Fundisi Muhapa
JF-Expert Member
- Nov 25, 2013
- 4,422
- 2,112
Umeongea mengi ukasahau unaemsifia kanunua ndege wakati hospitali hazina chanjo na madawati ni ya kuombaomba. We ndo bado hujamwelewa.Mimi sio ccm lakini ukweli utabaki kuwa hivyo kwa jinsi hii nchi ilivyokuwa imefikia mahali kubaya hata angeshuka malaika bado mngemwona ni mlaghai kuna watu walikuwa wakiishi kama wao ndio Mungu aliowakabidhi hii nchi na familia zao tu wengine tuliishi kama wakiwa tusie na mahali pa kusaidiwa matatizo yetu hii nchi ilifika mahala ukienda ofisi za serikali kutaka huduma ambayo ni haki yetu mtu ulikuwa ukikaripiwa kama mtoto mdogo tena wengine wakitoa lugha chafu na kuonyesha dharau kama vile umeenda kumwomba akuongezee damu ya kukuongezea siku za kuishi,
Ilifika kipindi mama mjamzito akienda kujifungua uhakika wa kurudi yeye na mtoto wakiwa salama ni kama kukutana na tembo posta acheni hizo bana Magufuli karejesha heshima mliozoea kukesha bar mkijua kesho mtapata nyingine za kugonga kutokana na michongo mlioijua nyie sasa hiyo kitu hakunaga na kama kuna michongo ipo ole tusiwakamate mkafanye kazi mpate hela kihalali sio kuishi maisha ya kitapeli tapeli tu ndio maana nchi haiwezi kwenda na kasi ya maendeleo kutokana na kila mtu kujaza mawazo kichwani ya rushwa, wizi na mambo yafananayo nayo,
Mtamwelewa tu we ngoja mahakama ya mafisadi ikamilike vyema ndio mtajua kama yupo seriously hakuna binadamu aliyekamilika hata kama ana mapungufu ukiwa kama mwananchi mzalendo wa Tanzania umeisaidia nini Tanzania kusukuma gurudumu la maendeleo tuache kulialia kwa pamoja tunaweza pepo la lawama na lishindwe tusonge mbele.
Unachosubiri kuhusu mahakama ya mafisadi ni ndoto. Utang'amua hilo punde.