Katibu Mkuu CCM (Chongolo) amtaka Waziri wa Maliasili na Utalii, Pindi Chana kujiuzulu

Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Daniel Chongolo amemtaka Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk Pindi Chana kuachia nafasi hiyo na kuruhusu mamlaka za uteuzi zifanye maamuzi mbadala, iwapo ameshindwa kudhibiti changamoto ya tembo wanaoharibu mazao ya wananchi wilayani Meatu katika Mkoa wa Simiyu.

Kauli hiyo ya Chongolo imekuja baada ya miezi mitatu tangu Rais Samia Suluhu Hassan alipoiagiza Wizara hiyo kushughulikia changamoto hiyo.

Katika maelezo yake alipokuwa ziarani Wilaya ya Meatu mkoani Simiyu leo Jumatano Juni Mosi, 2022, Chongolo amesema kuwapo kwa changamoto hiyo hadi sasa ni ishara kwamba Wizara husika imekaidi au kudharau maelekezo ya Rais.

"Hatuwezi kuwa na watu wanaoagizwa na Rais juu ya kuchukua hatua hawafanyi wanakaa ofisini, hii inaleta matatizo kwa wananchi na inaonyesha dharau kwa aliyekuagiza," amesema.

Amewahakikishia wananchi ndani ya mwezi mmoja uongozi wa wizara hiyo utakwenda eneo hilo kwa ajili ya kutatua changamoto hiyo.

Ameongeza kuwa CCM haitaridhia kuona wananchi wanateseka ilihali kiliomba ridhaa ya kuwaongoza vyema.
 
Attachments

  • CA803AF0-2BCD-47F2-BB52-7825473B426D.jpeg
    CA803AF0-2BCD-47F2-BB52-7825473B426D.jpeg
    50.2 KB · Views: 11
Apumzike tu huyo mama, hyo wizara na huyo mama hapana!
 
Sio kazi yako nawe mwachie rais aamue. Suala la tembo sio Meatu tu
Kazi yake ni ipi, unaijua wewe?
Sasa kama "suala la tembo si Meatu tu" hiyo ndiyo iwe sababu ya kutolishughulikia?

Watu wengine mna akili za tope kwelikweli.
 
Chana Kaichana Maliasili. Ngoja akakae benchi kwenye michezo ya Utamaduni na Ngoma za asili huko Basata
 
Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Daniel Chongolo amemtaka Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk Pindi Chana kuachia nafasi hiyo na kuruhusu mamlaka za uteuzi zifanye maamuzi mbadala, iwapo ameshindwa kudhibiti changamoto ya tembo wanaoharibu mazao ya wananchi wilayani Meatu katika Mkoa wa Simiyu.

Kauli hiyo ya Chongolo imekuja baada ya miezi mitatu tangu Rais Samia Suluhu Hassan alipoiagiza Wizara hiyo kushughulikia changamoto hiyo.

Katika maelezo yake alipokuwa ziarani Wilaya ya Meatu mkoani Simiyu leo Jumatano Juni Mosi, 2022, Chongolo amesema kuwapo kwa changamoto hiyo hadi sasa ni ishara kwamba Wizara husika imekaidi au kudharau maelekezo ya Rais.

"Hatuwezi kuwa na watu wanaoagizwa na Rais juu ya kuchukua hatua hawafanyi wanakaa ofisini, hii inaleta matatizo kwa wananchi na inaonyesha dharau kwa aliyekuagiza," amesema.

Amewahakikishia wananchi ndani ya mwezi mmoja uongozi wa wizara hiyo utakwenda eneo hilo kwa ajili ya kutatua changamoto hiyo.

Ameongeza kuwa CCM haitaridhia kuona wananchi wanateseka ilihali kiliomba ridhaa ya kuwaongoza vyema.
[emoji38][emoji38][emoji38][emoji38]
 
Sasa pale ccm ni waziri gani anapaswa kusifiwa kwa kazi nzuri na wananchi wafurahi maana kila waziri anapaswa kuachia ngazi naona kila waziri anavimeo kibao
Bashe
Mwigilu
Pindi chana
January
Nape
Tamisemi
Elimu
Kila kona kuna malalamiko sijui chongolo anataka kumwambia nn Rais
 
Huyu naye hamnazo,ameshindwa kuhoji ujio wa lile dege kubwa na kupakia wanyama wetu,anakimbilia kumwambia ajiuxuru kwa vitu vya kipuuzi,
 
Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Daniel Chongolo amemtaka Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk Pindi Chana kuachia nafasi hiyo na kuruhusu mamlaka za uteuzi zifanye maamuzi mbadala, iwapo ameshindwa kudhibiti changamoto ya tembo wanaoharibu mazao ya wananchi wilayani Meatu katika Mkoa wa Simiyu.

Kauli hiyo ya Chongolo imekuja baada ya miezi mitatu tangu Rais Samia Suluhu Hassan alipoiagiza Wizara hiyo kushughulikia changamoto hiyo.

Katika maelezo yake alipokuwa ziarani Wilaya ya Meatu mkoani Simiyu leo Jumatano Juni Mosi, 2022, Chongolo amesema kuwapo kwa changamoto hiyo hadi sasa ni ishara kwamba Wizara husika imekaidi au kudharau maelekezo ya Rais.

"Hatuwezi kuwa na watu wanaoagizwa na Rais juu ya kuchukua hatua hawafanyi wanakaa ofisini, hii inaleta matatizo kwa wananchi na inaonyesha dharau kwa aliyekuagiza," amesema.

Amewahakikishia wananchi ndani ya mwezi mmoja uongozi wa wizara hiyo utakwenda eneo hilo kwa ajili ya kutatua changamoto hiyo.

Ameongeza kuwa CCM haitaridhia kuona wananchi wanateseka ilihali kiliomba ridhaa ya kuwaongoza vyema.
😆😆😆😆
 
Back
Top Bottom