TANZIA Katibu Mkuu Kiongozi, John W. Kijazi afariki dunia

Poleni familia, Wahamasishe watu wachukue tahadhari sana. Wanaotaka kujifungia wajifungie, wengine tahadhari kubwa.

Rais kubali Chanjo za Pfizer zitapunguza vifo.

Hospitalization.
Rais huyu?
 
Naongea kwa uchungu sana sio kwa ajili ya hawa viongozi wawili kufariki kinachoniuma watu pamoja na elimu zao kubwa kwa uwoga kabisa walishindwa kumshauri mzee kwenye hili please unakosea na usalama wa taifa wanafanya nini? walishindwa kumwambia mzee huu mchezo ni hatari? uwoga gani huu? hawa wameondoka kwa kiasi fulani wanawajibika na vifo vyao walikebehi wavaa mask hata ugonjwa. huku mitaani ndio shida. bado walirundika vijana katika matamasha hayana kichwa wala miguu sijui serengeti festival mikutano ya hovyo tena kwa sifa, vijana hawaumwi hata wanafunzi sio sana ila wanasambaza kwa kasi. please shutdown schools na hawa wanaofanya maamuzi ya kizembe wawajibike. this is series wafunge midomo yao kupotosha watu mpaka ufiwe na wa kwako ndio uone kuna shida.
 
Kuchukua tahadhari hadi uambiwe na serikali? Are u serious?
Tahadhali ya nini wakati baba yako unayemsifu na kumuabudu kasema Tanzania hatuna Corona? Mnayesifu na kuabudu "This unscientific and unreasonable Devil", mnashiriki kusababisha vifo hivi. Kilangila.
 
Na mkewe nasikia pia hali siyo nzuri pale MNH
Sio mkewe tu please nenda Hosp zote za Tanzania uwone wagonjwa wanavyopigania maisha yao, halafu una waziri wa afya anafanya utani na viclip vyake huku anacheka, una katibu wa afya anatembea na kupiga picha hakuna wagonjwa wako wa tatu wengine kawaida tuu wanasukari. sukari? mamilioni ya watu wana sukari miaka yote tumeona haya? katibu wa afya kama yuko na anaogopa Mungu basi angetuma barua ya kujiuzulu, wasiri wa afya angesema samahani na angeachia ngazi. sisemi kama ni hawa tu tatizo ila itakuwa mwanzo wa kuanza upya katika hili. wajitoe kafara basi.
 
Mwalimu Nyerere aliwahi kusema "Hatuwezi kuyashinda matatizo yetu kwa kujidanganya kwamba hayapo". Tuendelee kuchukua hatua, tuendelee kujilinda. The situation is alarming. Kwaheri Balozi Kijazi.!
Tuna hitaji alie apa kuilinda katiba na watu wake atoe tamko leo!!!!
Hatuwezi kuendelea kuona Watanzania wana kufa kwa uzembe wa mtu mmoja.
 
Kwa hali hii; tutanyoa sana vipara mpaka viote sugu. RIP Balozi Engineer Kijazi. Mungu awalinde watoto na nduguze. Amina.
 
Asee ipunguze punguze hao wajuu kwanza kabla ya kufika kwetu wanyonge.
Asee mkuu bado hujajielewa wanyonge gani nenda sehemu zenye baridi huko Moshi na Arusha ndo utaona watu wanavyopukutika.
 
Kuchukua tahadhari hadi uambiwe na serikali? Are u serious?
Unajuwa kazi ya serikali ni nini?? kazi yao kutoa miongozo sahihi kulinda wananchi wake wizara ya afya kazi yake nini? kula mananasi?? wakati tatizo lipo wao wako busy waziri na katibu wa afya kwenda katika media kupiga mapicha kuwa hatuna shida wako wagonjwa watatu tu wengine wana sukari na pressure tu, unatuma ujumbe gani kwa watu? watu wameanza kuvaa barakoa bila kuambiwa ila wao viongozi wa serikali hawataki kuvaa wanatuma ujumbe gani? wanashindwa kufunga shule maana watoto wako strong ila hawa ndio watawaletea magonjwa home na vijana. mimi nimesha zuia mtoto wangu kwenda shule mimi binafsi na liwalo liwe ila serikali inafanya nini? kazi yao nini? kula mananasi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…