Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Mara ya ngapi tenaKuna wakati tutaoshuhudia nchi inauzwa na hatuna cha kwetu tena.
Madini siku zote yalikuwepo na mali ya Tanzania.Hayo madini ndio yamepata thamani sasa kabla ya hapo yalikuwa bado kwa hiyo huwezi kuja kimfukuza yule alikuwepo zamani kwa sababu sasa hiyo madini yanahitajika ni kama vile umnyanganye mtu ardhi kwa sababu hajajenga gorofa pale chole road baada ya kumuacha auze anufaike na mali yake. Kwani nani kawekeza sasa kwenye hiyo migodi huyo alipe??
Wangempa nafasi ya kufanya alichotaka wote wangefaidika By the way UK Tanzania BIT haijaexpire soma vizuri uelewe 1996 plus 30yrs and if you don’t the treaty it’s automatically going onMadini siku zote yalikuwepo na mali ya Tanzania.
Mkataba wake yeye mwekezaji ni kufanya exploration, kuyatoa, kugawana mapato na serikali mpaka hela yake irudi, kulipa kodi ya faida, PAYE na kadhalika.
So performance wise had the contract been executed serikali ingepata mapato yote hayo. Mwekezaji ajafanya chochote mpaka muda wa expropriation, na muda wake wa awali uli expire 2015 akaongezewa haraka haraka. I don’t know how they manage to loose these cases.
Anyway wenyewe kwa wenyewe washaanza kugeukana kuna nyingine ya mgogoro baina ya wabia nani anamiliki nini; baada ya kuona kuna mgao Ntaka Limited wamefungua kesi kudai share zaidi. So hata hao wazawa waliosuka huo mpango washapigwa na wazungu.
Mtu makini ni Magufuli?? Mbona yeye ndio aliesababisha matatizo yote haya. Kesi ziko nyingi na zinakuja kwa hiyo umdhaniae ndie sio matatizo haya ni ya Magufuli tuwe wakweliLabda uweke hiyo link inayoonyesha serikali walitokea kwenye arbitration.
Decision niliyoona mimi Tanzania aija respond kwenye hayo madai ya Indiana.
Ila wana siku 120 za kutoa pingamizi toka tarehe ya maamuzi bila ya kufanya hivyo zikipita hizo siku hayo maamuzi ni enforceable.
Ni hivi kama na wewe ni sehemu ya wanufaikaji ni muda wa kuambizana inatosha na kumwambia huyo mama airudishe nchi alipoikuta 2021 na kufungasha virago 2025.
Kabla ya kufungusha atuwekee mtu sahihi anaeweza kasi ya 2015-2021 ameifanya nchi imerudi kuwa ya ovyo sana ndani ya muda mfupi.
Nitakiachia niliyoachiwa na waliopita hasa baada ya kuelewa kuwa Tanzania life is about connection.Kama kuna wengi kama wewe wanafikiri hivyo ulivyosema basi Tanzania ina shida kubwa ya raslimali watu na inaelekea ni umekata tamaa ya maisha je kizazi chako utakiachia nini??
True datNitakiachia niliyoachiwa na waliopita hasa baada ya kuelewa kuwa Tanzania life is about connection.
Kama huna koneksheni usithubutu kuwekeza Tanzania na kama ni foreigners wataishia arbitration ambazo ziko nyingi mno kuhusu Tanzania nina wasiwasi Tanzania inawezekana kuwa ni nchi ya kwanza kuwa na migogoro mingi sana katika mahakama za kimataifaNitakiachia niliyoachiwa na waliopita hasa baada ya kuelewa kuwa Tanzania life is about connection.
Upewi nafasi forever kuna terms za uwekezaji ukishindwa unanyan’ganywa. ‘Performance’ ni sehemu kubwa ya mkataba ukishindwa kuna madhara.Wangempa nafasi ya kufanya alichotaka wote wangefaidika By the way UK Tanzania BIT haijaexpire soma vizuri uelewe 1996 plus 30yrs and if you don’t the treaty it’s automatically going on
Mbona awakuzifungia hizo kesi wakati uhai wake.Mtu makini ni Magufuli?? Mbona yeye ndio aliesababisha matatizo yote haya. Kesi ziko nyingi na zinakuja kwa hiyo umdhaniae ndie sio matatizo haya ni ya Magufuli tuwe wakweli
Jifunze jinsi kesi za kimataifa BIT zinavyofunguluwa kwanza unafanya diplomatic ubalozi wa mfungua kesi unaijulisha Tanzania kwamba tuna tatizo mwananchi wetu anadhulumiwa kwa hiyo rekebisha miezi 6 Tanzania wasipojibu wanaandaa mchakato wa kesi na unweza chukua mwaka mzima kama Tanzania hawatoi ushirikiano kesi kama hizo ni miaka 2 au 4 mpaka ziisheMbona awakuzifungia hizo kesi wakati uhai wake.
Yeye alikuwa ana malizana tu na hiyo michezo; watanzania tulimpenda ila mungu akampenda zaidi kabla kazi yake aijaisha. Team yake yote wameitoa kwenye civil services kwa asilimia kubwa wamerudisha majizi na mambo ya hovyo yamerudi upya.
It’s still in force haijakuwa terminated!!Upewi nafasi forever kuna terms za uwekezaji ukishindwa unanyan’ganywa. ‘Performance’ ni sehemu kubwa ya mkataba ukishindwa kuna madhara.
Wote hao waliopo mahakamani didn’t meet their part of the performance obligations, kuendelea na hiyo mikataba serikali ilitakiwa iwatoze loss of income au yenyewe ndio iwafungulie case za conditional (material) breach kudai fidia na kuvunja mkataba juu.
BIT ya Tanzania na U.K. ilisainiwa 1994 with 10 years duration kwa hivyo ili expire 2004. Hiyo miaka 20 ya sunset clause inalinda investment zilizofanyika ndani ya 10 years ambazo bado zinaendelea after 2004. Not anything entered after 2004 those are not covered.
Kulipa hizo hela either kuna incompetence serikalini au ni deal za watu; I pick the latter.
It’s still in force haijakuwa terminated!! 1994 but in force 1996 started 10ths 2006 plus 20 Yrs is 2026 please 🙏🏿 get your arithmetic code rightUpewi nafasi forever kuna terms za uwekezaji ukishindwa unanyan’ganywa. ‘Performance’ ni sehemu kubwa ya mkataba ukishindwa kuna madhara.
Wote hao waliopo mahakamani didn’t meet their part of the performance obligations, kuendelea na hiyo mikataba serikali ilitakiwa iwatoze loss of income au yenyewe ndio iwafungulie case za conditional (material) breach kudai fidia na kuvunja mkataba juu.
BIT ya Tanzania na U.K. ilisainiwa 1994 with 10 years duration kwa hivyo ili expire 2004. Hiyo miaka 20 ya sunset clause inalinda investment zilizofanyika ndani ya 10 years ambazo bado zinaendelea after 2004. Not anything entered after 2004 those are not covered.
Kulipa hizo hela either kuna incompetence serikalini au ni deal za watu; I pick the latter.
It’s still in force haijakuwa terminated!! 1994 but in force 1996 started 10ths 2006 plus 20 Yrs is 2026 please 🙏🏿 get your arithmetic code right
Huo sio utaratibu wa kimataifa ni recommended dispute resolution process kuanza diplomatically before escalating to tribunals.Jifunze jinsi kesi za kimataifa BIT zinavyofunguluwa kwanza unafanya diplomatic ubalozi wa mfungua kesi unaijulisha Tanzania kwamba tuna tatizo mwananchi wetu anadhulumiwa kwa hiyo rekebisha miezi 6 Tanzania wasipojibu wanaandaa mchakato wa kesi na unweza chukua mwaka mzima kama Tanzania hawatoi ushirikiano kesi kama hizo ni miaka 2 au 4 mpaka ziishe
Tatizo ni mianasheria yetu mimbumbumbu mila rushwa haina uzalendo, hiko localised haina International exposure! Hiyo kesi naifahamu vizuri Tanzania hatupaswi kulipa hata senti tano. Hizi kesi zinaendeshwa na madalali ya kimataifa baada ya kugundua kwasasa tuna rais mbumbumbu asiyejua kitu kutokana na kusaini mkataba wa DP WORLD! Kwahiyo hao madalali wananunua kesi za kimataifa na kutumia loopholes za udhaifu wa Tanzania kutupiga! Ndugu watanzania, maisha magumu tuliyonaya yanasababishwa na seriakaliWanabodi,
Hizi kelele za wanasheria manguli wabobezi na wabobevu kuhusu hii IGA ya DPW na Bandari zetu, sio za kuzipuuzia!. Katiba hii mbovu tuliyonayo!, Sheria zetu mbovu tuliyonayo, mikataba mibovu ya kimataifa tunayoingia, mwisho wa siku tunajikuta tumepigwa!, tunafunguliwa mashitaka, tunashindwa, tunapigwa tozo za mabilioni ya fedha!, ambazo ni lazima tulipe.
Haya yote ni matokeo ya kazi ya wanasheria wabovu na baadhi yao vilaza!. Leo nimeianza siku kwa bad news kutoka Marekani, Tanzania tumeshindwa kesi, tunadaiwa tozo ya dola za Marekani zaidi ya Millioni 100!, na lazima tulipe!.
Soma taarifa hii hapa chini
View attachment 2692021
Mungu ibariki Tanzania
- Kama Tanzania tulipitisha sheria kuwa kwenye uwekezaji hakuna mashauri yoyote ya nje ya nchi!. Mashauri yote ni hapa nchini kutumia sheria za Tanzania!, sasa haya mashauri yanaendelea vipi kupelekwa nje?.
- Hii maana yake ni ama tuna sheria mbovu, ama tuna wanasheria wabovu wanaotunga sheria mbovu, zinazotupa mikataba mibovu, na mwisho wa siku tunaishia kupigwa na kutozwa matozo ya ajabu ajabu!.
- Huku kila siku kushindwa kesi za kimataifa na kupigwa tozo nako ni ama tuna sheria mbovu za mikataba mibovu ama kama sheria ni nzuri, then tuna wanasheria wabovu wasio na uwezo wa kushauri the right thing to do!, hivyo serikali yetu inavunja mikataba kitutusa na mwisho wa siku tunaishia kuumizwa kwa kushindwa kesi na kupigwa tozo!.
- Kabla ya kuvunja mkataba wowote, serikali yetu inaomba ushauri wa kisheria kufanya kitu kinachoitwa mitigation, wanasheria hawa huishauri vibaya serikali yetu, mwisho wa siku, tunaishia kuumizwa!.
- Issues ya Richmond, Dowans, tukaunda tume, ikatoa matokeo kwa mbwembe kuwa Richmond ni kampuni hewa hata tukivunja mkataba, hatutashitakiwa popote!.
- Tukamfanya Edward Lowassa ni mbuzi wa kafara, tukavunja mkataba!.
- Tukashitakiwa tukashindwa, tukapigwa tozo!. Waliotushauri tuvunje mkataba wakajiapiza "over my dead body!, hatulipi". Tulilipa kisiri siri every cent!. Hawa wanasheria walifanywa nini?
- Mitambo ya Richmond ikanunuliwa na Simbion, tukaingia nao mkataba ule ule na tukawalipa!.
- Chuma JPM, alipoingia tukavunja mkataba wa Simbion, tukashitakiwa, tukashindwa, tukapigwa tozo, Chuma JPM, akagoma hatulipi!
- Mama kaingia, tumelipa fasta fasta, kimya kimya!. Wanasheria waliotufikisha hapa walifanywa nini?!.
- Tulipotunga sheria mbovu, watu humu tulishauri Zita Act Retroactively? Tutavunja Mikataba Yote Iliyopo? Can we Stand? Do we have the Guts?, leo baada ya kutuletea hii IGA mbovu, watu tumeeleza matatizo yake kibao!.
- Wanasheria hawa hawa, Bunge letu hili hili wanaipitisha hivyo hivyo ilivyo, wanaiambia serikali yetu hii IGA ni nzuri, safi na haina matatizo yoyote!.
- Wanasheria hawa wanao tufikisha hapa, tukiwaita ni wanasheria wabovu au vilaza, itakuwa ni kuwaonea?.
- Tanzania tutaendelea kufanywa shamba la bibi na kichwa cha Mwendawazimu na wanasheria wabovu na vilaza wa aina hii hadi lini?!.
Paskali