Wewe unadhani ni demokrasia gani ya kukufaa: ya kukupa kila kitu na ya kusifia tu, ukisema jambo fulani siyo zuri linaweza kufanyika kwa namna bora zaidi unakuwa umekosea? Hiyo ndiyo demokrasia unayoitaka? Hata hiyo unayoitaka ulizaliwa nayo au nayo utakuwa umeletewa na hao wanaoitekeleza? Elimu umeletewa, mbona huipingi? Afya umeletewa, mbona huipingi? Aina ya ujenzi wa miundombinu ya kisasa, usafiri wa magari, ndege etc na hata uvaaji wa nguo, viatu, matumizi ya TV, kompyuta, simu etc - vyote hivi umeletewa...Kwa hiyo, unasemaje, tufanyeje? Tuvirudishe huko vilikotoka?