Katiba Mpya impe Nguvu Rais, aendelee Mpaka aseme "BASI" mwenyewe

Jamani watanzania msameheni bure na huyu hajui anachokiongea. huyu ndio wale vitabu vya dini vinawaita wapumbavu, silaha ya mjinga ni kujipendekeza.
 
Utashangaa CHADEMA wanapinga na kuona wivu. Maana akili zao wanazijua wao wenyewe
hao wamepuuzwa kila mahali nchini na hakuna mahali wanaeleweka wala kukubalika kwa wananchi.

umadhubuti wa uongozi wa kipenzi cha waTanzania wote Dr. Samia Suluhu Hassan ndio habari ya kitaifa na kimataifa Tanzania kwa sasa kuelekea uchaguzi mkuu wa october
 
Uchaguzi upo palepale na utafanyika kama ilivyopangwa na watanzania wote watashiriki kikamilifu kabisa kumchagua Rais Samia na viongozi wengine mbalimbali wa ubunge na udiwani kupitia CCM
Kwani ni lazima Samia achaguliwe? Kwa Taarifa yako Samia hatagombea CCM ina watu wengi mno ,Haiko Tayari kumrudisha muuaji na mtekaji Ikulu
 
Acheni kujitekenya na kujichekesha. Hata Lissu alikuwa anaropoka ropoka Hovyo na kujiona hagusiki. Lakini leo yupo ndani Amesahaulika kabisa na hakumbukwi na yeyote yule
 
Anzeni mchakato kesho ,bunge bado lipo, mnachelewa nini sasa
 
Hata kwa JPM walisema hivyo na Mungu akafanya yake. Chunga ulimi wake ponjoro mkubwa wewe.
 
Nikiwa Mtanzania mzalendo, ninatoa rai kwa Watanzania wenzangu, hasa tunapoelekea kwenye mchakato wa katiba mpya, kuufikiria kwa uzito uwezekano wa kuweka kipengele kitakachompa nafasi Rais Samia Suluhu Hassan kuendelea kuliongoza taifa hili.

Sio kwa mapenzi binafsi wala ushabiki wa kisiasa, bali kwa sababu ya kazi kubwa, ya kihistoria, na yenye matokeo makubwa aliyoifanya kwa muda mfupi wa uongozi wake.

Tangu aingie madarakani mwaka 2021, Mama Samia amekuwa chachu ya mageuzi ya kweli katika kila sekta muhimu.

Amefungua nchi kidiplomasia kupitia ziara zake za kimkakati nje ya nchi, hatua ambayo imeirudisha Tanzania kwenye ramani ya majadiliano ya kimataifa na kuiwezesha kuvutia wawekezaji wakubwa. Mfano halisi ni ujio wa kampuni kama DP World, inayowekeza kwenye uboreshaji wa bandari na miundombinu ya usafirishaji.

Katika sekta ya afya, Rais Samia amesimamia ujenzi wa zaidi ya hospitali 300, kuanzia ngazi ya zahanati hadi hospitali za wilaya, sambamba na kuhakikisha zina vifaa na watumishi wa kutosha. Wananchi wengi sasa wanapata huduma bora karibu na makazi yao, jambo lililokuwa changamoto kwa miaka mingi.

Sekta ya elimu imepata msukumo mpya chini ya uongozi wake. Kuondolewa kwa ada kwa wanafunzi hadi kidato cha sita kumeongeza idadi ya wanaojiunga na kumaliza elimu ya sekondari, hasa kwa mabinti waliokuwa wakikumbwa na changamoto za kifamilia na kiuchumi.

Kilimo pia kimepata sura mpya kupitia mpango wa Building a Better Tomorrow (BBT). Mama Samia amewekeza kwa vijana na wanawake kwa kuwapa mafunzo, ardhi, mitaji na masoko. Vilevile, ruzuku ya pembejeo imeongezwa, hali iliyochochea uzalishaji na kuongeza kipato cha wakulima vijijini.

Kwa kipindi kifupi tu, Rais Samia ameonesha kuwa ana maono, uthubutu na dhamira ya dhati ya kuipeleka Tanzania mbele kwa kasi na kwa umoja.

Sauti yake ni sauti ya mshikamano, maelewano na maendeleo.

Ametuonesha kuwa inawezekana kuwa na kiongozi mwanamke mwenye dira na weledi wa hali ya juu.

Kwa msingi huu, ni wakati sasa Watanzania wazalendo kutomruhusu Rais Samia aondoke wakati bado anahitajika.

Katiba mpya impe nguvu Mama, aendelee mpaka aseme “basi mwenyewe,” kwa sababu taifa bado linamhitaji.
 
Hata kwa JPM walisema hivyo na Mungu akafanya yake. Chunga ulimi wake ponjoro mkubwa wewe.
Rais Samia ni Mpango wa Mungu Mwenyewe kuliongoza Taifa letu Ameinuliwa kwa mkono wa Mungu na atalindwa kwa mkono hodari wa Mungu Mwenyewe
 
No Reforms, No Elections.
Wakulima bado wanalia huko mitaani, hizo pesa zinaishia kwenye matumbo yenu. Machawa kama wewe mwisho wenu umekaribia
 
Wewe jifanye kushupaza shingo na uendelee na huo upuuzi wako. Wewe na wenzako wenye mambo ya hovyo, mnamwaga uharo mitandaoni, halafu mnatupa shida ya kusafisha uchafu wenu.
No reforms no election
 
Mpuuzeni huyu, akili hana anachojua ni uchawa tuu kwa watu hata wasiomjua
 
Usisahau pia na idadi ya waliotekwa imeongezeka sana
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…