ilani ya CCM ndiyo iliyoshinda, waachwe waitekeleze. Wananchi tusiyumbishwe na Wasaliti na mafisadi katika maisha yao.
Kaka Mayala umeandika mambo kwa uzalendo mkubwa sana. Lakini nimepata shida kutafsiri uzalendo wako maana umekuwa ukibadilika badilika kulingana na upepo, hiyo hali sijaipenda. Amua moja kaka. Hapa duniani tunaishi mara moja tuuu
 
Mimi nazungumzia mbuzi wewe unasema kuku Sidhani kama umenielewa kwa hiyo endelea na mindset yako it’s your prerogative
Nadhani kama ambavyoRasbamba na Mayor Quimby mlivyoshindwa kuelewana hata hao wataalamu wetu kwenye mikataba huwa wanashindwa kuelewana na mwisho wa siku wanatumbukia kwenye mikataba nyonya damu !!

Sasa ni muda muafaka wa kutafuta wataalamu kutoka Umoja wa mataifa au kokote duniani ili tusaidiwe tusiingie kwenye mikataba nyonya damu tena !!

Ndugu Paskali alipata kusema mtu akishindwa kufanya kitu ni lazima asaidiwe !!

Na mhe Tibaijuka naye kabla hajaingia kwenye politics alipata kusema huko UN kipo kitengo cha kusaidia Nchi zilizoingia kwenye mikataba kichwa kichwa bila kuielewa vizuri !!

Kama tumeshindwa ni muda muafaka tuombe tusaidiwe !!
 
Wanabodi,
Hizi kelele za wanasheria manguli wabobezi na wabobevu kuhusu hii IGA ya DPW na Bandari zetu, sio za kuzipuuzia!. Katiba hii mbovu tuliyonayo!, Sheria zetu mbovu tuliyonayo, mikataba mibovu ya kimataifa tunayoingia, mwisho wa siku tunajikuta tumepigwa!, tunafunguliwa mashitaka, tunashindwa, tunapigwa tozo za mabilioni ya fedha!, ambazo ni lazima tulipe.

Haya yote ni matokeo ya kazi ya wanasheria wabovu na baadhi yao vilaza!. Leo nimeianza siku kwa bad news kutoka Marekani, Tanzania tumeshindwa kesi, tunadaiwa tozo ya dola za Marekani zaidi ya Millioni 100!, na lazima tulipe!.

Soma taarifa hii hapa chini
View attachment 2692021
  1. Kama Tanzania tulipitisha sheria kuwa kwenye uwekezaji hakuna mashauri yoyote ya nje ya nchi!. Mashauri yote ni hapa nchini kutumia sheria za Tanzania!, sasa haya mashauri yanaendelea vipi kupelekwa nje?.
  2. Hii maana yake ni ama tuna sheria mbovu, ama tuna wanasheria wabovu wanaotunga sheria mbovu, zinazotupa mikataba mibovu, na mwisho wa siku tunaishia kupigwa na kutozwa matozo ya ajabu ajabu!.
  3. Huku kila siku kushindwa kesi za kimataifa na kupigwa tozo nako ni ama tuna sheria mbovu za mikataba mibovu ama kama sheria ni nzuri, then tuna wanasheria wabovu wasio na uwezo wa kushauri the right thing to do!, hivyo serikali yetu inavunja mikataba kitutusa na mwisho wa siku tunaishia kuumizwa kwa kushindwa kesi na kupigwa tozo!.
  4. Kabla ya kuvunja mkataba wowote, serikali yetu inaomba ushauri wa kisheria kufanya kitu kinachoitwa mitigation, wanasheria hawa huishauri vibaya serikali yetu, mwisho wa siku, tunaishia kuumizwa!.
  5. Issues ya Richmond, Dowans, tukaunda tume, ikatoa matokeo kwa mbwembe kuwa Richmond ni kampuni hewa hata tukivunja mkataba, hatutashitakiwa popote!.
  6. Tukamfanya Edward Lowassa ni mbuzi wa kafara, tukavunja mkataba!.
  7. Tukashitakiwa tukashindwa, tukapigwa tozo!. Waliotushauri tuvunje mkataba wakajiapiza "over my dead body!, hatulipi". Tulilipa kisiri siri every cent!. Hawa wanasheria walifanywa nini?
  8. Mitambo ya Richmond ikanunuliwa na Simbion, tukaingia nao mkataba ule ule na tukawalipa!.
  9. Chuma JPM, alipoingia tukavunja mkataba wa Simbion, tukashitakiwa, tukashindwa, tukapigwa tozo, Chuma JPM, akagoma hatulipi!
  10. Mama kaingia, tumelipa fasta fasta, kimya kimya!. Wanasheria waliotufikisha hapa walifanywa nini?!.
  11. Tulipotunga sheria mbovu, watu humu tulishauri Zita Act Retroactively? Tutavunja Mikataba Yote Iliyopo? Can we Stand? Do we have the Guts?, leo baada ya kutuletea hii IGA mbovu, watu tumeeleza matatizo yake kibao!.
  12. Wanasheria hawa hawa, Bunge letu hili hili wanaipitisha hivyo hivyo ilivyo, wanaiambia serikali yetu hii IGA ni nzuri, safi na haina matatizo yoyote!.
  13. Wanasheria hawa wanao tufikisha hapa, tukiwaita ni wanasheria wabovu au vilaza, itakuwa ni kuwaonea?.
  14. Tanzania tutaendelea kufanywa shamba la bibi na kichwa cha Mwendawazimu na wanasheria wabovu na vilaza wa aina hii hadi lini?!.
Mungu ibariki Tanzania
Paskali
We ngoja tu kunasiku tutakulupua ofisini mwao wakae gerezani.
 
Ndio shida ilipo ya kujibizana na watu ambao wanasoma sheria lakini awaelewi hayo mambo in principal.

BIT ina breach ‘clause’ how is that even possible. Inaonekana hujui ata breach ni kitu gani. Just because umeona neno breach kwenye treaty doesn’t equate its definitive in future contracts.

You can’t have a definitive ‘breach in a contract’ bila ya kuwa na consideration na wala performance agreement.

Consideration na performance ni mambo ambayo utayakuta kwenye mkataba wa utekelezaji; lakini ni vitu ambavyo uwezi kukuta kwenye BIT yeyote duniani.

Unapovunja makubaliano ya performance ndio breach inatokea. Na breach zote sio sawa kuna ‘conditional breach terms’ ni serious which could lead to fines and termination of a contract if the claimant chooses to do so. Whereas ‘warranty terms’ ni less serious not enough to terminate a contract but could lead to paying compensation or imposing forms of sanctions.

Kuna ‘innominate terms’ hizi ni zile ambazo ngumu kujua ni ‘conditional au warranty’ mahakama itaamua baada ya kuelewa msingi wa mkataba wenyewe na performance agreements.

Hizo ni expressed terms huwa ni specific kwenye kila mkataba wa utekelezaji sio implied (aziwezi kuwa kwenye treaty yoyote) kwa sababu performance aziwezi fanana kwenye kila mkataba. Ndio maana hao wawekezaji hayo mambo wanataka yawe siri wanapoingia kwenye lease/concession agreements or any orher investment agreement like PSA and the likes.

BIT pekee ni sheria (after ratification) for the most part terms zake zinaelezea ni how to resolve issues when there is a dispute or in the event of breach; another item is the protection of investment against ‘frustrating events’ ambazo msingi wange ni mabadiliko ya kisheria. That’s pretty much what’s in the BIT, sasa hizo ni clauses ambazo ata usipoziweka kwenye specific concession agreement kwa sababu kuna sheria yake ya BIT zinaitwa implied terms and they’re enforceable part of future contract.

Ukitunga sheria ya kuchukua mali za watu kuna BIT inalinda against ‘frustrating events’ that when it becomes enforceable kwa sababu performance pia ina muda (provided bado muda aujaisha that’s a conditional breach).
Shida ni unaposema BIT ni mkataba kwangu it’s a Treaty between nations and mkataba contract between two parties for a particular business could be state or individual’s and is subject to the Treaty’s basta
 
Hizi kesi niz fedha nyingi zinahitaji uzalendo na uqdilifu mkubwa hasq kukiwa na uhakika wa kulipwa!
 
Shida ni unaposema BIT ni mkataba kwangu it’s a Treaty between nations and mkataba contract between two parties for a particular business could be state or individual’s and is subject to the Treaty’s basta
Kiswahili kina shortage of ‘vocabulary’, but then I had just explained from the post you quoted a BIT doesn’t have key terms which forms a ‘contract’ therefore it’s beyond me even tacitly how you came to that conclusion.

Unaposoma post za wenzako jaribu kun’gamua kilichoandikwa sio kutafsiri vitu ambavyo havipo na kuweka maana zako.

Ukiweza kujua aina ya terms tofauti zinazowekwa kwenye hizo unazoita ‘contracts’ ndio utaelewa how a BIT fits in; hint nimeshakueleza several times including the post you quoted some of its articles (from a BIT) are part of implied terms in future contracts.

👋
 
Katika hili Paskali ameamua liwalo na liwe na hajadeclare interest kama ilivyo kawaida yake. Kwa kweli ni mambo ya kusikitisha kwamba kesi zinafanyika nje na huko tunashindwa pamoja na kuwa kwenye mikataba inaelezwa wazi kwamba matatizo yanayoweza kujitokeza yatasuluhishwa ndani ya nchi. Kuna kesi ziliamliwa hapa nchini ambapo maamuzi yalikuwa upande wetu. Baadae zikapelekwa kwenye International Court of Arbitration huko tukakwaa kisiki na kuamliwa kulipa. Nafikia mahali naona kuna mapungufu katika kuandaa mikataba. Wanasheria wetu bado tupo mbali Sana. Tukapeleka Maprofesa wa Sheria kwenye lile sakata la Makinikia, kilichojitokeza ni kinyume kabisa na matarajio ya wengi. Hatuna budi kujifunza toka katika makosa ya awali ili kuweza kufanya vizuri huko mbele. Vinginevyo wajanja wataendelea kuvuna bila jasho toka kwetu.
 
Wanabodi,
Hizi kelele za wanasheria manguli wabobezi na wabobevu kuhusu hii IGA ya DPW na Bandari zetu, sio za kuzipuuzia!. Katiba hii mbovu tuliyonayo!, Sheria zetu mbovu tuliyonayo, mikataba mibovu ya kimataifa tunayoingia, mwisho wa siku tunajikuta tumepigwa!, tunafunguliwa mashitaka, tunashindwa, tunapigwa tozo za mabilioni ya fedha!, ambazo ni lazima tulipe.

Haya yote ni matokeo ya kazi ya wanasheria wabovu na baadhi yao vilaza!. Leo nimeianza siku kwa bad news kutoka Marekani, Tanzania tumeshindwa kesi, tunadaiwa tozo ya dola za Marekani zaidi ya Millioni 100!, na lazima tulipe!.

Mungu ibariki Tanzania
Paskali
Ukiacha kutetea DP world tutakuunga mkono
Mkuu JakiDubai, kuna watu wanaandika jf ili waungwe mkono?, utaniunga mkono ili iweje?.
Anyway karibu, hili ni moja ya mabandiko yangu kuunga mkono IGA ya DPW na Bandari zetu, angalia tuu tarehe ya bandiko hili ili ulinganishe na wengine, na ikitokea una uwezo wa kusoma contents, soma contents uone jinsi ninavyoisupport DPW na Bandari zetu!.

Karibu

P
 
Bwana Mayala: haya yooooote unaweza kuyasema kwa neno moja: RULE OF LAW, i mean maneno matatu.

Sheria ya zamani ilikuwa na RETENTION LICENSE, yaani wakati unachimbachimba kutafuta dhahabu ulipewa miaka 5, unachukua RETENTION LICENSE kwa miaka mingine mitano ujaribu tena. Usipopata ndiyo basi. Huyu alikuwa na haki zote, kafanya kama ilivyotakiwa na sheria, kaja mtu mmoja akamnyanganya eneo lake, just like that. Huo si uzalendo, ni uvunjifu wa sheria tu.

Inawezekana huyo ndiyo alikuwa na maslahi yake binafsi, aulizwe - hii haihotaji tumehuru. Rais yuko Magogoni machimbo tako Makongolosi Chunya, atajuaje? Ni huo ushauri mbovu, si katiba mpya. Nakumbuka wote mlishangilia hiyo sheria isiyo sheria ilipopitishwa uweje sasa mnatupa crocodile tears?

Kuna wazalendu uchwara hawajui kama na wenzao nao ni wazalendo kwa nchi zao. Bomba la Mafuta linatoka Uganda ni maliasili yao watataka watumie sheria za Uganda.

Bomba linapita Katoma na Ng'wakitolyo hadi Chumbageni Tanga hiyo ni Nji yetu turataka tutumie sheria yetu. Nani ashinde? Nani ashindwe? Ndiyo maana wapuuzi kina Shivji Marxist na Slaa Msaliti wanagangania tutumie Jaji wa Kisutu wakati Mwarabu naye HELA zake ni mali ya Mfalme wake.

Katika hali hii tunatumia Geneva Convention inayotaka muende kwenye Nchi ya tatu lakini hawa wapumbavu hawataki kusikiliza. Mimi nakushauri soma Ilani ya CUF ilisemaje kuhusu bandari na ya CHADEMA halafu linganisha na ta CCM.

Mwaka 2020 ni ilani ya CCM ndiyo iliyoshinda, waachwe waitekeleze. Wananchi tusiyumbishwe na Wasaliti na mafisadi katika maisha yao.
Hivi Ng'wakitolyo maana yake nini?
 
Back
Top Bottom