Inafahamika kuwa maadui zetu ni walamba asali pekee. Hao ndiyo walio wanufaika wa hali iliyopo.
Wengine wakiwamo chawa na hata waliowahi kuwa chawa au kuwa walamba asali, wote ni wahanga tu.
Kundi la wasiojitambua halipaswi kuwa mzigo tena kufikia sasa.
Tunaotaka katiba mpya Kwa namna yoyote, sote tu washirika bila kujali historia.
Hatutapata katiba mpya kirahisi kwa kuwekeza kwenye kufukua fukua makaburi.
Tunahitaji busara ya kuziunganisha nguvu zetu ndani ya tofauti zilizopo, katu si katika kupalilia utengano.
Kuipata katiba mpya (Kwa mujibu wa mheshimiwa Mbowe) tunahitaji umahiri wa kushawishi. Ni muhimu tuweze kuwashawishi wote maadui na marafiki zetu ikiwezekana kuja upande wetu.
Kwa mujibu wa mheshimiwa Mbowe pia, mapande mapande ya uvyama au kiitikadi hayatusaidii.
Bila hivyo tunajichelewesha na tunajiwekea mazingira magumu sisi wenyewe.
United we stand, divided we fall!