Katiba Mpya: Mapambano yako katika Hatua za Mwisho

Katiba Mpya: Mapambano yako katika Hatua za Mwisho

Haupo woga, tunasonga mbele tuko vizuri na tunakuwa vizuri zaidi kila siku ipitayo. Hatukuwahi kuwa hapa. Leo:

1. Tunajua vita vyetu ni vya amani
2. Tunajua wingi wetu na utayari wetu wa kuyajaza magereza yao ni silaha na ngao yetu kuu
3. Tunajua kuwa hakuna mtanzania mwenye akili timamu asiyetaka haki, usawa, uhuru na demokrasia
4. Tunajua kuwa hatuna haja ya kushughulika na kuelimisha watu tena kwani walio vizingiti ni kwa sababu ni wanufaika wa mfumo uliopo
5. Tunajua kuwa vyama kama NCCR, ACT na vingine vipo tunaweza kufungamanisha jitihada hizi
6. Tunajua kuwa wigo wa ushiriki ni shuruti upanuliwe kuwahusisha wote wenye maslahi na katiba mpya
7. Nk

Tunaweza kuimba nyimbo za hamasa zenye kumtia kiwewe adui na kutia hamasa ya kutosha.

Apumzike kwa amani brigedia Chefe Ali.
Wakipatikana 50 wenye nia na uthubutu wako mtashinda tatizo mkipanga hivyo yule kiongozi wenu akidakwa tuu nyie wengine mnaingiwa na ganzi ghafla ndio maana kila uchwao hao polisi wanafanikiwa kuwadhibiti
 
Ndugu yangu Wastendi Karibu tujumuike kwenye,kazi hii ya kuwaandalia watoto na wajukuuzetu na kizazi kijacho mazingira bora ya uhuru ,haki na jamii yenye kufuata sheria na katiba ya taifa hili.
Lianzisheni kwanza nikuone pale mbele kabisa na mimi niatapata morali wa kuingia
 
Waoga wanaoonekana ni kwa sababu ya kukosekana organization tu.

Wanachama wakereketwa wa vyama hivi tunatosha sana panapo hamasa kutoa uongozi unaotakikana.

Tuelezane ukweli. Ukweli mchungu na msema kweli ni mpenzi wa Mungu.
Vyama gani? Maana katika nchi yenye watu mil 60 wanaohangaika na hiyo katiba ni Bavicha tu! No support kutoka vyombo vya habari, vyama vingine vya upinzani, taasisi za kidini, serikali na vyombo vyake, wala jumuiya ya kimataifa! And unajipa moyo hapa! Katiba mpya itapatikana siku makundi yote muhimu yataamua kuitafuta hiyo katiba, na hilo halitotokea karibuni! Ila kujipa faraja hapa jf si mbaya, inaondoa stress nyingine za maisha tulizonazo
 
Ni nyakati za mwisho mwisho hizi. Katiba Mpya i akuja.

Kuwaandaa zaidi wanachama wetu na wa washirika wetu sawa sawa ndiyo ulio msingi madhubuti zaidi kwetu kwa sasa.

Kuwa na wanachama wakereketwa 100 (walio tayari kujaza) tu kwa kila mkoa kuna tupa katiba mpya.

Tutake nini zaidi kwa Mungu sisi?
 
Lianzisheni kwanza nikuone pale mbele kabisa na mimi niatapata morali wa kuingia

Ndiyo maana wenye kujua thamani Yaani wenye ngoma katika vyama tunapaswa kutoa uongozi.

Pumzika kwa amani brigedia Chefe Ali.
 
Wakipatikana 50 wenye nia na uthubutu wako mtashinda tatizo mkipanga hivyo yule kiongozi wenu akidakwa tuu nyie wengine mnaingiwa na ganzi ghafla ndio maana kila uchwao hao polisi wanafanikiwa kuwadhibiti

Tuko wengi zaidi ya hao 50. Ninakubaliana nawe 50 tu kwa mkoa timbwili la kutosha.

Amani amani lakini magereza yajae.

100 kwa mkoa itapendeza zaidi.
 
Kuwaandaa zaidi wanachama wetu na wa washirika wetu sawa sawa ndiyo ulio msingi madhubuti zaidi kwetu kwa sasa.

Kuwa na wanachama wakereketwa 100 (walio tayari kujaza) tu kwa kila mkoa kuna tupa katiba mpya.

Tutake nini zaidi kwa Mungu sisi?
Mungu ni mwema. Na wanazidi kuboronga kila kukicha unaweza kudhani ni dharau lakini lazima mwisho wao ufike. Ndio namna hiyo.
 
Hii inathibitisha kuwa Mbowe alifaniliwa sana kupenyeza matendo ya uovu na kihalifu kwa wafuasi wake ktk kipindi chake chote akiwa Mwenyekiti wa Chadema.
Tabia za wanachadema zinazo onekana leo hii kama vile; Uhalifu, Ujambazi, Uzaji wa madawa ya kulevya, Kupanga njama za kuuwa watu, kupanga njama za kutenda uhalifu, kujiteka, kuzua taharuki ktk jamii, kueneza uvumi ktk mitandao n.k zote hizo zilikuwa jitihada za Mwenyekiti wao.
 
Mapambano ya kudai katiba mpya ni mapambano kudai haki, uhuru na demokrasia.

Demokrasia ni kuwa na utawala unaowajibika kwa wananchi. Siyo utawala unaowajibika kwa watawala.

Kwenye demokrasia:

1. tozo za miamala ya simu zisingekuwapo,
2. bambikizaji za kesi zisingekuwapo,
3. polisi wasingejikweza kiasi cha kujengeka kwa chuki kubwa iliyopo baina yao na wananchi,
4. Waziri asinge thubutu kuja na habari za watu kuhamia Burundi,
5. madhila ya gonjwa la Corona yangekuwa jukumu ya serikali na si mzigo kwa wananchi
6. Tusingekuwa na rundo la vigogo wasiolipa kodi,
7. nk.

Ni wazi kuwa hayupo mtanzania mwenye akili timamu anayeweza kuyapinga au hata kutokuwa sehemu ya jitihada hizi.

Wenye maslahi na mfumo uliopo hatuna haja ya kupoteza nao muda kujaribu kuwaelimisha. Hao ndiyo walio kizingiti pekee.

Kwa hakika tunatatizika kwenye organization. Yaani uongozi wa mapambano kumalizia tokea tulipo salama. Chadema wanayo nafasi hii takatifu ya kutoa uongozi unaohitajika kufanikisha hili.

Katika hatua hizi za mwisho ilitosha kuwaunganisha washirika wengine kama ACT, NCCR na wanaoweza kuwa tayari. Tujikite zaidi kwenye kuhamasisha wanachama wetu kutoa uongozi unaohitajika kwenye jitihada hizi.

Ukweli ni lazima uelezwe wazi wazi. Hii vita haiwezi kuwa rahisi. Kutakuwa na machungu. Kuna watakaokamatwa, kuna watakaoteswa, kuna watakao fungwa, kuna watakao kufa, nk. Ni majukumu ya washirika kuona ya kufanya kuhusu haya.

Pamoja na yote, hatutatumia nguvu ila wingi wetu na utayari wetu wa kuyajaza magereza yao ikibidi, vinatosha sana.

View attachment 1923610

Hamasa za machungu (sober) kama hizi zitatufaa sana kama wapambanaji wenye kuhimiza amani kama msingi wa maelewano.

Apumzike kwa amani brigedia Chefe Ali.

Ifahamike halipo kosa kisheria katika kudai haki hii kama ilivyo kwa mujibu wa katiba.

Shime waungwana hatuko mbali na ushindi ni dhahiri.

1630770712572.png

ni mda wako sasa kwenda kupimwa akili
 
Hii inathibitisha kuwa Mbowe alifaniliwa sana kupenyeza matendo ya uovu na kihalifu kwa wafuasi wake ktk kipindi chake chote akiwa Mwenyekiti wa Chadema.
Tabia za wanachadema zinazo onekana leo hii kama vile; Uhalifu, Ujambazi, Uzaji wa madawa ya kulevya, Kupanga njama za kuuwa watu, kupanga njama za kutenda uhalifu, kujiteka, kuzua taharuki ktk jamii, kueneza uvumi ktk mitandao n.k zote hizo zilikuwa jitihada za Mwenyekiti wao.

Huu uzi kwani unawahusu nini ninyi?

Hayupo mwenye akili timamu ambaye haki, usawa, uhuru na utawala wa kidemokrasia ukidaiwa anakereka isipokuwa aliye mnufaika vilivyo wa mustakabala uliopo kama wewe.

Ninyi ni adui zetu "by your own declarations."

Kwani hata tuna haja ya kushughulika nanyi?

Sisi ninyi tunawapuuza tu.

Kwa amani na nyimbo za hamasa kama za brigadier Chefe Ali, twaja.

Apumzike kwa amani brigedia Chefe.
 
Sijuia vijana wa bavicha akili zimekimbilia kwenye makalio

Humu msiohusika mnafuata nini? Uzi huu mbona umewatambua na kuwapa nafasi yenu:

"Ni wazi kuwa hayupo mtanzania mwenye akili timamu anayeweza kuyapinga au hata kutokuwa sehemu ya jitihada hizi.

Wenye maslahi na mfumo uliopo hatuna haja ya kupoteza nao muda kujaribu kuwaelimisha. Hao ndiyo walio kizingiti pekee."

Kwa kujikaribisha mwenyewe usipotakikana ni kujiweka kwenye mkao wenyewe kamili wa kuwa huna akili timamu.

Wewe wala huhitaji kupimwa akili!

Hatuna mtanzania mwenye akili timamu asiyetaka haki, usawa, uhuru, na utawala wa kidemokrasia.

Hata mheshimiwa Rais Samia analijua hilo.

Apumzike kwa amani brigedia Chefe.
 
View attachment 1923811

ni mda wako sasa kwenda kupimwa akili

Itifaki yote ilizingatiwa:

"Ni wazi kuwa hayupo mtanzania mwenye akili timamu anayeweza kuyapinga au hata kutokuwa sehemu ya jitihada hizi.

Wenye maslahi na mfumo uliopo hatuna haja ya kupoteza nao muda kujaribu kuwaelimisha. Hao ndiyo walio kizingiti pekee."

Wewe ni mtanzania hutaki haki, usawa, uhuru wala utawala wa kidemokrasia?

It's has been said, "you are insane!"

The rest is tantamount to poking of your nose into other people's business.

Unahusika vipi wewe kwenye uzi huu?

Apumzike kwa amani brigedia Chefe.
 
Vyama gani? Maana katika nchi yenye watu mil 60 wanaohangaika na hiyo katiba ni Bavicha tu! No support kutoka vyombo vya habari, vyama vingine vya upinzani, taasisi za kidini, serikali na vyombo vyake, wala jumuiya ya kimataifa! And unajipa moyo hapa! Katiba mpya itapatikana siku makundi yote muhimu yataamua kuitafuta hiyo katiba, na hilo halitotokea karibuni! Ila kujipa faraja hapa jf si mbaya, inaondoa stress nyingine za maisha tulizonazo

Hivi huwa hamjishangai? Hukuona kuwa itifaki ilizingatiwa:

"Ni wazi kuwa hayupo mtanzania mwenye akili timamu anayeweza kuyapinga au hata kutokuwa sehemu ya jitihada hizi.

Wenye maslahi na mfumo uliopo hatuna haja ya kupoteza nao muda kujaribu kuwaelimisha. Hao ndiyo walio kizingiti pekee."

Nyie msiotaka haki, usawa, uhuru wala demokrasia mada hii inawahusu nini?

Hata mheshimiwa SSH anajua watanzania wenye akili timamu wanayataka hayo usiyoyataka wewe.
 
Back
Top Bottom