Katiba Mpya: Ukweli Usiosemeka

Katiba Mpya: Ukweli Usiosemeka

brazaj

JF-Expert Member
Joined
Jul 26, 2016
Posts
31,698
Reaction score
41,733
Mazingira yanaoizunguka katiba mpya ni muhimu yakajulikana yote wazi wazi.

Inafahamika kuwa CCM walio wanufaika wa katiba iliyopo, hawana sababu yoyote ya kujitia kitanzini kwa kuridhia ujio wa katiba mpya kirahisi.

IMG_20210702_051847_798.jpg

Kutokupatikana kwa katiba mpya kutaifanya CCM kuwa imefanikiwa katika malengo yake. CCM inategemea itafanikiwa malengo yake kwa kuamini:

1. Wadai katiba ni wastaarabu wasiotaka kutumia nguvu au makabiliano yoyote ya kuhusisha nguvu.

2. Wadai katiba wako tayari kususia chaguzi zote bila ya kuwa na tume huru au katiba mpya.

Sababu mbili hizi zinapendwa sana na CCM kwani:

1. Kwa kukomaa tu, wadai katiba kistaarabu watapisha makabiliano. Hivyo CCM wataendelea kwa raha zao.

2. Kwa kukomaa tu, wapinzani watasusa chaguzi na CCM wataendelea kwa raha zao.

Inatakikana jitihada kubwa ya makusudi ya kuukata mnyororo huu wa matukio.
 
Hivi ni kweli limekimbia nchi,vipi kuhusu wale mbususu wake
Kama vipi tukajifunze kwa wenzetu wa Swaziland a.k.a Eswatin, ili kuona ni kwa namna gani waliweza kupata ujasiri wa kupambana na lile lidubwasha lao, kiasi cha kulilazimisha kukimbilia uhamishoni..
 
Kama Mwenyekiti wa kudumu hataki kuachia hatamu je ataheshimu katiba kwa kutoka madarakani endapo akiwa Rais wa nchi?

Chama kinachodai katiba kina kasoro za kikatiba katika chama chao.
 
Jomba hii katiba co ya chadema,achen kupenda mbeleko hoja ya katiba mpya haijaanza jana wala juz

Tuonesheni mfano kwanza isije ikawa mnatufundisha msichoweza kukifanya Mwenyekiti wa kudumu apumzike na wengine waongoze.
 
Kwa nini watu wanadai KATIBA mpya? Majibu mengi: Kwa ajili ya uchaguzi na wanaongeza na sababu hii bila KATIBA mpya hatushiriki Uchaguzi. Hapo naona vyama vya upinzani ni WASAKATONGE.

Wangedai katiba mpya kuboresha kilimo cha nchi badala yake katiba mpya kwa ajili ya UCHAGUZI tuu hapo kuna shida. Katiba mpya kwa ajili ya madaraka BIG NO. KATIBA yetu ni nzuri na kazi iendelee.
 
Mkuu Katiba inakuja hakuna wa kuzuia, aya Mambo ni magumu KWA maana tufikilia kibinadam
Mazingira yanaoizunguka katiba mpya ni muhimu yakajulikana yote wazi wazi.

Inafahamika kuwa CCM walio wanufaika wa katiba iliyopo, hawana sababu yoyote ya kujitia kitanzini kwa kuridhia ujio wa katiba mpya kirahisi...
 
Kama Mwenyekiti wa kudumu hataki kuachia hatamu je ataheshimu katiba kwa kutoka madarakani endapo akiwa Rais wa nchi?

Chama kinachodai katiba kina kasoro za kikatiba katika chama chao.

Katiba ni ya wananchi. Wanaoihitaji ni wananchi.

Mwenyekiti wa wananchi wepi unayemwongelea wewe?
 
Nasema hv acha kuwa zumbukuku,kwnn mnapenda huu mserereko uliopo ktk hii katba chakavu ya chama chakavu?????
Hapana Mwenyekiti wa kudumu atuoneshee kwa mifano aachie na wengine waongoze then tutamuelewa.
 
Kama Mwenyekiti wa kudumu hataki kuachia hatamu je ataheshimu katiba kwa kutoka madarakani endapo akiwa Rais wa nchi?

Chama kinachodai katiba kina kasoro za kikatiba katika chama chao.
Katiba za vyama zimekuwa za hovyo kwa sababu ya katiba mama ya nchi. Laiti tungekuwa na katiba nzuri inayotenganisha mamlaka za kidola wala upuuzi usingekuepo kwa wananchi hata watawala.

Na ndiyo maana

Jk ndiyo aliifanyia katiba mpya UNAFIKI technically . Mambo yalikuwa vizuri tu mpaka kabla ya uwasilishaji. Lakini ratiba ilipochezewa tu, ili Jaji Warioba atangulie kisha yeye aje kuponda mapendekezo ya wananchi . Kuanzia hapo alililetea jambo hilo ushabiki kwa wajumbe ambao mwanzo walikuwa wamoja .

So Kikwete hakuitaka katiba mpya .
 
Katiba ni ya wananchi. Wanaoihitaji ni wananchi.

Mwenyekiti wa wananchi wepi unayemwongelea wewe?
Sasa kama katiba ya wananchi sasa kwanini mwenyekiti wa kudumu anatuongelea utafikiri tulikaa na akakusanya maoni yetu?

Atuoneshe kwa vitendo aachie na wengine waongoze.
 
Katiba za vyama zimekuwa za hovyo kwa sababu ya katiba mama ya nchi. Laiti tungekuwa na katiba nzuri inayotenganisha mamlaka za kidola wala upuuzi usingekuepo kwa wananchi hata watawala....
Sasa mwenyekiti wa kudumu aanze kuibadili ya chama then aachie madarka kwa wengine hapa lazima tuwaunge mkono kurekebisha hii ya nchi.
 
Back
Top Bottom