Katiba mbovu, sheria mbovu, mikataba mibovu. Leo tumetozwa zaidi ya Tsh. Bilioni 260. Kufanywa kichwa cha Mwendawazimu hadi lini?

Katiba mbovu, sheria mbovu, mikataba mibovu. Leo tumetozwa zaidi ya Tsh. Bilioni 260. Kufanywa kichwa cha Mwendawazimu hadi lini?

Wanabodi,
Hizi kelele za wanasheria manguli wabobezi na wabobevu kuhusu hii IGA ya DPW na Bandari zetu, sio za kuzipuuzia!. Katiba hii mbovu tuliyonayo!, Sheria zetu mbovu tuliyonayo, mikataba mibovu ya kimataifa tunayoingia, mwisho wa siku tunajikuta tumepigwa!, tunafunguliwa mashitaka, tunashindwa, tunapigwa tozo za mabilioni ya fedha!, ambazo ni lazim
Wewe ulikuwa mtu wa kusifia kila kitu cha awamu iliyopita.
Leo walalamika?.
 
Wanabodi,
Hizi kelele za wanasheria manguli wabobezi na wabobevu kuhusu hii IGA ya DPW na Bandari zetu, sio za kuzipuuzia!. Katiba hii mbovu tuliyonayo!, Sheria zetu mbovu tuliyonayo, mikataba mibovu ya kimataifa tunayoingia, mwisho wa siku tunajikuta tumepigwa!, tunafunguliwa mashitaka, tunashindwa, tunapigwa tozo za mabilioni ya fedha!, ambazo ni lazima
Paskali
Nikuishinikiza serekali ya chadema imeshindwa ijiuzulu iingie serekali mpya ya ccm.
 
Walau leo umevua miwani yako ile ya kijani,inyochuja mambo na kuruhusu yale yanayofanana na wale jamaa wavaa kijani kupita.Umeandika uhalisia.Hongera.
Pamoja na nchi yetu kugeuzwa shamba la bibi,Bado viongozi wa CCM na serikali yao wamekumbatia mkataba ambao Kila sentesi yake inampendelea DP WORLD .Serikali imetumia nguvu kuutetea,kutisha waoupinga,kulipa machawa wautetee.CCM Imetumia vijana wao kudhoofisha nguvu za wazalendo.Yote haya yanafanyika ili mwarabu apewe bandari,ili baadaye akija mzalendo mwingine madarakani ,auvunje huo mkataba,tushitakiwe na mwisho tuwalipe DP WORLD.
 
Taasisi pekee inayoweza kuibwekea serikali na ikamtii ni CCM.

Na kwa kuwa Serikali ndiyo CCM, basi kama nchi tuna hasara ya kuwa na Chama cha Hovyo cha CCM.

Chama kikiwa cha hovyo hata Wanachama wake ni wa HOVYO. Paskali ukiwepo.

Nawe ni wa Hovyo.
Mtu ambaye siyo hovyo hawezi kuwa CCM. Labda awe lake jambo.
 
Mpigwe tu maana hamna namna , mlidhani wale waliokuwa wanatetea mkataba hadi mimacho inawatoka walikua wanatetea bure? walishalamba chao mapemaa, kimsingi walishalambishwa asali hao, nilishangaa sana hata lile zuzu la Jukwaa la wahariri linaitwa balile nalo lilienda TBC kubwabwaja na kutoa mipovu kwenye mic , kwa kweli mzalendo mwenye njaa hayupo hata mmoja. #NJAA MBAYA SANA.
 
kama lengo la kumleta dp world ni kuondoa utendaji mbovu na kuongeza ufanisi, basi serikali n mihimili yake mitatu panahitaji wawekezaji waje kututolea utendaji wa hovyo, wa kimazoea na wakifisadi ili kuwa na serikali fanisi na tajiri kama aliyoiita baba wa taifa.

haya makosa yamefanywa na eti wasomi na viongozi wa nchi hii, rubbish kwa sauti ya lisu
 
Shida kubwa sio sheria zetu wala BIT tunazoingia.

Shida kubwa zipo huko wanapoingia mikataba ya kibiashara on expressed terms.

Hata bila ya kuona hiyo mikataba yenyewe logically kutokana na mazingira yenyewe ya utaifishwaji kuna matatizo mawili makuu kwenye expressed terms za mikataba waliyokuwa wana sign inavyoonekana.

(i) sidhani kama walikuwa wanaweka clear definition ya performance terms kwa muwekezaji, wao walikuwa wanawapa tu maeneo bila ya kujali muda au kipimo cha kazi kuendelea kuyakalia.
(ii) kwa kuwa hakuna definition ya perfomance na muda wa kuanza uzalishaji. Hata definition za breach terms kama ‘condition, warranty and innominate’ hazipo; ili wachukue hatua sahihi.

Vinginevyo aingii akilini mtu atelekeze eneo halafu serikali ichukue na bado ishindwe kesi.
 
Tunaingia mikataba ya kijinga, mwisho wa siku tunagundua ni ya kijinga wakati tushajitia kitanzi, tukijaribu kujitoa ndio wanatushitaki na kushinda mabilioni.

Inejirudia tena na tena. Angalau mwamba JPM aliona mikataba hii mibovu inatokana na usiri wake, watu wanapelekwa nje huko kupetiwa petiwa kisha wanasaini tu. Akaamua kuleta sheria ya kulinda rasilimali za nchi na kuweka uwazi kwenye hiyo mikataba.

Leo hii watu wanakwenda above and beyond kutaka kurudia ujinga na upumbavu uleule wa mikataba ya kijinga, wako tayari hata kuibadilisha ile sheria iliyowekwa ili kuinusuru nchi ili mradi upumbavu waliousaini upite.

Mtu asiyeweza kujifunza ni MPUMBAVU! Tumekuwa taifa la kipumbavu, kichwa cha mwendawazimu. Wahuni wanajipigia tu.
 
Hivi ikikamatwa ndege huko mimi naathirikaje?
Hivi wakilipa hela hizi mimi naathirikaje?
Mbona naona kama wakilipa hela sipungukiwi kitu na hata tungeshinda kesi siongezewi kitu! Try & error; hivi nchi yote ikiuzwa tutapungukiwa nini sisi raia zaidi ya wale watakaopoteza vyeo vyao?
 
Back
Top Bottom