Katiba ya CCM haina suala la Ukomo wa muda wa uongozi.

Wakati wa vita, adui anapokuchagulia Jemedari, na ukamkubali unakuwa umesalimu amri.
 
Mkuu Gideon Jeremiah, haki wewe u miongoni mwa wachache mnaipenda Chadema kwa dhati!. Kuna wengi ambao ni wanachama, wapenzi na mashabiki wa Chadema ambao ni wapambe tuu!, hawana lolote wala hawaisaidii Chadema kwa kuiibia nyimba tuu za sifa na mapambio!, mapenzi ya kweli, yanaonyeshwa pale mtu unapoumia mpaka nafsini na moyoni, ukiona chama unachokitegemea kinafanya madudu!, Mwigamba ameibua madai mazito ya msingi, halafu viongozi wanakujsa humu na majibu ya ....(mepesi) halafu mijitu humu inawashangilia!.
Asante tena Gideon Jeremiah.
Pasco.
 
Mkuu Lunyungu, sisi wengine huishia kusema tuu!, mambo ya ushahidi ni mahakamani, hapa sio mahakamani, niliuiza hili, wakuu wako wakajibu na ushahidi wao wakaleta!, kinachoendelea sasa ni matokeo tuu na sio chanzo!.
Naamini hata bila ushahidi, the effects is visible ama hili la visibility nalo unalitakia ushahidi!.
Pasco.
 
Kwa nini wana CCM wakerwe na viongozi wabaya wa CHADEMA?

Mkiwa vitani unaweza kukubali adui yako akuchagulie Kamanda wa vikosi vyako?

Tafakari.
Mwanaukweli with due respect, you're missing the point.

Hivi wewe viongozi wa CCM na serikali yake hawakukeri kwa maneno na matendo yao?. Kama wanakukera, kwa nini watu wengine pia wasikereke na viongozi wa CHADEMA kwa maneno na matendo yao.

Hoja za kisiasa kama hizi hazichagui watoa hoja kwa sababu kila mtanzania mwema huko huru kisheria kuwa mwananchama wa chama chochote kama anatimiza masharti ya uanachama ambayo kisheria siyo discriminative.

Kama chama kinataka kuepuka hoja kama hizi ni lazima kifanye kile kinachohubiri kwa wananchi.

Huwezi kuacha kuhoji pale mtu anapohubiri yeye ni maraika halafu matendo anayoyafanya niya kishetani.
 

Mkuu unampa sifa isiyo yake,

Yeye kwafani yake ya kusomea ni mkunga, na aliajiriwa na wizara ya afya kufanya kazi katika zahamati ya Mvomero Morogoro,

Hivi sasa kaacha kazi hiyo na yupo jijini Dar akilala Tabata Mawenzi na kushinda vijiwe vya Lumumba Mnazimoja akijifanya ni mpigania ccm kwa ndoto za ipo siku atapa hata u DC tu,


Kwakifupi mimi hupenda kumuita NGARIBA
 

Kwa hiyo mnalenu jambo nyuma yake mnataka CHADEMA ife sio?
 
Chadema uchaguzi wao wa ndani ni baada ya 2015 .Wamekosea kama walikuwa wanadhani wanaweza kupeta kirahisi .Hakuna Uchaguzi wafe tu huko waliko .

Mkuu lunyungu huo ndo ukweli. hata nchi huwa zinahairisha chaguzi zao kwa sbb mbalimbali. cdm tumeona kuwa sio muafaka kufanya uchaguzi sasa mbona magamba ma------ yao yanawawasha. mkapa alimkabidhi jk uenyekiti wa magamba kabla ya muda wake kuisha mbona ilionekana powa tu kwao? nasapoti uchaguzi usifanyike hadi baada ya uchaguzi. haya mambo ya mwigamba ni mashauri tu wala sio kesi. kamanda mbowe, dr slaa na zitto tuvusheni salama watanzania kuelekea kwenye ukombozi kamili dhidi ya mkoloni mweusi.
 
Hivi neno Chadema liko kwenye ilani ya uchguzi ya CCM? Hivi ni kwa nini CCM hawatekelezi ilani yao ya uchaguzi baadala yake wambaki kuparamia Chadema?

CDM ndiyo chama kinachoongiza katika njia moja au nyingine kwani ccm ishapoteza so watu wanahaki ya kukitaja na kukikosoa na ukiona hivyo ujue chadema ndiyo mbadala.
 
Kwa hiyo mnalenu jambo nyuma yake mnataka CHADEMA ife sio?
Hakuna Mtanzania mwenye kuitakia mema nchi hii kwa dhati, anayetaka Chadema ife!.

Mzazi anayejali, humcharaza bakora mwanaye anayempenda ili kumrudi asipotee!.

Tunachokifanya akina sisi, tena kwa nia njema na dhamira safi, ni kuitembezea Chadema bakora za nguvu, na kuipitisha kwenye tanuru la moja, kama haijakomaa, acha uingulie humo na kugeuka majivu!, lakini kama imekomaa, itaibuka ikiwa ni chuma cha pua!.

Baada ya miaka 50 ya utuymwa wa CCM, 2015 hatuhitaji kubahatisha!, we need to be definite sure kuhusu capabilities za Chadema!. Better be sure than sorry!, ndio maana Chadema unapofanya madudu, sisi wengine hatuna huruma hata kidogo, ni bakora kwa kwenda mbele!, hata hao tuwatumainia kwa kuwadhania ndio watatuvusha, lazima wapimwe kwa mkono wa chuma!, na sio kubembelezana kwa kupeana pipi na lawalawa za nyimbo za shangwe na mapambio!, they need to be tasked, tested and approved ndipo tuwape!.

Nasisitiza tena tena tena, ni wale wenye uono finyu tuu ndio wanaoamini kuwa watakao inngiza Chadema ikulu ile 2015 ni wanachama, wafuasi na wapenzi wa Chadema tuu, sisi wengine wote tunao i task, hatuitakii mema!. They are wrong!. Watakao iingiza Chadema ikulu hiyo 2015 (if at all!), ni sisi!, (yes ofcourse pamoja na nyinyi!).
Pasco.
 
Nenda kaisome katiba ya Chadema inasema nini kuhusu uchaguzi wa ndani!. Nyie ndio sisi tunaowaita "washabiki maandazi!" mnaipenda Chadema kwa upendo upepo!.

Utakuta mtu mzima na akili zake anashabikia uchaguzi wa ndani wa Chadema usogezwe mbele for justified reasons!, lakini utashangaa mtu huyo akisikia uchaguzi mkuu umesogezwa mbele kwa mwaka mmoja ili kuisubiria smooth transition ya katiba mpya kwa CCM kuendelea kutawala mwaka mmoja zaidi!, atapiga kele kwa kupaza sauti mpaka mbunguni!.
Pasco.
 
mchezo umeisha,kumbe hata wapiga kelele wapo kama sie..........safi sana mleta mada
 
Nyerere alikuwa mwenyekiti mpaka akaona chama kimekomaa.
 

Pasco ntake radhi mimi sio shabiki maandazi wa CDM Bali ni full member. Kama watu wamekubaliana kwa kufata taratibu baada ya upembuzi yakinifu kufanywa kuna shida gani? NAJUA WEWE SIO MAGAMBA lakini mbona wa shabiki maandazi wengi wa B7fc wanalalamikia sana CDM kuhairisha uchaguzi?
 
You are missing the point dude!

Tatizo sio kuwepo au kutokuwepo kwa kipengele.

Tatizo ni utaratibu unaotumika kuingiza na kutoa vipengele pamoja na kauli za UONGO zinazotolewa na viongozi waandamizi wa chama kulaghai watu juu ya utaratibu huo.

Cdm haiendeshwi na wanalumumba au kauli za ikulu na vibaraka wenu,sahau kabisa hizo suala kuna taratibu zao kichama na wala si kwa mashinikizo,mwambie aliyekutuma umewakosa akupe buku saba yako tu ukakojoe ulale
 
Mkuu Khakha, naomba unisamehe!, unajua humu jf sasa mashabiki wa Chadema wamejaa sana hadi kwen ye msafara wa mamba, huwezi jua kenge ni yupi!.
Pasco.
 
Weka ushahidi kama kilikuwepo sio kubwabwaja tuu
 
Mkuu Khakha, naomba unisamehe!, unajua humu jf sasa mashabiki wa Chadema wamejaa sana hadi kwen ye msafara wa mamba, huwezi jua kenge ni yupi!.
Pasco.

Ahahaha, nimekusamehe mkuu Pasco wa JF.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…