Kwa nini watu wanadai KATIBA mpya? Majibu mengi: Kwa ajili ya uchaguzi na wanaongeza na sababu hii bila KATIBA mpya hatushiriki Uchaguzi. Hapo naona vyama vya upinzani ni WASAKA TONGE. Wangedai katiba mpya kuboresha kilimo cha nchi badala yake katiba mpya kwa ajili ya UCHAGUZI tuu hapo kuna shida. Katiba mpya kwa ajili ya madaraka BIG NO. KATIBA yetu ni nzuri na kazi iendelee.
Sababu za kudai katiba ni mbalimbali kwa kila mwananchi na ndiyo maana makundi yote hushirikishwa.
Hapa chini ni baadhi ya mapungufu ya wazi ya katiba iliyopo, ambayo yanaweka umuhimu na dharura ya katiba mpya hasa kwa mtanzania yule wa kawaida:
1. Katiba iliyopo haiwawajibishi baadhi ya watendaji wakuu kwa kuikiuka, na hii ni kwa mujibu wa katiba yenyewe.
2. kwa katiba iliyopo pana watu hata kama wakiiba, wakipora, wakiuwa, wakidhulumu nk hiyo ni halali kwa mujibu wa katiba yenyewe.
3. katiba iliyopo inawapa baadhi ya watu mamlaka ya kujifanyia lolote bila kuhojiwa au hata kuwajibishwa tu.
4. Katiba iliyopo haitoi haki sawa kwa watu wote ndani ya nchi.
5. Kuna mianya mingi katika katiba hii ambayo inaweza kuifanya mihimili mingine hata kupoteza uhuru wake wa kiutendaji kwa mujibu wa katiba yenyewe.
6. Kuna utitiri wa nafasi za uongozi wasio na tija wala ridhaa ya wananchi ambao pia ni mzigo mkubwa kwa mlipa kodi.
7. Kuna utitiri wa vigogo wenye mapato yasiyoakisi tija, wala kuwa na ridhaa ya wananchi na wasiolipa kodi wanaopata uhalali kwenye katiba hii.
8. Kwa katiba hii polisi wanaweza mshikilia mtu kwa kumbambikizia kesi hata kwa miaka kadhaa. Mhanga akaja kuachiliwa bila ya wahusika kuwajibika kwa lolote. Hili likihalalishwa na katiba hii.
9. Nk.Nk.
Yako mengi, kwenye mazingira haya hudhani kuwa mwananchi wa kawaida anaihitaji zaidi katiba mpya kuliko hata hao wanasiasa?
Kwamba, hudhani kuwa anayedhani hahitaji katiba mpya ni kwa sababu tu ya ujinga wake au kukosa elimu au kuwa na uelewa mdogo tu?
Au nasema uongo ndugu zangu?