Katiba Mpya: Mapambano yako katika Hatua za Mwisho

brazaj

JF-Expert Member
Joined
Jul 26, 2016
Posts
31,698
Reaction score
41,733
Mapambano ya kudai katiba mpya ni mapambano kudai haki, uhuru na demokrasia.

Demokrasia ni kuwa na utawala unaowajibika kwa wananchi. Siyo utawala unaowajibika kwa watawala.

Kwenye demokrasia:

1. tozo za miamala ya simu zisingekuwapo,
2. bambikizaji za kesi zisingekuwapo,
3. polisi wasingejikweza kiasi cha kujengeka kwa chuki kubwa iliyopo baina yao na wananchi,
4. Waziri asinge thubutu kuja na habari za watu kuhamia Burundi,
5. madhila ya gonjwa la Corona yangekuwa jukumu ya serikali na si mzigo kwa wananchi
6. Tusingekuwa na rundo la vigogo wasiolipa kodi,
7. nk.

Ni wazi kuwa hayupo mtanzania mwenye akili timamu anayeweza kuyapinga au hata kutokuwa sehemu ya jitihada hizi.

Wenye maslahi na mfumo uliopo hatuna haja ya kupoteza nao muda kujaribu kuwaelimisha. Hao ndiyo walio kizingiti pekee.

Kwa hakika tunatatizika kwenye organization. Yaani uongozi wa mapambano kumalizia tokea tulipo salama. Chadema wanayo nafasi hii takatifu ya kutoa uongozi unaohitajika kufanikisha hili.

Katika hatua hizi za mwisho ilitosha kuwaunganisha washirika wengine kama ACT, NCCR na wanaoweza kuwa tayari. Tujikite zaidi kwenye kuhamasisha wanachama wetu kutoa uongozi unaohitajika kwenye jitihada hizi.

Ukweli ni lazima uelezwe wazi wazi. Hii vita haiwezi kuwa rahisi. Kutakuwa na machungu. Kuna watakaokamatwa, kuna watakaoteswa, kuna watakao fungwa, kuna watakao kufa, nk. Ni majukumu ya washirika kuona ya kufanya kuhusu haya.

Pamoja na yote, hatutatumia nguvu ila wingi wetu na utayari wetu wa kuyajaza magereza yao ikibidi, vinatosha sana.

Hamasa za machungu (sober) kama hizi zitatufaa sana kama wapambanaji wenye kuhimiza amani kama msingi wa maelewano.

Apumzike kwa amani brigedia Chefe Ali.

Ifahamike halipo kosa kisheria katika kudai haki, hii kama ilivyo kwa mujibu wa katiba.

Shime waungwana hatuko mbali, na ushindi ni dhahiri.
 
Kweli kabisa

Hatuko mbali. Nani mwenye akili timamu hataki haki, usawa uhuru na utawala wa kidemokrasia?

Hatuna haja ya kupoteza muda na mtu huyo leo.

Tujikite kuongeza washirika na hasa walio organized tutie hamasa.

Apumzike kwa amani brigedia Chefe Ali.
 
Tatizo woga ndio mana nawaambia hamko tayari bila damu nyingi hiyo katiba mtaishia kuiimba tuu

Haupo woga, tunasonga mbele tuko vizuri na tunakuwa vizuri zaidi kila siku ipitayo. Hatukuwahi kuwa hapa. Leo:

1. Tunajua vita vyetu ni vya amani
2. Tunajua wingi wetu na utayari wetu wa kuyajaza magereza yao ni silaha na ngao yetu kuu
3. Tunajua kuwa hakuna mtanzania mwenye akili timamu asiyetaka haki, usawa, uhuru na demokrasia
4. Tunajua kuwa hatuna haja ya kushughulika na kuelimisha watu tena kwani walio vizingiti ni kwa sababu ni wanufaika wa mfumo uliopo
5. Tunajua kuwa vyama kama NCCR, ACT na vingine vipo tunaweza kufungamanisha jitihada hizi
6. Tunajua kuwa wigo wa ushiriki ni shuruti upanuliwe kuwahusisha wote wenye maslahi na katiba mpya
7. Nk

Tunaweza kuimba nyimbo za hamasa zenye kumtia kiwewe adui na kutia hamasa ya kutosha.

Apumzike kwa amani brigedia Chefe Ali.
 
Nadhani anatania jitihada hizi zinawahusu sana watoto wa wajukuu zake.

Ashukuriwe yeyote anajitoa kwa hali na mali kwenye vita hivi.

"Mh. Mbowe na wote mikononi mwao, heshima kwenu mmetangulia nasi tunakuja nyuma."
Ndugu yangu Wastendi Karibu tujumuike kwenye,kazi hii ya kuwaandalia watoto na wajukuuzetu na kizazi kijacho mazingira bora ya uhuru ,haki na jamii yenye kufuata sheria na katiba ya taifa hili.
 
Mapambano ya kudai katiba mpya ni mapambano kudai haki, uhuru na demokrasia.

Demokrasia ni kuwa na utawala unaowajibika kwa wananchi. Siyo utawala unaowajibika kwa watawala.

Kwenye demokrasia:

1. tozo za miamala ya simu zisingekuwapo,
2. bambikizaji za kesi zisingekuwapo,
3. polisi wasingejikweza kiasi cha kujengeka kwa chuki kubwa iliyopo baina yao na wananchi,
4. Waziri asinge thubutu kuja na habari za watu kuhamia Burundi,
5. madhila ya gonjwa la Corona yangekuwa jukumu ya serikali na si mzigo kwa wananchi
6. Tusingekuwa na rundo la vigogo wasiolipa kodi,
7. nk.

Ni wazi kuwa hayupo mtanzania mwenye akili timamu anayeweza kuyapinga au hata kutokuwa sehemu ya jitihada hizi.

Wenye maslahi na mfumo uliopo hatuna haja ya kupoteza nao muda kujaribu kuwaelimisha. Hao ndiyo walio kizingiti pekee.

Kwa hakika tunatatizika kwenye organization. Yaani uongozi wa mapambano kumalizia tokea tulipo salama. Chadema wanayo nafasi hii takatifu ya kutoa uongozi unaohitajika kufanikisha hili.

Katika hatua hizi za mwisho ilitosha kuwaunganisha washirika wengine kama ACT, NCCR na wanaoweza kuwa tayari. Tujikite zaidi kwenye kuhamasisha wanachama wetu kutoa uongozi unaohitajika kwenye jitihada hizi.

Ukweli ni lazima uelezwe wazi wazi. Hii vita haiwezi kuwa rahisi. Kutakuwa na machungu. Kuna watakaokamatwa, kuna watakaoteswa, kuna watakao fungwa, kuna watakao kufa, nk. Ni majukumu ya washirika kuona ya kufanya kuhusu haya.

Pamoja na yote, hatutatumia nguvu ila wingi wetu na utayari wetu wa kuyajaza magereza yao ikibidi, vinatosha sana.

View attachment 1923610

Hamasa za machungu (sober) kama hizi zitatufaa sana kama wapambanaji wenye kuhimiza amani kama msingi wa maelewano.

Apumzike kwa amani brigedia Chefe Ali.

Ifahamike halipo kosa kisheria katika kudai haki hii kama ilivyo kwa mujibu wa katiba.

Shime waungwana hatuko mbali na ushindi ni dhahiri.
Mkuu, uzi mzuri.
 
Tatizo woga ndio mana nawaambia hamko tayari bila damu nyingi hiyo katiba mtaishia kuiimba tuu
Hii ni pamoja nawewe na hata hao mapolisi yanayohangaika kubambikia watu kesi kwenye hizi harakati. Sote tusongeni mbele Kwa umoja wetu hadi kieleweke.
 
Ni jambo jema kutaka,na kuhakikisha haki inatendeka kwa wote na kwa maslahi ya taifa.Na njia pekee kwa sasa nikupatikana katiba mpya. Kwani njia nyingine zimethibitisha kushindwa kufanya kazi, ikiwa ni pamoja na watawala kushindwa kuwahakikishia hilo wananchi ambao ndio waajiri wao,kupitia katiba iliyopo sasa iliyokuwa na mapungufu makubwa yanayotumiwa na watawala na kundi la wachache kwa manufaa yawachache na sii kwa manufaa mapana ya wananchi na taifa letu pendwa Tanzania.
 
Hii ni pamoja nawewe na hata hao mapolisi yanayohangaika kubambikia watu kesi kwenye hizi harakati. Sote tusongeni mbele Kwa umoja wetu hadi kieleweke.

Waoga wanaoonekana ni kwa sababu ya kukosekana organization tu.

Wanachama wakereketwa wa vyama hivi tunatosha sana panapo hamasa kutoa uongozi unaotakikana.

Tuelezane ukweli. Ukweli mchungu na msema kweli ni mpenzi wa Mungu.
 
Hii ni pamoja nawewe na hata hao mapolisi yanayohangaika kubambikia watu kesi kwenye hizi harakati. Sote tusongeni mbele Kwa umoja wetu hadi kieleweke.
Nina kiapo changu siwezi fanya hivyo nitakuwa nimekiuka.
 
Mapambano ya kudai katiba mpya ni mapambano kudai haki, uhuru na demokrasia.

Demokrasia ni kuwa na utawala unaowajibika kwa wananchi. Siyo utawala unaowajibika kwa watawala.

Kwenye demokrasia:

1. tozo za miamala ya simu zisingekuwapo,
2. bambikizaji za kesi zisingekuwapo,
3. polisi wasingejikweza kiasi cha kujengeka kwa chuki kubwa iliyopo baina yao na wananchi,
4. Waziri asinge thubutu kuja na habari za watu kuhamia Burundi,
5. madhila ya gonjwa la Corona yangekuwa jukumu ya serikali na si mzigo kwa wananchi
6. Tusingekuwa na rundo la vigogo wasiolipa kodi,
7. nk.

Ni wazi kuwa hayupo mtanzania mwenye akili timamu anayeweza kuyapinga au hata kutokuwa sehemu ya jitihada hizi.

Wenye maslahi na mfumo uliopo hatuna haja ya kupoteza nao muda kujaribu kuwaelimisha. Hao ndiyo walio kizingiti pekee.

Kwa hakika tunatatizika kwenye organization. Yaani uongozi wa mapambano kumalizia tokea tulipo salama. Chadema wanayo nafasi hii takatifu ya kutoa uongozi unaohitajika kufanikisha hili.

Katika hatua hizi za mwisho ilitosha kuwaunganisha washirika wengine kama ACT, NCCR na wanaoweza kuwa tayari. Tujikite zaidi kwenye kuhamasisha wanachama wetu kutoa uongozi unaohitajika kwenye jitihada hizi.

Ukweli ni lazima uelezwe wazi wazi. Hii vita haiwezi kuwa rahisi. Kutakuwa na machungu. Kuna watakaokamatwa, kuna watakaoteswa, kuna watakao fungwa, kuna watakao kufa, nk. Ni majukumu ya washirika kuona ya kufanya kuhusu haya.

Pamoja na yote, hatutatumia nguvu ila wingi wetu na utayari wetu wa kuyajaza magereza yao ikibidi, vinatosha sana.

View attachment 1923610

Hamasa za machungu (sober) kama hizi zitatufaa sana kama wapambanaji wenye kuhimiza amani kama msingi wa maelewano.

Apumzike kwa amani brigedia Chefe Ali.

Ifahamike halipo kosa kisheria katika kudai haki hii kama ilivyo kwa mujibu wa katiba.

Shime waungwana hatuko mbali na ushindi ni dhahiri.
Ni nyakati za mwisho mwisho hizi. Katiba Mpya i akuja.
 
Back
Top Bottom