Katiba mpya imuongezee Dr. Samia Suluhu walau miaka minne 4 ya ziada ili asimamie utekelezaji wake kabla ya Rais mpya kuingia madarakani

Katiba mpya imuongezee Dr. Samia Suluhu walau miaka minne 4 ya ziada ili asimamie utekelezaji wake kabla ya Rais mpya kuingia madarakani

Kabla ya hata kuufikiria uamuzi huo, tathimini ya kina ifanyike ili ipate kuthibitika ya kwamba uongozi wake ni ASSET ama LIABILITY kwa Taifa letu..

Angalizo tu kutoka katika Maandiko Matakatifu lipate kuzingatiwa, ameua na kutamalaki. Vipi kuhusu suala la vijana wanaohisiwa na watawala kuwa ni watovu wa adabu, pale wanapo hoji mambo ya msingi itawapasa kucharazwa mikwaju katika kipindi hicho!?
Gentleman,
sote ni mashahidi kama Taifa,
na sidhani kama kuna mTanzania mzalendo asie mfuata mkumbo anaweza kukataa kwamba Dr.Samia Suluhu Hassan na uongozi wake wote, sio tu kwamba ni ASSETS bali pia ni LIABILITY kwa Taifa letu.

Nchi yetu inaongozwa kwa misingi ya kisheria, lakini pia kwa katiba ya nchi. Kwa wote wanaokosa ustaarabu na utii katika misingi hiyo, sheria hizo hizo za nchi huwanyorosha na kuwashikisha adabu.

Haipo ruhusa ya kukika sheria kwa kisingizio cha uhuru wa kutoa maoni ya kutukana wengine, kuzusha uongo au uichocheo fujo na vurugu na kuvuruga amani🐒
 
Damu inamlilia muda huu. she must pay back.
hizo ni ramli zinazowafaa ninyi washirikina pekeee gentleman.

Kama taifa, tunasonga mbele kwa pamoja kwa kasi ya mwendo wa ngiri bila mbambamba yoyote madarakani 🐒
 
Baadhi sio wote, usifikiri nchi hii wote ni wanachama wa chama fulani
wafuata mkumbo kwa hisani ya AZAKI hawana athari zozote kwenye mchakato wa kuelekea katiba mpya gentleman,

hakuna haja ya kubabaika nao,
CCM ni ya waTanzania wote 🐒
 
wafuata mkumbo kwa hisani ya AZAKI hawana athari zozote kwenye mchakato wa kuelekea katiba mpya gentleman,

hakuna haja ya kubabaika nao,
CCM ni ya waTanzania wote 🐒
Endelea kuota ndoto za mchana
 
Wengi wenu mmemuona Rais Samia kama rais wa JMT, baada ya kutokea kilichotokea, ila mimi nilimuona siku nyingi kabla Siku ya Wanawake Duniani: Je, tuna Wanawake wenye sifa za Presidential Material? Humo kuna kitu nilizungumzia kuhusu age

Hili la umri wa Dada Mkubwa, niliwahi kuandika humu kushauri PreGE2025 - Ukimuondoa Rais Samia, kama ni lazima awe mwanamke, then mwanamke huyo ni Dkt. Tulia, ameonesha uwezo, anaweza! Tumchagize au tuache tu bora liende?
P
ni kweli mwalimu Paskali,
wengi tumeanza kufuatilia siasa na wanasiasa wa Tanzania kuanzia kipindi kile cha RICHMOND, ESCROW na mgawa wa vijisenti na hela ya mboga kutoka EPA,

background za wanasiasa wengi wa Tanzania kiukweli hatunazo in deep na tulikua tukikushangaa tu hata wewe kwenye vipindi vyako vile vya moja kwa moja kutoka viwanja vya sabasaba na wakati mwingine ukihojiana na viongozi na wanasiasa mbalimbali nchini katika vipindi maalumu.

So,
nikiri tu kwamba ni kweli wengi hatukuona ulivyoviona kabla na mapema zaidi kumuhusu Dr.Samia Suluhu Hassan na pengine viongozi wengine waandamizi serikalini na katika medani za siasa.

Na,
we thank you for the reference ambazo pia hatukua tukizitilia maanani wakati umezipost zikiwa fresh.
 
Endelea kuota ndoto za mchana
ndoto ni taarifa muhimu sana ambazo ukiweza kuzitilia maanani na kuzitafsiri kwa ufasaha, unaweza kupiga hatua muhimu sana maishani mwako, lakini unaweza kuepuka hatari kubwa zaidi maishani mwako

So,
usipuuze ndoto zaka za mchana au usiku gentleman,

But muhimu zaidi, jikite kwenye hoja mezani bila kuonyesha dalili za kukata tamaa🐒
 
Naunga mkono hoja, ila napendekeza tumuongeze miaka 5, na kwa vile yeye amejaaliwa mwili wa shukrani, apart from kumpatia mtu mzuri wa gym, pia apate na mtu mzuri wa diet, a good dietation, afeed more on supplements, than the normal foods, ili ule mwili ufike 75 with good srengths.
P
 
Hivi kuna kiwango kibaya zaidi ya kile cha kuua watu 10,000, kumwaga damu lita 500,000; halafu mtu kutembea kifua mbele na kumsifia? Haoni mwenzie Yuda Escariote alivyofanya baada ya kumwaga damu ya Yesu? Huyo shetani naye angefanya vile vile labda angesamehewa, she doesn't repent, she has no remorse, The Sadist
Gentleman,
hizo porojo hazina athari zozote zile za kisiasa kuelekea mchakato wa katiba mpya na nyongeza ya muda wa uongozi wa Dr.Samia Suluhu Hassan kuelekea kipindi cha mpito cha utekelezaji wa matumizi ya katiba mpya kabla ya Rais mpya kushika hatamu.

So,
ni muhimu kujikita kwenye hoja mezani bila kumbwelambwela na mambo yasiyohuska na kabisa yasiyo na athari zozote kuelekea mchakato wa katiba mpya 🐒
 
Huyu mama muuaji, kaua maelfu ya watu na watoto, kawazika mwenyewe kwenye makaburi ya halaiki.
acha porojo na uzushi usio na athari zozote kuelekea mchakato wa katiba mpya gentleman,

jikite kwenye hoja bila kuweweseka na itapendeza zaidi gentleman 🐒
 
Huyu mama muuaji, kaua maelfu ya vijana na watoto, kawazika mwenyewe kwenye makaburi ya halaiki.
Mkuu Chivu, Chivundu , kwani mauaji yale yalifanyika kwa siri?, au yalifanyika usiku?, mauaji yale yalifanyika mchana peupe waziwazi, hivyo wauaji wote wameonekana na watu, kuna mtu yoyote alimuona huyu amebeba silaha yoyote kuua mtu yoyote?.

Labda kama hoja yako ingekuwa, walioua ni vyombo vya dola, polisi, jeshi na usalama wa taifa, ila aliyetoa amri waue ni nani?, aliyetoa amri watumie risasi za moto ni nani?.

Mauaji yalifanyika kwa amri ya Raisi mwenye kiapo kwa "Presidential decree". Kama kulizimwa internet, kukatolewa amri ya kutotoka nje, maana yake hiyo ni "Presidential decree".
 
Mauaji yalifanyika kwa amri ya Raisi mwenye kiapo kwa "Presidential decree". Kama kulizimwa internet, kukatolewa amri ya kutotoka nje, maana yake hiyo ni "Presidential decree".
Kila presidential decree, lazima itolewe kwa maandishi and it is a is a public document, na ofisa yoyote wa serikali, anapotoa order ya utekelezaji hiyo decree, lazima aifanyie citation hiyo decree.

Kwenye ile amri ya kutotoka nje baada ya saa 12:00, ilisemwa ni presidential decree?, ilikuwa cited?, ilikuwa attached?. No!, it was not!.

Usichanganye mamlaka ya Rais Kutangaza hali ya hatari, presidential decree na presidential order!
Ile October 29, japo ni kweli kulikuwa na hatari, lakini hakuna taarifa yoyote ya rais kutangaza hali ya hatari kwa mujibu wa katiba!.

Madaraka ya kutangaza hali ya hatari
(1) Bila ya kuathiri Katiba hii, au sheria iliyotungwa na Bunge kwa ajili hiyo, Rais aweza kutangaza hali
ya hatari katika Jamhuri ya Muungano au katika sehemu yake yoyote.

(2) (3) (4) (5) (6) Rais aweza tu kutangaza kuwa kuna hali ya hatari iwapo–
(a) Jamhuri ya Muungano iko katika vita; au
(b) kuna hatari hasa kwamba Jamhuri ya Muungano inakaribia kuvamiwa au kuingia katika hali
ya vita; au
(c) kuna hali halisi ya kuvurugika kwa amani ya jamii au kutoweka kwa usalama wa jamii katika
Jamhuri ya Muungano au sehemu yake yoyote kiasi kwamba ni lazima kuchukua hatua za
pekee ili kurejesha amani na usalama; au
(d) kuna hatari dhahiri na kubwa, kiasi kwamba amani ya jamii itavurugika na usalama wa raia
kutoweka katika Jamhuri ya Muungano au sehemu yake yoyote ambayo haiwezi kuepukika
isipokuwa kwa kutumia mamlaka ya pekee; au
(e) karibu kutatokea tukio la hatari au tukio la balaa au la baa ya kimazingira ambalo linatishia
jamii au sehemu ya jamii katika Jamhuri ya Muungano; au
(f) kuna aina nyingineyo ya hatari ambayo kwa dhahiri ni tishio kwa nchi.
Endapo inatangazwa kwamba kuna hali ya hatari katika Jamhuri ya Muungano nzima, au katika
Tanzania Bara nzima au katika Tanzania Zanzibar nzima, Rais atatuma mara nakala ya tangazo hilo
kwa Spika wa Bunge ambaye, baada ya kushauriana na Kiongozi wa shughuli za Serikali Bungeni,
ataitisha mkutano wa Bunge ndani ya siku zisizozidi kumi na nne, ili kuitafakari hali ya mambo na
kuamua kupitisha au kutopitisha azimio, litakaloungwa mkono na kura za wajumbe wasiopungua
theluthi mbili ya wajumbe wote, la kuunga mkono tangazo la hali ya hatari lililotolewa na Rais.
Bunge laweza kutunga sheria inayoweka masharti kuhusu nyakati na utaratibu ambao
utawawezesha watu fulani wenye kusimamia utekelezaji wa mamlaka ya Serikali katika sehemu
mahususi za Jamhuri ya Muungano kumuomba Rais kutumia madaraka aliyopewa na ibara hii
kuhusiana na yoyote kati ya sehemu hizi endapo katika sehemu hizi kunatokea yoyote kati ya hali
zilizotajwa katika aya ya (c), (d) na (e) za ibara ndogo ya (2) na hali hiyo haivuki mipaka ya sehemu
hizo; na pia kwa ajili ya kufafanua utekelezaji wa mamlaka ya Serikali wakati wa hali ya hatari.

Hivyo japo tarehe 20 October kulikuwa na hali ya hatari, hakuna taarifa yoyote ya rais kutangaza hali ya hatari, hivyo aliyetoa amri ile ya kutumika kwa risasi za moto na kuwaua Watu wasio na hatia na sio waandamani, bado anatakiwa atajwe, awajibike na kuwajibishwa!.

Pasco,
Kwanza nakushukuru kwa kutoa maelezo mazuri na ufafanuzi kuhusu "Precedential decree". Maelezo hako ni haya hapa;

Kila presidential decree, lazima itolewe kwa maandishi and it is a is a public document, na ofisa yoyote wa serikali, anapotoa order ya utekelezaji hiyo decree, lazima aifanyie citation hiyo decree

Majibu yangu; Pasco, ni kweli lakini sio lazima kila presidential decree sharti itolewe kwa maandishi na labda itangazwe kwenye gazeti la serikali.

Katika scenario za dharura au udikteta, presidential order/executive order huwa hazitolewi kwa minajiri ya kisiasa, na hapo ndipo kinazaliwq kitu kinaitwa "Rule by decree".

Rule by decree inakwepa bunge/legislature na inakwepa pia utaratibu wote huo hapo juu.
Hiki ndicho kilitokea Oktoba 29, Katiba iliwekwa pembeni, utaratibu uliwekwa pembeni, nchi kwa siku zote zile iliendeshwa kwa "Rule by decree", katika siku zile kimadaraka ulikuwa ukimtafuta Raisi humuoni, ukitafuta bunge hulioni, ukitafuta utaratibu huuoni, ukitafuta jeshi hulioni. Kwa siku zile tano, nchi iliendeshwa kwa "Rule by decree".

Kwa mazingira hayo "Order-to-kill" ilitoka kwa Mkuu wa nchi, tulikuwa kwenye "Rule by decree" kwa siku zile. Kulikuwa hakuna maelekezo wala utaratibu, ilikuwa ni utekelezaji tuu kwa kile ambacho kiliitwa "Kurudisha hali ya amani kwa namna yeyote".

Kuhusu hali ya hatari, kusingekuwa na tangazo hilo, maana lingekuwepo leo tusingekua tunapata shida ya nani alitoa "Amri ya kuua".
Ambaye angetangaza hali ya hatari, ndie huyo huyo mwenye kutoa "Order-to-kill" kwa hiyo alichanga vyema karata zake.

Walijua athari ya kufanya hivyo; ndio maana wakaona watumie "Rule by decree" yaani maelekezo yanatoka lakini hayajulikali yametoka wapi, wala hayatangazwi ila yanatekelezwa.
 
Hiyo miaka minne akuongoze wewe na mkeo
No,
anaongoza taifa na watu wake wote kuelekea mchakato wa katiba mpya my lady.

muhimu zaidi, usichoke kufuatilia shule muhimu sana inayoshushwa na walimu wa sheria ndani ya hoja hii 🐒
 
Back
Top Bottom