Tetesi: Katibu Mkuu CCM, Kinana kujiuzulu Novemba 2016?

Tetesi: Katibu Mkuu CCM, Kinana kujiuzulu Novemba 2016?

Status
Not open for further replies.
Katibu mkuu CCM taifa Kinana anatarajia kujiuzulu mwezi Novemba mwaka huu ambapo mkutano mkuu wa NEC taifa utakaa amesema hayo kufatana na kutoridhishwa na mwenendo wanaofanyika ndani ya chama kutomridhisha.

Alisema muda wingi amekuwa akitoa ushauri lakini haufanyiwi kazi amedai kuwa kuna matatizo mengi ameyafikisha kwenye serikali likiwepo la kusimamishwa ajira waajiriwa wapya walioajiriwa May 2016 lakini halijafanyiwa kazi alidai ameiomba serikali kutatua hatima ya hawa wahanga lakini haijafanya hivyo alisema na migogoro ya watumishi wa umma kuhusu madai hayo na matatizo mbalimbali ambayo jamii inakabiliwa bado hayatekelezwi amedai na amesema hayo ameomba kuachia ngazi ili kuwapa nafasi wengine wajaribu kuongoza hicho chama cha ccm.

Chanzo: Mwanahalisi
dcdb0ef5e5f3ebe3f460df9df758a7af.jpg
wewe mwanahalisi uwongo ndio ibada? kama kujiuzuru ni muda mrefu aliomba apumzike
 
Hakuna tatizo hata kidogo. Kama waliweza kuhama chama waliokuwa mawaziri wakuu, tena katika wakati mgumu wa kipindi cha kampeni za uchaguzi, kusitokee mpasuko, itakuwa kuhama leo mtu mmoja?
 
Magufuli kama anataka kujenga nidhamu lazima aanze na chama chake maana ndo chanzo cha matatizo yooote tuliyo nayo kama taifa.
 
Siasa mchezo usiotaka hasira pia. ..mihemuko itapandisha presha bila sababu
 
Umeongea mengi ukasahau unaemsifia kanunua ndege wakati hospitali hazina chanjo na madawati ni ya kuombaomba. We ndo bado hujamwelewa.

Unachosubiri kuhusu mahakama ya mafisadi ni ndoto. Utang'amua hilo punde.
Kwani maana ya kuwa na wizara ama mawaziri kazi yake nini wale wamewekwa kwa ajili ya kusimamia yanayowahusu sasa kukosekana kwa madawa hosp hapo rais anaingiaje hivi mbona hampendi kutumia hizi asilimia 99% zilizobaki hata nusu yake kufikiri ? Hamkawii kumwamwia aje awasongee ugali majumbani kweni miafrika ndivyo tulivyo.
 
NOSENSE WW SI UNA NDUGU ZAKO WAPO AMBAO HAWANA AJIRA WANATAABIKA OVYO WW UNALALA LUMUMBA UNAJISAHAU
Ndugu nikuambie kitu mimi sio ccm na haitokaa itokee kuwa ccm hiyo ndio nira yangu Rais ni binaadamu mwenye moyo wa nyama kama wako na mwenye hofu ya Mungu kama ilivyokuwa wewe nakuuliza kaswali kadogo tu ulitaka woote waliomaliza vyuo waajiriwe kwa mfumo gani mzuri alioukuta mfano viwanda vikubwa na vidogovidogo sekta kwanza mfumo wenyewe wa elimu ni wa kufumuliwa usukwe upya wewe mtu anakwambia amesoma mpaka chuo kikuu ana masters hata kufuma kitambaa hajui inabidi elimu ya sasa mtu akimaliza shule kuanzia sekondary mpaka chuo kikuu awe na maarifa na ujuzi wa kitu chochote kutokana na wakati tuliopo ili tuweze kukimbiza gurudumu la maendeleo sio kila kitu rais rais hivi nyie wasomi wa hii nchi mmeisaidia nini Tanzania kazi kulialia tu humu .
 
Ccm hawatetereki ki hivyo, hawa watu wanajua kujipanga kumaliza mambo yao kwa kweli
 
Hili gazeti ni kama la The Sun ama News of the world lilomgharimu Rupert Madorch malaki ya pounds kwa kuandika uongo, hapa magazeti kama hili na Uhuru tunayaita "Toilet Rugs" maana yanaandika habari zisizo na ukweli ili kuuza takataka zao. Mwanahalisi ililiandika habari za Lowasa kifasaha sana alipokuwa CCM na watu wa Lowasa wa CCM waliliita takataka, leo limebadilika linamsifia Lowasa yuleyule na watu walewale wa CDM waliounga mkono kuhusu habari za kashfa za Lowasa wanaunga mkono habari za kumsifia Lowasa. Ndiyo ujue dunia inaharibiwa na waandishi uchwara ndiyo maana watu kama kina Donald trump wameweza hata kupitishwa kuwa wagombea urais sababu na matakataka kama haya ya mwanahalisi.
Kweli kabisa
 
Serikali inashauriwa na Bunge siyo Chama! Wabunge wa Chama husika ndani ya Bunge ndiyo wanatakiwa kujenga hoja ya kuituma serikali!
 
Source yenyewe mwana halisi??

Tambala la kusafishia Mafisadi
 
Huyu kesha pima joto, yale mambo yetu yale hayana kwa kupitishia maana port pamebana wamekaba hadi penati.Acha na vile viumbe vipumue kidogo.
 
ww ni ccm haikusaidii hebu fikria ndugu zako wanavyopata shida ww si upo lumumba
Mimi nimezungumzia gazeti sasa hiyo ccm imetoka wapi? Ukiniita mimi Lipumba kwa kusema ukweli basi wewe uitwe mtu uliyeazimisha ubongo wako kwa wanasiasa na ni aibu kwa mtu mzima kutotumia uwezo aliopewa na mungu kuamua lipi Zuri na lipi baya kwa kupelekeshwa na wanasiasa kama umeazima akili za wale watalii wanaozuru kwa makundi pale masai mara na serengeti
 
Mzee Kinana, tuwe wakweli ni jembe. Alisaidia sana kukipa uhai CCM baada ya mtangulizi wake mzee Wilson Mukama kuelekea kumshinda. Hivyo kwa watu makini, lazima wamshukuru sana Mzee kinana, anayebeza labda hana kumbukumbu. Alifanya kazi kubwa na ya ziada. Falsafa yake kubwa ilikua ni mikutano kwa wananchi, na kwa hilo alifanikiwa.
Mkuu ukweli ndio huo mimi si wa team mapangaboi ila huyu jamaa huyo kwa siasa za fitina hana mfano yuko vizuri sana na ccm itawachua muda mrefu sana kumpata mtu wa kariba ya Kinana.
 
Uliotajwa nili
ww ni ccm haikusaidii hebu fikria ndugu zako wanavyopata shida ww si upo lumumba
ulisoma nilichoandika ama umekurupuka kama watendaji wa magufuli. Inaonekana uelewa wako ni mfinyu sana mimi sipo hapa kusemea upande wowote kama wewe. Ccm wakiboronga nawalima vilevile cdm na kama unajua kusoma na kuandika kiswahili nimeyasema magazeti yote ya propaganda ya ccm na cdm. Lakini utaelewaje wakati wewe unaangalia upande moja tu
 
Rais Magufuli go hakuna kugeuka nyuma usijekuwa jiwe la chumvi sauti za kukubeza, kukuzomea, kukusengenya zitakuwa nyingi tena zitaongezeka kadri siku sitakapo kwenda lakini nakusihi kamwe usigeuke nyuma huko kuna walaghali, wafilisi, mafisadi, wenye jicho la husda wabinafsi wenye roho mbaya wahujumu uchumi songa mbele kwenye nchi ya ahadi na Mungu atakutangulia amini hivyo.
Mmmm huu ni wimbo wa kusifu na kuabudu hebu lete ile pambio nyingine.
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom