Zanzibar 2020 Katibu Mkuu CCM, Dkt. Bashiru ashangaa watu 12 kujitokeza kutaka urais Zanzibar, adai wengine wanatumika na mabeberu kutaka kuvuruga nchi yetu

kasahau ccm bara 2015 kulikuwa na watia nia 42?!
Kwa akili yake aliona vyama 42 ndani ya ccm?!
 
Gambino,
Ni kweli mtu kama Jecha anataka kuharibu taswira ya nchi yetu kwenye mataifa mengine.
1. Jecha ameamua kuwakomesha (anataka deal) kwa sababu hawakurudisha hisani baada ya kuwaondolea dhahama ya Maalim Seif 2015.
2. Hussein Mwinyi hakubaliki Zanzibar licha ya kuonekana anabebwa kuwa Makamu II kisha aje kugombea urais wa Muungano 2025.
3. Profesa Mbarawa anayeandaliwa na JPM kuwa Rais wa Zanzibar hakubaliki huko kwa kuwa hana base ya kisiasa Zanzibar.
4. Hao wengine wana-protest mipango ya utawala wa Magufuli kutaka ku-impose surrogate president kisiwani Zanzibar.
 
Na huyu nae ana PhD tena ya siasa ?
 
Alijuaje idadi kuwa wako 12 ?
 
Bashiru Ally haamini ktk demokrasia ndani ya CCM CCM Tanganyika?

CCM Zanzibar wameamua kutoa nafasi sawa kwa wanaCCM WaZanzibari.

CHADEMA pia imeamua wanaCHADEMA ruksa kutia nia Urais .

CCM Tanganyika imebaki kundi pekee lisilokubali ushindani ndani ya chama.
30 August 2018
12 Mnatafuta Urais Zanzibar! Katibu Mkuu Wa CCM, Dkt Bashiru Ally Amesema Anawajua Wanasiasa na Baadhi ya wanachama Wa CCM Zanzibar Wanaozunguka Zunguka Kabla Ya Muda Kuwania Kiti Cha Urais Wa Zanzibar.
 
Hata wakiwa 100 hakuna tatizo, ndio demokrasia.. Mbona somo la demokrasia ni gumu sana kwa binadamu.
 
Hivi huku bara 2015 watia nia ndani ya CCM kugombea urais walivyofika zaidi ya 40 walikua wanatumiwa na wakina nani? Mabeberu au Majike?
Huyu jamaa anazingua
 
SISI TULIOHAMIA CCM KUTAFUTA DEMOKRASIA MBONA MNATUYUMBISHA?
 
ni haki yao ya kikatiba, kwa mtu yeyote akijiona anasifa mwache achukue form.
tena kwa maoni yangu 12 ni wachache waache wafike hata 100 , si baadae watashindanishwa na hatimaye atapatikana mmoja
 
Nina uhakika Jecha amefuata chenji yake ya uwekezaji aliofanya 2015 kumzuia Maalim kuapishwa urais wa Visiwa vya Karafuu.
 
Mimi ni mkristo nataka nikachukue fomu ya uraisi Zbar je inawezekana maana Huseni Mwinyi ni mtanganyika kachukua fomu kule.
 
Mwambie sasa hivi wamefika 22
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…