Katibu mkuu CWT agoma kurudi Temeke kufundisha

Huyu jamaa atajutia uamuzi wake wa kukataa UTEUZI.

Pia alishindwa kusoma upepo hata kama alinusa harufu ya kutotendewa haki.

Nina imani alikuwa kashakusanya maokoto angerudi fast kwa mwajiri halafu akaendelee na kazi huku akipanga namna ya kusimika mipango ya kuendeleza maokoto yake.

Ona sasa yupo hatarini kufilisiwa na kukosa kazi kabisa
 
Mbona huyo Dinna waliyegoma naye kwenda kuapishwa yeye haadhibiwi? Hii ni double standard. Nchi ya kipuuzi sana hii inayopenda kulipiza kisasi ndio maana imelaaniwa kwa sababu za kishetani kama hizi.
Dinna aliapishwa na yupo ofisini kama DC kule Kigoma
 
Some people are smart; inawezekana jamaa alishakusanya kimyakimya alichovuna huko CTW saa hii yupo zake Boso anaendeleza maisha yake kwa utulivuuu. Najaribu kuwaza tu
 
Hii inaonekana ni vita
Kwani yeye mwenyewe amesema ana shida na hiyo kazi?
 
Some people are smart; inawezekana jamaa alishakusanya kimyakimya alichovuna huko CTW saa hii yupo zake Boso anaendeleza maisha yake kwa utulivuuu. Najaribu kuwaza tu
Hata kama ni hivyo, amekosea.

Ilitakiwa arudi kwenye kituo chake cha kazi cha mwanzo then baadae angeweza kuacha kazi kwa taratibu zinazoeleweka na asingepata taabu ambayo anaenda kuipata sasa.

Ila humo CWT inaonekana kuna maokoto ya bwerere sana, sio kwa mtifuano huo
 
Aliyekuwa Rais wa CWT ndio nasikia alikubali/alihudhuria kuapishwa/uapisho
Yule anaitwa Leah Ulaya. Waliogoma ni Dinna na Maganga. Kwanini Dinna haguswi anakomaliwa Maganga tu? Ipo namna hapa sio bure. Serikali kuna mahali inajichanganya yenyewe kwenye maamuzi yake kwa sababu uovu wao umeshikwa pabaya.Kwanini serikali inaingiza siasa CWT kila mwaka kutaka kuingiza mamluki ili wachote pesa za walimu? Wamezoea kuchota.pesa kwenye mifuko ya hifadhi ya kamii na NHIF. Kule CWT wamekosa kuingia wanakuwa wakali. Kwani nyie serikali hizo hela ni za kwenu hadi mtake kuzipora? Mungu anawaona!
 
Naona bora Maganga aachane nao, kina cha maji ni kirefu asije akapoteze vyote bure
 
Kwani bado alikwenda ofisi za CWT kama Rais/Katibu Mkuu wao.Au nako ameacha kwenda.Ukaguzi maalum ufanyike kuhakiki mali na fedha za wanachama.Ukionq kiongozi haendi likizo au hataki kuachia uongozi,ujuwe kuna makandokando au masilahi binafsi ni makubwa,ukilinganisha na masilahi ya umma
 
Pay ya Maticha imewapa kiburi sana! CWT ni dude fulani dhulmati viongozi wake hujiona kama miungu
 
Ametakiwa yeye arudi kituo chake cha kazi, hawezi kujitetea mbona mwenzake hajarudi, atekeleze alichotakiwa kufanya
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…