Katiba ya Tanzania inatamka watu wote kushitakiwa kwa mujibu wa sheria. Kwanini CCM inataka kuwapa kinga TISS?

Kama wewe nifisadi jiandae lakini Kama nimtu wa kawaida uwe na amani mkuu lengo la hii Sheria ni

kuiondoa SERIKALI ILIYO NDANI YA SERIKA
Kama bado uko hai ndugu yangu sheria zote zinatungwa kwa ajili ya kumkandamiza mtu wa kawaida kama hujui. Fisadi anaogopwa. Kwa Tanzania fisadi yuko salama kuliko wewe wa kawaida.

Rejea report zote za CAG inawataja watu wengi kukwapua mamilioni ya Watanzania,lakini fisadi gani au kiongozi umeona amechukuliwa hatua. Lakini wewe wa kawaida jaribu kupatikana na nyama kilo moja ya swala uone mvua zitakavyokunyeshea. Unafikiri hao vigogo hawa vigogo wanakula nyama gani sana?.

Jaribu leo kwenye mtandao kuongea ukweli mbaya fulani kuhusu kiongozi fulani. Kama hujatafutwa na hao wasiojulikana. Na ndio hao wanawekewa kinga hata wakikupa kilema wewe wa kawaida huna pa kwenda. Kama hujui kwa nchi hii wa kawaida ndio daima wenye kutungiwa sheria,ndio wenye kuandamwa
 
Kwa maoni yangu, hawa watu watajiwekea kinga nyingi sana. Ila pia ni funzo kwetu sisi wapiga kura wao kwamba hayo ndiyo matunda ya kazi tuliyoifanya kipindi cha uchaguzi. Kwa hiyo, kwa upande mwingine tufurahi kwamba hayo ndiyo matunda ya kura zetu. Shida inayokuja kwangu ni kwamba kama hao watu wanatenda haki, kinga zaidi ni ya nini? Au huwa hawatendi haki? Kama hawatendi haki wanastahili wachukuliwe hatua za kisheria. Kuongeza kinga "kwa makosa yanayoweza kutendeka wakati wa utekelezaji wa majukumu..." maana yake ni kuruhusu ukiukwaji wa sheria wakati wa utekelezaji wa sheria. Kama sheria zinafuatwa, hayo makosa yatatendekaje wakati wa utekelezaji wa majukumu? Kuweka kinga kwa maoni yangu kunaongeza mwanya wa kukiuka sheria wakati wa utekelezaji wa majukumu/sheria. Pili, kuongeza kiwango cha adhabu kulingana na uzito wa kosa ili kuendana na mazingira ya sasa hakuna maana yoyote. Kwani mazingira ya sasa ndiyo yanayohitaji kiwango kikubwa cha adhabu? Sheria ingesema law enforcers waongeze ufanisi katika utekelezaji wa majukumu yao. Ufanisi ndio unaotakiwa na wala siyo kinga wala kiwango cha adhabu. Lakini kuongeza kinga kuna maana kuweka mwanya wa kukiuka haki za watu wanaohisiwa kuwa wametenda kosa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…